Amiri Jeshi mkuu wa Tz ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amiri Jeshi mkuu wa Tz ni nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyange, Mar 25, 2010.

 1. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Jan, tar. 12 tulishuhudia askari wetu wakipita mbele ya mgeni rasmi Mh. Karume wakitoa heshima kwa mkuu. Lakini Mh. mwingine ambaye ni Rais wa jamhuri ya Muungano wa TZ alikuwepo.
  Mpaka leo sipati jibu kuhusu amiri jeshi mkuu ninani? na kwanini Mh. wa Zanzibar ndiye alikuwa mkuu, wakati mkuu kabisa alikuwepo? au labda hivi vyeo ni vya kupokezana kwa muda? Wataalam wa protokali tueleweshe.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hayo ndo mambo ya Ki-TZ. Mambo yetu mengi hayafuati sheria, bali yanaendeshwa kwa uwiano, kwa compromise.
   
 3. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Inawezekana hicho cheo hakimo kwenye mambo ya muungano.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  usikute amirijeshi mkuu alikuwa kwenye hitima akamuagiza amuwakilishe
   
 5. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Umeshasema kwamba askari walikua wanatoa heshima kwa mgeni rasmi....sasa swali lako la nn tena?
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ngoja nijaribu na kujaribu sio kushindwa

  Amiri Jeshi Mkuu J .M. K
  Amiri Jeshi Mkuu Msaidizi A .A. K

  Ila nadhani sasa imefika muda KATIBA yetu sasa ijadiliwe upya mikanganyiko kibao jamani
   
 7. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  umeichekesha sana mkuu............... kweli mamabo yanavyoenda shaghalabagala nchi hii................... hayo yalianza toka enzi za mkapa na dr salmini............. mi naconclude kuwa ni ukosefu wa ushupavu wa uongozi............. katiba waliyoapa kuilinda wanaiangalia tu..................
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Mar 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hata mie niliwaza hivyo mwanzoni, kuwa jamaa alikua mkekani akisubiri pilau kwa biliani na soda bariiidi.....
  lakini kumbukumbu zangu za onyesha kuwa alikuwapo pale uwanjani, Karume akikagua.
  swala hapa ni compromise kama mkuu alivyogusi hapo juu, tunawabembeleza Wazenj kama watoto wadogo.
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Hii ni sherehe ya Kijamhuri,kwa hiyo protokali ilitakiwa iwe AAK akague vikosi vilivyo chini yake(mgambo,KMKM,JKU etc)....big boss JMK anakagua yale makubwa(TPDF,POLICE etc)kwa kuwa wanajeshi hutoa kiapo cha utiii wakati wa hizi shughuli....TPDF haiapi kwa AAK
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwenu wanajamvi,

  Amiri jeshi mkuu wa Tanzania ni Rais wa JMT ambae ni Jakaya Mrisho Kikwete.Binafsi nilistuka sana kuona mkuu wa nchi [JMT] anakaa jukwaa na Bwana mdogo Karume anapewa kiapo cha utii.

  Hizi sarakasi zilianza tangu enzi za komando Salmin Amour akiwa Rais wa Zanzibar sasa yamekuwa mazoea tu.Sijui kama kumbukumbu zangu ziko sahihi protokal haikuzingatiwa hata wakati waheshimiwa walipokuwa wanaingia uwanjani na wakati walipokuwa wanatoka.Kawaida Rais anatakiwa awe mtu wa mwisho kuingia kiwanjani,na anakuwa mtu wa kwanza kuondoka kiwanjani lakini hili nalo niliona limegeuzwa kabisa Karume ndiye aliyekuwa wa mwishi kuingia na wa kwanza kuondoka kiwanjani.
   
 11. u

  uvivumwiko Member

  #11
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umesema vema mkuu. Kwa kuongezea ni kwamba katiba yetu in mapungufu hivyo inatakiwa ifanyiwe marekebisho. Pia si sahihi Zenji kuwa na bendera, wimbo wa Taifa na jeshi kwa sababu Zanzibar si Taifa.
   
 12. N

  Nanu JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna Cheo cha Amiri Jeshi Mkuu Msaidizi Tanzania!!!
   
 13. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Jamani Rais JMK alitembelea nchi ya Zanzibar kwenye sherehe ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar..
   
 14. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Nashukuru kwa comments zenu. Kumbe tuko wengi tunao kosa majibu ya swali hili. Labda mhusika wa hii blog atusaidie kui- 'forwad kwa wataalam kama akina Dr. Sira napengine tuikuze ili itusaidie tumpe live mhusika siku nyingine awe makini na mambo ya kiitifaki, pia kukumbushana kulinda Katiba yetu.
   
 15. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kukagua jeshi tu mbona simple sana, hata Masha waziri wa mambo ya ndani huwa anakagua Gwaride la Polisi. Mi naona hapo wanachukulia vitu simple tu bila kujali umuhimu wake katika katiba.
   
 16. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #16
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Wana JF,
  Hili jambo lisitushangaze sana. Ndio maana tunapodai Katiba mpya mara nyingi watu wengi walikuwa hawaelewi. Hali hii haikuanza leo kama mwenzetu mmoja alivyosema ilianza wakati wa Komando Dr. Salmin. Lakini inaenda mbali zaidi. Kwa mujibu wa Katiba yetu, Baraza la Mawaziri linaundwa na i) Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungnao ambaye ni Mwenyekiti, Mhe. Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar, na Mhe. Waziri Mkuu na Mawaziri wote wa Serikali ya Jumhuri ya Muungano. Lakini kwa muda mrefu sasa Rais wa Zanzibar amekuwa hahudhurii Baraza la Mawaziri kama Katiba ya Jamhuri inavyosema. Tatizo, Protokali iwe vipi? Je nafasi ya Rais wa Zanzibar ni ipi hasa...? Ni kweli ni Waziri kama Mawaziri wengine? Je cheo cha Rais kinafutikia wapi? Wakati wa Komando mgogoro huo ulienda mbali zaidi kiasi cha kuhoji "nani humwapisha Rais wa Zanzibar kama mjumbe wa Baraza la mawaziri? Je ni Rais wa Jamhuri au Jaji Mkuu? Kuna migogoro mingi ndani ya Katiba yetu, ndiyo maana wakati umefika maswala haya yanahitaji kujadiliwa wazi na Watanzania. Kuna siku sisi tutakuwa tumeondoka lakini tukawaachiwa watoto na wajukuu zetu mgogoro mkubwa sana ambao hawakuuzalisha na wala bila kujua misingi ya migogoro hii. Kumbe sisi wazazi tumekuwa na Sera ya Mbuni, ya "kujificha kwenye "mchanga" . Kutokutaka kujadili haya mambo yanajenga ufa mkubwa ambao hatimaye lazima tutajenga Ukuta. Rais wa Zanzibar akisafiri nje ya nchi hupigiwa Mizinga kwa heshima yake, huimbiwa Wimbo wa Taifa la Zanzibar, lakini Sera ya nje inasema nchi yetu ni mmoja -Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo haya mambo yanatia wasiwasi huko tuendako. Nawashukuru kwa kuyagundua haya. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
   
 17. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #17
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kikatiba Zanzibar siyo nchi.
  Kama siyo nchi mbona ina Rais??!! .... na kwa vile ina Rais, basi ni nchi.
  Huwezi kusema Rais wa nchi ni kama waziri.
   
 18. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  tatizo ni uzingatifu wa protokali, siyo kukagua tu
   
 19. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Nyange, nimesoma mara kadhaa posting yako bila kupata wazo unalotaka usaidiwe.

  Kuwa amiri jeshi mkuu hakuna uhusiano wowote na kukagua gwaride au kupewa heshima. Na kupewa heshima na jeshi hakuna maana ya kupewa ukuu na jeshi hilo, bali ni kutambuliwa tu kama kiongozi.

  Rais anakuwa amiri jeshi mkuu kutokana na uwezo aliopewa kimadaraka wa kuamuru jeshi liingie vitani...na kwa Tz JK ndio mtu pekee anayeweza kutoa amri hii...sio rais wa Zanzibar.
   
 20. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #20
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
Loading...