Amepata stroke baada ya kunifuma na mke wake roho inaniuma sana

Amepata stroke baada ya kunifuma na mke wake roho inaniuma sana

Joined
May 3, 2015
Posts
8
Reaction score
5
Wakuu,

Nimepanga nyumba moja hivi yenye wapangaji watatu, mimi, familia moja hivi na huyu binti tuliefumaniwa nae. Huyu binti kwao Rwanda ni mtusi mumewe ni dereva wa Malori yaendayo Rwanda na alimpata huko huko Kigali wakafunga ndoa na akaja kumpangia chumba hapo tunapoishi.

Jamaa ana miaka 51 na binti ana 27 mimi nina duka hapa hapa kwenye fremu ya mbele, huyu binti alianzisha mazoea ya kukopa vitu dukani kwangu kwa kuwa mumewe ni mtu wa kusafiri muda mrefu binti anaishiwa pesa za matumizi hivyo huja kukopaKatika hali hiyo shetani akatupitia tukaanzisha mahusiano akidai huwa hatosheki kwa mumewe na huwa nampa mahitaji bure.

Sasa sielewi mumewe alijuaje tukiwa chumbani tunafanya tendo la ndoa kwangu nikahisi kuna mtu dirishani anachungulia, kabla sijachomoa nashtukia mtu akipiga kelele ya mwano dirishani huku akiita jina la mkewe na kisha kuanguka kwa kishindo tukavaa tukazunguka kwa nyuma na kukuta jamaa anatoa mapovu huku amejishika kifuani, mwanamke akakimbia.

Mimi nikaita Tax kijiweni nikawaomba masela tusaidiane tukamkimbiza hospitali ya wilaya temeke wakasema ni shambulio la moyo kesho yake asubuhi nilipofika nikasaini makaratasi fulani akahamishiwa muhimbili. Nikàanza kazi ya kutafuta ndugu kwenye phone book nikakutana na jina mama watoto nikaipiga ile namba na kumueleza aliepokea tatizo lililopo.

Akadai yeye ni mke wa jamaa na akasema anaondoka siku hiyo hiyo kuja Dar es salaam maana anaishi Morogoro na akashangaa imekuaje maana jamaa kaondoka Morogoro mzima asubuhi nikabaki nimeduwaa kumbe huyu ndugu ana mke na watoto Moro? Mkewe akafika akawa anamuuguza mumewe muhimbili Icu mkewe sikumweleza chochote maana hajui kama huku kuna mke mwingine.

Sasa zimepita wiki tatu tangu tukio hili, mgonjwa ameondolewa ICU ila amepooza upande mmoja wakati wowote anaweza kutoka mnyarwanda kanipigia simu tayari yupo Mwanza kwa ndugu yake ananiambia niachane na mgonjwa atajua mwenyewe anasema nimtumie hela tukapange sehemu nyingine huwa tunaongea kwa sim kila siku

Wakuu najisikia vibaya sana kwa tukio hili, kwa kuwa chanzo ni mimi pia naomba mnishauri maana mke wa huyu jamaa ananisumbua na maswali kila siku kwamba ilikuaje huyu jamaa akafika hapo alipopata matatizo na kwamba kuna kitu namficha, pia anataka kujua kwa nn siku mbili za mwanzo nilikatalia simu. Ukweli ni kwamba nilifuta SMS zote za mapenzi nikamzungusha zungusha ndipo nikampa siku ya tatu hospital.

Sijawa na amani rohoni ukizingatia kuwa hali ya jamaa si nzuri sana sema tu wagonjwa ni wengi Muhimbili hivyo mwenye nafuu kidogo wanamtoa. Kwa kweli dhamira inanishtaki.
 
Mwambie ukweli mkewe ufiche mpk lini...

Mwambie ulikua na hawara wake akakufumania unakula utamu
 
Wewe huna Mke? Huyo mzinzi Mwenzio hana ubinadamu, Wala usijione wewe bingwa kitandani ulikua unaliwa vyako, Achana na huyo kituko anaekwambia mkapange, jitahidi kumsaidia Huyu Mke wa jamaa kwani ww ndio sababu...
 
Kuendelea kujiweka kwa huyo binti ni kuendelea kujichimbia kaburi..hebu fikiria kama ameshindwa kuonyesha utu japo kidogo kwa mumewe huyo wewe ndio atakujali upepo ukibadilika? Mke mkubwa wa huyo jamaa wala usifanye haraka kumwambia,muache amuhudumie mumewe kwanza
 
Dunia ina mambo toka kitambo....... enzi hizo unatambaa na beat na mistari yenye vina aah sorry jamaa we mkule huyo mnyarwanda lakini kumbuka ukiona mwenzako ananyolewa zako tia maji.
 
Huyo mzee mwenyewe alikuwa anamuibia mkewe. We lipia gharama za hospital hapo na huduma nyingine kwa uwezo wako, maybe it will ease the guilt. Huyo manzi mpotezee kabisa.


Kuhusu kumwambia mkewe sijui nini we endelea kupotezea tu, wataelezana wenyewe.
 
Hutakiwi kumwambia chochote
infact ili huyo jamaa aweze kupona unapaswa pia kupunguza kuonana na huyo jamaa
ili usimuongezee machungu.....
 
aiss ushapigwa kipapai tayari subiri jamaa apone arudi Kongo utaona kitakachofuata!
 
wahi kwa mchungaji haraka ukaombe rehema kwan yeye yupo kwa niaba ya mungu ivyo atasisima kukuombea kwa mungu. na hapo ndipo vakuwa umesamehewa hata mbinguni. lkn pia cha muhmu zaidi ni kumpa yesu maisha yako. la sivyo na ww ukioa tu utafanyiwa ivyoivyo. "www.heaven.jesuschrist.com"
 
Sasa ukimwambia mkewe naye akapata strock utafanyaje? Mambo mengine unakausha tu as long sio nduguyo wala jirani haitokuwa shida kiivyo, nyie vibabu na nyie mtulie mzeeke vzr na wake zenu, mxiiuuuuuu zenu!
 
Mkewe usimsambie, ila pia achana na huyo mwanamke maana ni zimwi na hospital punguza kwenda akikuona atakuwa anaumia
 
Mwambie huyo mama kuwa ulimsaidia tu ka jirani yako hivyo tangu uanze safari za Muhumbili biashara yako haiendi tena hivyo nafasi ya kuja Muhumbili kila siku huna.
Mwachie mzigo wake pale, nenda dukani, fanya kazi kwa bidii. wasiliana naye kwa sm tu. Ka ana hitaji la pesa, mtumie tena kwa tishio kuwa akipona aje kulipa ili atumie kwa uangalifu.
Akipona, utaamua kumtoza au kumsamehe. Ila usiendelee kwenda pale hospital. Jamaa aweza rudi ICU akikuona na mkewe tena huku akijua kuwa weye ni kipanga. Pia aweza kudhani umesha mwambia mkewe ujinga wake na mnyarwanda.
Akipona kabisa amwambie mkewe kama hana akili zake, ila si wewe kutangaza
 
Yeye anakosa kwa kuwa na mchepuko wakati ana mke na watoto. Wewe unakosa kwa kusarandia kidumu cha mtu na hatimae kumpa "Stroke" mwenye kidumu. Suluhu ni jamaa atulie na mke wake, na wewe achana na huyo mwanamke, kama mwenzio kafanyiwa hivyo leo, kesho wewe utakuja kufanyiwa kibaya zaidi.
 
Ukiua kwa upanga utauliwa kwa upanga subiri kua mpole malipo utayapata hapa hapa duniani..usisite kuja kutujulisha ata kama ni mwaka 2030 Mungu atuweke hai.
 
Dunia haina huruma..! Huwa always nasemaga hivo.! Malipo si wajua ni humu humu kwa walimwengu eeeeeeeeeeehh kama ni shetani alikuingia ukamgegeda mwasi wa mshkaji mpaka akapata stroke wait for your turn.! "Quid pro quo"
 
Back
Top Bottom