Amini usiamini chuma kinaweza kuelea juu ya maji

Amini usiamini chuma kinaweza kuelea juu ya maji

Wana MMU.

Hebu niwashirikishe neno la Mungu kwenye wikiendi hii,najua wengi tunapita katika changamoto mbali mbali lakini Yesu akiwa upande wetu hata chuma kinaelea.

2 Wafalme 6:1-7:
"Wana wa manabii wakamuambia Elisha mahali wanapokaa ni padogo hapatoshi hivyo wakahitaji kutafuta miti ili waongeze nyumba za kuishi lakini mmojawapo akasema "uwe radhi, nakusihi uende nasi" na Elisha akakubali kwenda nao hadi katika mto yordan.

Wakati wakiendelea na kazi mmojawapo akaangusha shoka yake ikazama kwenye mto Yordani, ndipo akalia akasema ole wangu! maana shoka iliazimwa ile, ndipo Elisha akamuuliza iliangukia wapi, akamwonyesha mahali. Elisha akakata kijiti, akakitupa palechuma kikaelea chuma kikaelea akasema kiokote.

Pengine kuna jambo linakusumbua muda huu, na unapiga kelele kuwa 'ole wangu' lakini hebu muonyeshe Mungu pale tatizo lilipo haswa chuma kilipoangukia na utaona muujiza wa Mungu.

Na mbarikiwe nanyi nyote.


Amen kaka
 
amina ubarikiwe na wewe! usiache kutupa ujumbe mwingine maana wengine hata kanisani hatuendi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom