AMKA BABA

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Najua huwezi kumzidi kura mkeo; kura za nani ni bora kati ya baba na mama, lakini angalau ukaribiane nae kidogo kura kuliko kupata sifuri. Mwanamke (mama) hujizolea kura zote za Upendo kwa watoto kwa sababu ana Upendo kweli, anajali na ni mjanja pia ili kukuzidi kura.

#1. Ukirudi kutoka kazini hakikisha unaonana na watoto wako hata kama umechoka vipi. Ila kama wamelala waache wapumzike. Ongea nao kama rafiki yao. Piga nao stori kuhusu masomo yao na mambo yaliyojiri mchana kutwa hapo nyumbani na uwadokeze kidogo kuhusu mwenendo wa kazi yako. Anza nao tangu wangali wadogo ili wajue unapataje pesa. Ukiwa ni rafiki yao ni rahisi wao pia kukushirikisha usiyoyajua kuhusu wao.

#2. Usikubali kuwa askari na mahakama ya familia. Kila kosa watendalo wanao basi wewe ndio mahakama na mtoa adhabu mkuu. Usikubali mkeo alifanye jina lako liwe jehanamu kwa wanao, kila kosa linafikishwa kwako. Sina maana kuwa usiwaadhibu wanao, la hasha, adhabu ziwepo ila usigeuke kuwa mahakama na askari wa familia yako.

#3. Jifunze kutoa pesa za matumizi mbele ya wanao ili wajue kuwa unaihudumia familia. Iwe ni pesa ya chakula, bill za umeme, maji na hata pesa za ada na mavazi ya wanao. Tafuta credits hadharani ili wanao wajue mapema kuwa wewe ni baba unaewajibika. Hata ukitolea pesa chumbani, hakikisha unawauliza wanao iwapo walipata mahitaji yao kwa wakati. Maswali kama; Umekula? Umeshiba kabisa? Viatu vimekutosha? nk. Hii itaonesha kuwa kuna nafasi umeshiriki katika huduma unayouliza.

#4. Unaporudi na zawadi nyumbani, iwe matunda au vitu vingine, hakikisha wanao ndio wanakupokea. Ikitokea umepokelewa na mtu mwingine basi hakikisha kuwa unawauliza wanao iwapo waliipata zawadi hiyo uliyoileta na uwaulize kirafiki iwapo waliipenda au lah.

#5. Toka nao out mara moja moja ili kuRefresh mind na kuweka kumbukumbu ya happy moments wakiwa na wewe. Ukiwa nao out, hakikisha kuwa unashiriki vema out hiyo na ikiwezekana cheza nao (iwapo ni wadogo) na ziwepo picha za kumbukumbu ya outing zenu.

#6. Mara moja moja kaa nao na uwape nafasi ya kuchangia mawazo kwenye baadhi ya mipango ya familia iwapo umri wao unaruhusu kuchangia mawazo. Hii itawafanya wajione kuwa umewajali na kuwathamini pia hata kama mawazo yao ni dhaifu.

ANGALIZO:
Watoto wako kutojua magumu unayopitia katika kutafuta pesa ni marks kwa mkeo. Kutafuta michepuko nje ya ndoa ni marks kwa mkeo. Kutopata muda wa kukaa na wanao ni marks kwa mkeo. Anachokupigia bao mkeo kwa watoto wako na mwisho wa siku unaonekana hukuwalea hao watoto ni LOVE, CARE & CONCERN anayowapa mama yao.

Sasa we endelea kujidanganya kuwa jukumu lako ni kutafuta pesa tu. Ukirudi kutoka kazini unaoga, unakula, unasikiliza kesi, unawaadhibu watoto na kisha unalala. Fainali uzeeni. Wakati mkeo anaenda likizo kwa wanao, wewe utabaki nyumbani kulinda nyumba.
 
Hata uwafanyie nini bado mama yao atakuwa no 1,cha msingi nikuishi na mama yao vizuri, ukiwa na amani na mke wangu na watoto watajua umuhimu wako.

Kinachowabadilisha ni sumu wanayolishwa na wake zetu pindi tusipokuwepo, hata ukitoa kipato chako chote kama huna maelewano mazuri na mama yao bado utachukiwa tu.

Cha msingi wanawake waache kuwalisha watoto sumu, unawaambia watoto wadogo mambo mabaya kumhusu baba yao.
 
Mke ana wajibu wa kujenga taswira nzuri ya mume wake au baba kwa watoto wake regardless..ukiona hafanyi hivyo imekula kwako..
 
Usikubali kuwa askari na mahakama ya familia. Kila kosa watendalo wanao basi wewe ndio mahakama na mtoa adhabu mkuu. Usikubali mkeo alifanye jina lako liwe jehanamu kwa wanao, kila kosa linafikishwa kwako. Sina maana kuwa usiwaadhibu wanao, la hasha, adhabu ziwepo ila usigeuke kuwa mahakama na askari wa familia yako.
hili huwa tunalichukulia kawaida sana lakini lina athari sana kisaikolojia kwa watoto.
 
mambo mengi uliyoyataja hapo sikuwanafanyiwa na baba yangu lakin still nimejua kuwa baba ndio aliemfanya mama akaonekana bora bila hata kuambiwa na mtu yani kuna mda tu ukafika nikaelewa kuwa baba ndio kila kitu kwenye famly mama ni mtekerezaji tu...
respect qako father...
 
Najua huwezi kumzidi kura mkeo; kura za nani ni bora kati ya baba na mama, lakini angalau ukaribiane nae kidogo kura kuliko kupata sifuri. Mwanamke (mama) hujizolea kura zote za Upendo kwa watoto kwa sababu ana Upendo kweli, anajali na ni mjanja pia ili kukuzidi kura.

#1. Ukirudi kutoka kazini hakikisha unaonana na watoto wako hata kama umechoka vipi. Ila kama wamelala waache wapumzike. Ongea nao kama rafiki yao. Piga nao stori kuhusu masomo yao na mambo yaliyojiri mchana kutwa hapo nyumbani na uwadokeze kidogo kuhusu mwenendo wa kazi yako. Anza nao tangu wangali wadogo ili wajue unapataje pesa. Ukiwa ni rafiki yao ni rahisi wao pia kukushirikisha usiyoyajua kuhusu wao.

#2. Usikubali kuwa askari na mahakama ya familia. Kila kosa watendalo wanao basi wewe ndio mahakama na mtoa adhabu mkuu. Usikubali mkeo alifanye jina lako liwe jehanamu kwa wanao, kila kosa linafikishwa kwako. Sina maana kuwa usiwaadhibu wanao, la hasha, adhabu ziwepo ila usigeuke kuwa mahakama na askari wa familia yako.

#3. Jifunze kutoa pesa za matumizi mbele ya wanao ili wajue kuwa unaihudumia familia. Iwe ni pesa ya chakula, bill za umeme, maji na hata pesa za ada na mavazi ya wanao. Tafuta credits hadharani ili wanao wajue mapema kuwa wewe ni baba unaewajibika. Hata ukitolea pesa chumbani, hakikisha unawauliza wanao iwapo walipata mahitaji yao kwa wakati. Maswali kama; Umekula? Umeshiba kabisa? Viatu vimekutosha? nk. Hii itaonesha kuwa kuna nafasi umeshiriki katika huduma unayouliza.

#4. Unaporudi na zawadi nyumbani, iwe matunda au vitu vingine, hakikisha wanao ndio wanakupokea. Ikitokea umepokelewa na mtu mwingine basi hakikisha kuwa unawauliza wanao iwapo waliipata zawadi hiyo uliyoileta na uwaulize kirafiki iwapo waliipenda au lah.

#5. Toka nao out mara moja moja ili kuRefresh mind na kuweka kumbukumbu ya happy moments wakiwa na wewe. Ukiwa nao out, hakikisha kuwa unashiriki vema out hiyo na ikiwezekana cheza nao (iwapo ni wadogo) na ziwepo picha za kumbukumbu ya outing zenu.

#6. Mara moja moja kaa nao na uwape nafasi ya kuchangia mawazo kwenye baadhi ya mipango ya familia iwapo umri wao unaruhusu kuchangia mawazo. Hii itawafanya wajione kuwa umewajali na kuwathamini pia hata kama mawazo yao ni dhaifu.

ANGALIZO:
Watoto wako kutojua magumu unayopitia katika kutafuta pesa ni marks kwa mkeo. Kutafuta michepuko nje ya ndoa ni marks kwa mkeo. Kutopata muda wa kukaa na wanao ni marks kwa mkeo. Anachokupigia bao mkeo kwa watoto wako na mwisho wa siku unaonekana hukuwalea hao watoto ni LOVE, CARE & CONCERN anayowapa mama yao.

Sasa we endelea kujidanganya kuwa jukumu lako ni kutafuta pesa tu. Ukirudi kutoka kazini unaoga, unakula, unasikiliza kesi, unawaadhibu watoto na kisha unalala. Fainali uzeeni. Wakati mkeo anaenda likizo kwa wanao, wewe utabaki nyumbani kulinda nyumba.
point ya msingi ni kutafuta pesa na kuweka akiba ya kutosha ili usitegemee huruma ya watoto uzeeni
 
mambo mengi uliyoyataja hapo sikuwanafanyiwa na baba yangu lakin still nimejua kuwa baba ndio aliemfanya mama akaonekana bora bila hata kuambiwa na mtu yani kuna mda tu ukafika nikaelewa kuwa baba ndio kila kitu kwenye famly mama ni mtekerezaji tu...
respect qako father...
Chukua hatua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom