Amegundua vidonge vya ARV's chumbani kwa mpenzi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amegundua vidonge vya ARV's chumbani kwa mpenzi wake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ngaliba Dume, Jul 19, 2011.

 1. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Ni mshikaji wa muda mrefu!Tulifahamiana Tabora School(Boys) miaka iyooo.Tulipendana sana sbb 2likuwa tukiishi room moja,hata baada ya kumaliza tuliendelea na Elimu ya juu tena kwa Mafanikio makubwa. Jamaa yangu ni mtalaam wa i minara ya simu ktk kampun flani ya simu apa Tz,ana mpenz wake ambaye jamaa yng ana nia kabsa ya kuoa..uyu dada(shemej yangu)ni mkaguzi(Auditor)..."wanapendana sana"...lakn kama wiki imepta Mwanamke alpata likzo,akamua toka kwao kuja kukaa kwa rafk yngu kwa mda..ktk kipindi iki jamaa yangu aligundua ktk mkoba wa mpenz wake kuna "kadi",maelekezo na namna ya ku2mia vdonge vya kurefusha maisha,msichana hakuwah kumwambia jamaa wala ata sisi atukuwah kujua...japo kuna wakat walikuwa wanataka kwenda kupma ila mwnmke akawa relactant...jamaa anashndwa atamuanzaje mwanamke kumuliza mana alpekua tu mkobani bila ruhusa. Sabab mi n rakfye kanishrksha,jamaa kachanganyikiwa mpaka baadh ya kazi za kwenda kurekebsha minara watu wapate netwek kaziweka pending...yaan kachzka!TUNAFANYAJE?Mana mjini kushakuwa kuchungu..huzun yake n huzuni yangu! NAWASILISHA:
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kuwa muathirika sio mwisho wa maisha wanaweza wakaishi kama mume na mke na wakapata watoto hata kama mmoja wao ni muathirika, lakini hilo lazima iwe choice ya jamaa na kama yeye hataki kuoa muathirika basi asimwambie kama ameona ARV's bali amsisitize waende wakapime kabla ya kuendelea na mahusiano

  By the Way umemaliza Boyz mwaka gani?
   
 3. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Thanx VoiceofReason nimekpata ushauri wako...nazd kujfunza!1990's ndo boyzia nimepta!vp na wewe mazngra ayo nin?
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wapo watakaouliza huyo jamaa yako alikuwa akitafuta nini kwenye mkoba wa mdada. Watasema kufukunyua fukunyua mikoba ya wadada ni kujirusha roho bure tu.

  Binafsi naona mdada hakuwa 'forthcoming' kuhusiana na hivyo vidonge kama ni vyake au la. Inasikitisha lakini ndo hivyo tena, mtu utafanyaje sasa. Jamaa ni apige moyo konde, aongee naye apate kujua kinachoendelea halafu achukue hatua atakayoona inamfaa.

  But I must confess, finding such pills in your lady's purse can be devastating....
   
 5. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa. Hili gonjwa ni balaa. Sasa mpaka anatumia dawa manake alishaugua huyo binti. Kwa kifupi ni muuaji angekuwa na upendo wa kweli angemwambia mwenzie ili kumnusuru who knows labda angejua mapema angepona. Lets hope jamaa hajaukwaa. Jamani nyie mlio single pimeni afya kabla ya kuingia kwenye mahusiano na si ndoa tu.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  And it will never be the same!!!!
   
 7. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dah!..................kweli inachanganya sana...

  1. Wewe kama rafiki wa karibu.......zidisha ukaribu kuliko mwanzo.............rafikio yupo kwenye shida kubwa sana.
  2. Sina hakika kama walipoanza mahusiano walipima vvu kabla ya kujamiiana.....kwa hiyo hakuna wakumlaumu mwenzake
  3. Kama ambavyo VOR amesema hapo juu,jamaa amshauri mwenzake waende kupima.............baada ya hapo.............watapa ushauri namna ya kuishi
  4. Simshauri kumuacha kwa kuwa kama itaonekana tatizo wote wanalo.............na umesema wanapendana............si sahihi yeye kwenda kutafuta ambaye hajaathirika.......na kuendeleza maambukizi.
  5. Kama ataamua kumuacha iwe kwasababu nyingine na si hii ya kuathirika................ajiulize angekuwa ni yeye yuko katikati ya mahusiano....halafu akajigundua ameathirika........angefanyaje?
  6. Kuwa muathirika sio mwisho wa maisha...........ni mwanzo wa maisha ya kujitambua zaidi................endelea kumpa moyo.
   
 8. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Thanx mkuu for your talented advice...thats why i feel proud of JF!Siwez kumtenga,sitaweza!tumetoka mbali sana....na apa napokwambia na mpango nchukue ata likizo ata tuende Zenji kupumzka!...I wl take y advice in a seriously manner
   
 9. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nashindwa kumlaumu huyu dada kwa kuwa;
  .........hatujajua kama walipima kabla ya mahusiano
  .........hatuna hakika nani kamwambukiza mwenzake

  Pengine..............walianza mahusiano blindly...........dada hajijui na kaka hajijui..............baadae dada kupima akajikuta kaathirika.........akajaribu kuvuta kumbukumbu zake za mahusiano ya nyuma............hakuwa anatumia kinga........hivyo akahisi labda yeye ndie chanzo na kuamua kufanya siri akihofia kuvunja mahusiano.....Kumbe labda kaka nae huko nyuma ndie aliye vibeba......

  NB:Kuambukizwa si kwa njia ya ngono pekee.
  Naomba nisilaumu yeyote hapa,hata kama yuko wa kulaumiwa,.....si wakati wake huu.....haitawajenga kuface tatizo.
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Akapime/wakapime kama dada akikubali alafu akishapata majibu ndo aamue nini cha kufanya.

  Inawezekana dada kambebea mtu tu akajisahau navyo.
   
 11. k

  kisukari JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  pole sana kwa huyo kaka,kama huyo dada ni muathirika,kiukweli alikuwa na mapenzi ya kinafiki.mapenzi gani hayo ya kutokuambiana jambo kama hilo?kuogopa kuachwa?juu ya yote,ipo siku ingejulikana tu,kwa nini umuangamize mwenzio kimawazo{maana lazima ujihisi kuchanganyikiwa}mmmh,kuambukizana kimakusudi sio jambo zuri.mungu atamsaidia anaweza akawa negative,kikubwa akapime
   
 12. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli nataka kuchangia ila namna yako ya kuandika kiswahili... haki naumia kichwa maana ni kama unaandika codes.
  Nitarudi nikielewa kupitia ushahuri wa wengine.
   
 13. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Pole sana RR...Haikuwa dhamira yangu wewe usiielewe hii thread...lengo la thread hii ni kupata ushauri kwa Wana-JF na wewe ukiwemo! Kutokuielewa thread sabab ya codes kumepnguza idad ya ushauri,ushaur wako ulikuwa muhmu sana,pengne endelea kufatlia utajielimisha na utanipa nasaha zako!POLE KWA KUKUWEKA KANDO KWA UANDSHI WA KISWAHL CHANGU (little I hv been addicted wth codes)
   
 14. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kitendo cha binti kuficha kadi/vidonge kuna maanisha alikuwa muathirika toka mwanzo kabla ya uhusiano na jamaa yako na ameanza kumeza dawa baada ya CD count kushuka sana,pia inathibitisha amekuwa akienda kujuwa hali yake mara kwa mara.Hapa hamna cha ushauri wala kumung'unya maneno jamaa akapime kama ameathirika.Vyovyote atakavyokuta huyu mwanamke si wakuendelea nae.
   
 15. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Litakuwa jambo la busara sana..............mshauri naye aombe likizo ili peformance yake isishuke......................
  Pia usimsisitize kwenda kupima kwa sasa.....................unahitaji kupata ushauri wa kumrudisha kwenye normal state kwanza..........
  alafu ndio aanze kushauriwa kupima.....................
   
 16. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ballerina sikubaliani nawe kuhusu kuchelewa kupima,sehemu ya kupima ina washauri wazuri wenye utaalamu na pia kuchelewa kunazidi kumchanganya akili na anaweza kupima na kukuta hana.Kuna rafiki yangu walienda kupima yeye akakutwa anao na mpenzi wake hana na walikuwa hawatumii condom zaidi ya miezi sita ya uhusiano wao.
   
 17. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Halafu ikumbukwe kuwa ukimwi uligundulika nchini miaka ya 80 mwanzoni..................(uligundulika.....sio ulianza).

  Kuna wale waliozaliwa miaka hiyo na wazazi waathirika...............ambao walizaliwa wameathirika..................................
  Wapo ambao immunity zao ziko juu na wanaishi mpaka leo tena ni mabinti/wavulana wenye mvuto hasa.

  NB:Si kila mvulana aliyetulia au msichana bikra hana maambukizi ya VVU............ni muhimu kupima kabla kuanza mahusiano.
   
 18. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kupima hata mahospitali ya binafsi yanapima....................ila kwa kutoa ushauri wengine hawana hata muda......utafikiri anakuambia ukapime malaria................nimemshakumbana nao kama mara mbili...................sipendi kuzitaja hizo hospitali.

  Yaani unamwambia docta,mimi ningependa kupima na vvu..............anakuuliza tu "umewahi kupima".......unamjibu hapana......anauliza tena "kwanini unataka kupima" ....unajibu nataka kujua afya yangu.............anakwambi, "ok....nimekuandikia tayari.....watakupima"!.................hivi hapo kakushauri nini?

  Mimi nilimaanisha apate ushauri nasaha ambao utamuweka sawa ndio akapime..............mara nyingi AMREF wako makini na wanawashauri nasaha wazuri sana.
  Akikurupuka na kwenda private hospital, sitanii....tunaweza kumpoteza iwapo atajikuta ameathirika kwani atakuwa ameongeza stress.
   
 19. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sio Amref tu hata Muhimbili kama yuko Dar au hospitali za Mkoa ua Wilaya ni kweli hospitali nyingi za binafsi hawaipi uzito swala la ushauri kabla na baada ya kupima.
   
 20. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Tusimlaumu huyu dada , labda alikuwa anasubiri muda muafaka kuongea na mwenzake!
   
Loading...