Amini usiamini chuma kinaweza kuelea juu ya maji

Amini usiamini chuma kinaweza kuelea juu ya maji

Mlalamikaji daily

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2014
Posts
1,018
Reaction score
2,365
Wana MMU.

Hebu niwashirikishe neno la Mungu kwenye wikiendi hii,najua wengi tunapita katika changamoto mbali mbali lakini Yesu akiwa upande wetu hata chuma kinaelea.

2 Wafalme 6:1-7:
"Wana wa manabii wakamuambia Elisha mahali wanapokaa ni padogo hapatoshi hivyo wakahitaji kutafuta miti ili waongeze nyumba za kuishi lakini mmojawapo akasema "uwe radhi, nakusihi uende nasi" na Elisha akakubali kwenda nao hadi katika mto yordan.

Wakati wakiendelea na kazi mmojawapo akaangusha shoka yake ikazama kwenye mto Yordani, ndipo akalia akasema ole wangu! maana shoka iliazimwa ile, ndipo Elisha akamuuliza iliangukia wapi, akamwonyesha mahali. Elisha akakata kijiti, akakitupa palechuma kikaelea chuma kikaelea akasema kiokote.

Pengine kuna jambo linakusumbua muda huu, na unapiga kelele kuwa 'ole wangu' lakini hebu muonyeshe Mungu pale tatizo lilipo haswa chuma kilipoangukia na utaona muujiza wa Mungu.

Na mbarikiwe nanyi nyote.

 
Aaaaghh wapi siku hizi hio kitu haipo aiseeee, dunia imejaa dhambi balaaa hata MUNGU mwenyewe kaamua atulie tu sasa maana vinginevyo, atatufanya kitu kibaya. Si unakumbuka mambo ya Sodoma na Gomora? MUNGU alisema, Nitashuka Nikauone uovu wao!!!! Acha kabisa kilichotokea Sodoma na Gomora ni hadithi isisyoelezeka hadi leo. Tumuache huyu mtu ajifiche huko huko tu
 
Asante sana kwa ujumbe mzuri! Mungu ni mwema anaweza yote ila uovu wetu umetuweka mbali na uso wa Mungu kiasi hatuwezi kuona mambo haya yakitokea kwetu. Mungu atutie nguvu!
 
Amina! Asante sana kwa ujumbe mzuri. Mungu anaweza yoteee, ila maovu yetu yametuficha na uso wake hata tusiweze kuona mambo makuu yakitokea kwenye kizazi chetu! Mungu atusaidie tuone tulipokosea tukrekebishe.
 
biblia na quran ni vitabu vizuri sana kwa hadithi.
 
Amini mtumishi,MUNGU wa Elisha ndiye yule yule hata Leo.Kikubwa tuendelee kumtumaini.
Hawa wanataja magari na hawa wanataja farasi, Sisi tunalitaja jina la BWANA wetu.Wao wameinama na kuanguka,Bali sisi tumeinuka na kusimama.(Zaburi 20:7-8).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom