Masanilo
Platinum Member
- Oct 2, 2007
- 22,286
- 4,493
John na Sauda wamekuwa marafiki machoni kwa wanajamii kwa muda mrefu. Lakini hivi karibuni wamekuwa na ugomvi usiyo na maelezo. John alikuwa akishirikiana na Sauda kwenye biashara zao na hata tuliowengi tuliamini kuwa huenda ni wapenzi. Kama Mchungaji, John amekuja nishirikisha sababu ya ugomvi wao! Katika kuchakachua nini kilichotokea John anadai alimkopesha dada Sauda Sh 500,000 aongezee kwenye biashara yake, lakini kila akimkumbushia amrudishie imekuwa shida na anaambulia matusi. Na imefikia hata hawawezi kuongea tena. Kwa muda wangu nilimtafuta chemba Sauda kumuuliza kulikoni ugomvi na John, Sauda alinijibu huyo kaka amekuwa kama ndugu yangu, amenishangaza hivi karibuni amenitongoza kitendo hicho kimenikera sana sitaki hata kumsikia. Nikamuuliza hivi ni kweli alikukopesha pesa fulani? Sauda alibadilika rangi Rev Masanilo nakuheshimu mimi nitaifa kubwa kwa siku natumia 100,000 kwa vocha iweje nimkope huyo Shs 500,000/=? Mwambie anikome na asinifuate fuate mimi si wa hadhi yake. Wachungaji tuna viswali vyetu, baada ya kumbana sana alikuabali ni kweli alimkopa John na atafanya juhudi amlipe! Ameamua kumwaga radhi na kusingizia jamaa amemtaka kimapenzi ili kuuwa soooo!
NB Kina dada kwanini mnasingizia kutongozwa hata pasipostahili?
Rev Masa K
NB Kina dada kwanini mnasingizia kutongozwa hata pasipostahili?
Rev Masa K