America na Ulaya watu weusi bado wapo, Je uarabuni walitoweka vipi baada ya kukoma kwa Slave Trade?

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Katika historia yetu wazungu pamoja na waarabu katika vipindi tofauti walipokuja Africa waliwachukua watu kutoka Africa na kuwapeleka katika nchi zao kwa ajili ya kufanyishwa kazi na mambo mengine

Lakini baada ya biashara ya utumwa kukoma wazungu hawakuwafukuza waafrica bali waliwatengea maeneo yao maalum na maisha yakaendelea pamoja na ubaguzi na mateso yalikuwa ya hali ya juu lakini hadi leo Amrica na Bara la ulaya kuna watu weusi wengi sana hadi leo hii.

Lakini tukija kwa ndugu zetu waarabu pamoja na wao kuwa na historia ya kuwachukua waafrica wengi zaidi kipindi cha biashara ya utumwa na kuwapeleka kwao uarabuni lakini leo hii 2018, ukizunguka nchi za kiarabu huwezi kukuta wazawa wa kiafrica yaani waarabu weusi ambao bado wanaishi kule na ukiwakuta jua wametoka nchi nyingine either wapo kikazi au wana mambo yao mengine

Maswali yanayokuja je

1)Watu hawa walienda wapi?

2)Waliuawa au walitoweka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikumbuki historia vizuri maana nilikuwa naichukia ila sidhani kama waarabu walipeleka waafrica kwao..maana hakukuwa na shughuli kule( maana hakuna mashamba ni jangwa sehemu kubwa) badala yake walikuwa wanapelekwa kuuzwa kwenye mashamba ambayo yapo nchi za ulaya na america..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu mimi sio mwanahistoria sana kama akina #Humble African# lakini nitajibu navyo ijua historia kulingana na makala nilizosoma.

Vizalia vya waafrika havipo sana uarabuni kulinganisha na America kwa sababu kuu mbili
1. Waarabu wengi waliokuwa wakifanya biashara ya utumwa walikuwa ni madalali tu wa wazungu hasa waliowekeza America maana huko ndio man power ilihitajika kwa kiasi kikubwa kutokana na uzalishaji kwenye mashamba ya miwa na viwanda vidogo vidogo. Hivyo waafrika wengi waliochukuliwa na waarabu waliishia ulaya hasa America.

2. Waafrika walioenda uarabuni waliwekewa ulinzi mkali wa kuzaa na mabinti wa kiarabu, pia kama unavyojua nchi za kiarabu zinaongozwa na Islamic sharia na uzinzi kwa mtoto wa kike ni dhambi kubwa hivyo hakuna zinaa za wazi wazi kama ulaya na America. Pia mabinti wa kiarabu waliozaa na waafrika waliuawa au kutengwa na familia zao na hivyo kuhama. Ndio maana waarabu weusi wapo nchi kama Somalia na zinginezo Afrika na si uarabuni.

Mwisho kabisa waarabu walikuwa makatili kwa kuwaathi wanaume wa kiafrika, waliokuwa watumwa ili wasiwe lijali na kuwaingilia kinyume na maumbile kama wake zao. Hivyo hawakuweza kuzaliana na kuchangamana na waarabu.

Asante mkuu. Watakuja watu wa historia kukazia na kukosoa. Mimi sio mwanahistoria
 
Back
Top Bottom