Amini tu nawaambia...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amini tu nawaambia......

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by vukani, Mar 28, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hebu tuangalie mfano huu wa imani kwa kusoma katika kitabu cha Matayo 21:18-22, nitanuku,

  “Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini aliona njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara. Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, jinsi gani mtini umenyauka mara? Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia mkiwa na IMANI, msipokuwa na SHAKA, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yoyote mtakayo yaomba katika SALA mkiamini, mtapokea’

  Kuna watu ambao, kwa sababu ya kukosa kile ambacho jamii inakiona kuwa ndio ufunguo wa mafanikio, huwa wanaamini kwamba hawawezi kufanikiwa au kufanya vizuri maishani.

  Kwa mfano, kwa kukosa elimu, ujuzi au utaalamu fulani, watu wengine hujihesabu kama wanyonge. Huchukulia kwamba ni wale tu wenye elimu, ujuzi na utaalamu fulani ndio wanaoweza au wanaotakiwa kufanikiwa.

  Bila shaka umeshawahi kusikia au hata wewe mwenyewe kusema, “si wamesoma bwana, ndio wanaojaaliwa, sisi ambao hatuna shule kazi yetu itakuwa ni kuwatumikia”. Kauli kama hizi zina chimbuko lake mbali sana, pengine katika malezi yetu.

  Wazazi walizoea au wamezoea kuwaambia watoto wao “Usiposoma, kazi yako itakuwa ni kuwabebea wenzako mizigo”. Kwa bahati mbaya mtoto aliyelishwa “sumu” hii anaposhindwa shule huamini kwamba yeye atabaki kuwatumikia wengine tu.

  Tunapoamini kwamba, kwa sababu hatuna elimu ya kutosha na pengine ujuzi au utaalamu fulani, hatuwezi kufika juu kwenye mafanikio, ni wazi hatutafika.

  Moja ya vigezo muhimu vinavyoweza kutufikisha kwenye mafanikio ni kuamini kwetu kwamba tunaweza kufika huko. Tunapokuwa hatuna imani kwamba tunaweza kufika huko hujifungia njia wenyewe.

  Yesu aliposema “Amin, nawaambia mkiwa na IMANI, msipokuwa na SHAKA, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yoyote mtakayo yaomba katika SALA mkiamini, mtapokea”

  Hakuwa na maana nyingine bali ni kutuhakikishia kuwa kama tukiomba na kuamini, hakuna lisilowezekana mbele ya Mungu, haijalishi una elimu au huna, kinachotakiwa ni sisi kuamini tu, basi.

  Kama kwa kuamini tu inawezekana kuuambia mlima, ung’oke, ukatupwe baharini, na ikawezekana, kwa nini isiwe kwenye kufanikiwa?

  Naamini kila mtu anayo nafasi ya kufanikiwa na kupata kile anachokitaka na ambacho kitampa furaha, ni wajibu wake tu kuomba na kuamini.
   
 2. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa imani yote yawezekana!
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Amen, ubarikiwe kwa neno la imani na kututia moyo....
  Amen, imekuwa na imeshakuwa, ni kwamba tumeshafanikiwa. Amen... tumefanikiwa!!!
   
 4. C

  Cotan Member

  #4
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  ubarikiwe sana.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri kuwapa moyo walokata tamaa, safi best!
   
Loading...