Rufiji
Platinum Member
- Jun 18, 2006
- 1,881
- 941
Wana JF,
Hili jambo lisitushangaze sana. Ndio maana tunapodai Katiba mpya mara nyingi watu wengi walikuwa hawaelewi. Hali hii haikuanza leo kama mwenzetu mmoja alivyosema ilianza wakati wa Komando Dr. Salmin. Lakini inaenda mbali zaidi. Kwa mujibu wa Katiba yetu, Baraza la Mawaziri linaundwa na i) Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungnao ambaye ni Mwenyekiti, Mhe. Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar, na Mhe. Waziri Mkuu na Mawaziri wote wa Serikali ya Jumhuri ya Muungano. Lakini kwa muda mrefu sasa Rais wa Zanzibar amekuwa hahudhurii Baraza la Mawaziri kama Katiba ya Jamhuri inavyosema. Tatizo, Protokali iwe vipi? Je nafasi ya Rais wa Zanzibar ni ipi hasa...? Ni kweli ni Waziri kama Mawaziri wengine? Je cheo cha Rais kinafutikia wapi? Wakati wa Komando mgogoro huo ulienda mbali zaidi kiasi cha kuhoji "nani humwapisha Rais wa Zanzibar kama mjumbe wa Baraza la mawaziri? Je ni Rais wa Jamhuri au Jaji Mkuu? Kuna migogoro mingi ndani ya Katiba yetu, ndiyo maana wakati umefika maswala haya yanahitaji kujadiliwa wazi na Watanzania. Kuna siku sisi tutakuwa tumeondoka lakini tukawaachiwa watoto na wajukuu zetu mgogoro mkubwa sana ambao hawakuuzalisha na wala bila kujua misingi ya migogoro hii. Kumbe sisi wazazi tumekuwa na Sera ya Mbuni, ya "kujificha kwenye "mchanga" . Kutokutaka kujadili haya mambo yanajenga ufa mkubwa ambao hatimaye lazima tutajenga Ukuta. Rais wa Zanzibar akisafiri nje ya nchi hupigiwa Mizinga kwa heshima yake, huimbiwa Wimbo wa Taifa la Zanzibar, lakini Sera ya nje inasema nchi yetu ni mmoja -Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo haya mambo yanatia wasiwasi huko tuendako. Nawashukuru kwa kuyagundua haya. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Mheshimiwa Dr. Slaa,
Nikushukuru kwa mchango wako madhubuti, unaonyesha kwa undani kiini migogoro inayoletwa na katiba yetu. Ni jambo la kusikitisha kwamba Bunge letu linashindwa kuyatatua haya matatizo na kutaka kuvirisisha vizazi vijavyo matatizo. Swali la kujiuliza , je muungano wetu utaweza kudumishwa ndani ya hii katiba? Na jee, when everything is set and done, nyie wabunge mtakumbukwa kwa kitu gani ?
Ni jambo la kusikitisha sana kwamba Tanzania sasa inakimbilia kuanzisha East Africa Federation wakati tumeshidwa kutatua matatizo ya Muungano wetu huu. Tumekuwa wepesi sana wa kukimbilia mambo bila ya kuyafanya uchunguzi yakinifu ! Katiba iliyopo sasa haitaweza kuulinda huu muungano na hatima yake utakufa, kama ambavyo muungano wa East Africa utakavyokufa pia ...