Amenizidi miaka miwili

Amenizidi miaka miwili

banalunda

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
231
Reaction score
67
Habari wanajamvi!
Nimeingia kwenye mahusiano mapya mda si mrefu sana ila kiukweli ninampenda huyu binti na yeye pia ananipenda, wakati tunaanza kufahamiana tulianza kuwa marafiki tunaoheshimiana sana, na huyu binti ana heshima sana, tulipoaza kujuana alinitajia umri wake ambao ni miaka miwili zaidi ya umri wangu, ila yeye hajui kwani nilimwambia nimemzidi mwaka mmoja, so hivyo ndivyo anavyjua, sasa tunaendelea vizuri mno ila kinachonipa wasiwasi je, mnadhani hili swala la umri linaweza kuwa kikwazo kwangu kuwa na mwanamke aliyenizidi 2years?
 
Duh; gia ya kwanza unaanza kwa kudanganya umri?
 
mapenzi bwana ya mibongo lazima muanze kwa uongo...sasa bora uwe open mapema
 
Huyo kwako ni bibi

Mwanaume unatakiwa umzidi mwanamke miaka 5 na isizidi 15years
 
We jimwayemwaye tu hayo mambo ya umri ni minor
 
Kama umempenda kiasi cha kutaka kufunga pingu za maisha, basi hilo la kukuzidi miaka miwili lisikunyime raha hata kidogo. Kumbuka kupata wachumba miaka hii ni ngumu sana kama umeridhika naye basi we songa mbele tu.
 
Endelea kumdanganya tu kwani nani atamuambia?
Ila kama ulimkubali mwanzoni, sasaivi unashtuka nini?
 
Duh; gia ya kwanza unaanza kwa kudanganya umri?

manake kama vile umepelekwa kituo cha polisi bongo. hapo lazima uanze kwa kudanganya kwani polisi
wa bongo hawaamini mtuhumiwa unaweza sema ukweli bila kipondo kwanza. hivyo ukianza kwa kuwaambia
ukweli utakosa cha kuwaambia baada ya kipondo kwani lazima kipondo ukipate.
 
Duh!kwanza husipende sana kudanganya ni bora kusema ukweli ukakosa na ukawa huru kuliko kusema uongo na kuendelea kuwa mtumwa kwa ulichodanganya.

Inategemea una malengo gani na yeye kama shida ni kugegeda,piga sepa zako yaan umri sio nshu!

Na kama unamalengo ya kufanya nae maisha yaan kuwa wife pia umri sio nshu kwani si zani kama wewe utaoa umri!

Kila la kheri mkuu,na happy new year!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kuna watu wana 'uongo-liasis'
hata sehemu ambazo hazihitaji uongo wao wanapata cha kudanganya.

Mtu akinidanganya umri, natupa!
 
kuna watu wana 'uongo-liasis'
hata sehemu ambazo hazihitaji uongo wao wanapata cha kudanganya.

Mtu akinidanganya umri, natupa!

Kongosho heri ya mwaka mpya jamani.Sasa kama nitaka first imprition iwe umri nifanyaje,hata ukigundua baadae umeshakolea huwe nitupa,utasema miaka ni namba tu ha ha ha ha
 
Habari wanajamvi!
Nimeingia kwenye mahusiano mapya mda si mrefu sana ila kiukweli ninampenda huyu binti na yeye pia ananipenda, wakati tunaanza kufahamiana tulianza kuwa marafiki tunaoheshimiana sana, na huyu binti ana heshima sana, tulipoaza kujuana alinitajia umri wake ambao ni miaka miwili zaidi ya umri wangu, ila yeye hajui kwani nilimwambia nimemzidi mwaka mmoja, so hivyo ndivyo anavyjua, sasa tunaendelea vizuri mno ila kinachonipa wasiwasi je, mnadhani hili swala la umri linaweza kuwa kikwazo kwangu kuwa na mwanamke aliyenizidi 2years?
Sio mbaya lakn mwambie ukweli ili kama na yeye ana amani muendelee kwa raha zenu.
 
he he he, kama tumeshakula tundi ntafanyaje?

Nakuwa mpole.

Kongosho heri ya mwaka mpya jamani.Sasa kama nitaka first imprition iwe umri nifanyaje,hata ukigundua baadae umeshakolea huwe nitupa,utasema miaka ni namba tu ha ha ha ha
 
Back
Top Bottom