Amefanya kila njia nizae naye

Amefanya kila njia nizae naye

Sio mke wa mtu tu hata girl friend wako akikuambia mzae atalea unatakiwa ujiongeze maana shilingi hugeuka kwani hata hawa tunaowasikia wanalalamika wazazi wenza hawaleti matunzo sio wote wametelekezwa wengine waliomba wenyewe na wengine walitegesha.
 
Wadau habari,

Mimi ni kijana wa Makamo nna maisha mzuri tu na sijaoa. Sasa kuna Dada mmoja tulikaa naye mtaani(familia zetu) baada ya muda mrefu tumeonana nae nae baada ya mimi kuhamishiwa kikazi Mwanza.

Uyo dada kaolewa na ana muda mrefu kwenye ndoa lakini hajabahatika kupata mtoto... kwa kuwa tulikuwa tunafahamiana huko nyuma basi tumekuwa marafiki wa kawaida tu.

Siku za hivi karibu amewatuma rafiki zangu kama wa nne hivi waje waniombe nizae nae.. mi nikawa nachukulia utani. Baada ya muda kupita kamtuma mdogo wangu wa kiume akiomba aje aniambie jambo lilelile. Mimi sikuchulia serious muda umepita kanivaa mwenye mkavu kaniomba nimsaidie nimpe mimba tu.

Baada ya kuhoji kuhusu mumewe , akaniambia yupo ila wamejaribu imeshindikana na mumewe ni mtu mzima. Uyo dada kuonyesha yupo serious kuna kiasi cha pesa anata kunipa (pesa ndefu), nilipo muuliza mumewe akijua kasema hawezi kujua maana siri ya mtoto ni Mama, na mumewe alisha wahi kuwa na watoto wa2 huko nyuma na mwanamke mwingine kabla ya kufunga naye ndoa. Hivyo mumewe kizazi anacho ila ndo hajui tatizo kwa nini hapati mimba.

Weekend hii amekuja na picha za nyumba anasema zinauzwa nichague aninunulie kama zawadi nikikubali kumpa mimba, tatizo mimi nafahamika kwao na uyo dada maana familia zetu zinaishi jirani.. na kitu dada anaona mimi nafanana kidogo na mume wake, hivyo hata mtoto akizaliwa hakuta kuwa na issue sana. Kumbuka mimi pia nna position nzuri tu Serikalini, nawaza hii issue mbeleni uyo mwanamke hawezi kuitumia kama siraha kwangu ya kunichafua.

Wadau naomba ushauri nile mtego na chambo wake au niendelee kupotezea, au nichukue pesa au nyumba nikamilishe mchezo na mke wa mtu?
Maisha ndo haya haya..... Hadi umeandika huu Uzi lazima Kuna kitu unafikilia........ Fanya kile ambacho unafikilia....... Na kama utakubali akikupa nyumba iuze nunua nyingine mahali pengine maan ya mbeleni hatuyajui
 
Msome Equation hapa chini, ana maoni mazuri sana juu ya hilo jambo.

Umetupa na. Mfano kabisa
 
Kama ana pesa ya kukununulia nyumba IVF inamshindaje? Balaa linaloweza kukukuta huko mbeleni utarudi hapa kutusimulia.
 
In Vitro Fertilisation au IVF. AI iko zaidi kimifugo mifugo

Kwa sasa ni sehemu ya suluhisho kwa matatizo mengi ya infertility kwa wanandoa au wenye kuhitaji kupata watoto kwa mtindo huo/bila kuhusisha mzazi wa pili moja kwa moja/baba.
 
Kama ana pesa ya kukununulia nyumba IVF inamshindaje? Balaa linaloweza kukukuta huko mbeleni utarudi hapa kutusimulia.

Hata kama hana hela ndefu IUI ni rahisi zaidi. Ukilinbanisha na njia anayowazia. Nadhani ni kwa kuwa watu hawana taarifa sahihi. Labda kama wamefanya zote pia bila mafanikio, ingawa ingekuwa ngumu kurudi nyuma. Labda kwa faida nyingine pia??
 
Ewe mtumishi wa umma. Kwa niaba ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nakusihi ukatae rushwa. Rushwa ni adui wa haki na maendeleo !

Usikubali kudhalilisha utumishi wa umma kwa kujipatia mali kwa njia isiyo halali kinyume na maadili ya kanuni za utumishi wa umma !
 
Hata kama hana hela ndefu IUI ni rahisi zaidi. Ukilinbanisha na njia anayowazia. Nadhani ni kwa kuwa watu hawana taarifa sahihi.
IUI ni kitu gani mkuu, naomba elimu
 
IUI ni kitu gani mkuu, naomba elimu
Msingi mkuu: unafanya vipimo kuangalia lini yai linaachiwa/ovulation. Anafanyiwa na hormones analyaia kama yuko sawa.

Kila kitu kikiwa sawa, zinachukuliwa mbegu toka kwa mume au donor yeyote kulingana na tatizo kwa upande husika. Mbegu huoshwa kitaalamu na kuwekwa kwenye mju wa mimba na mimna kutungwa ndani ya mji wa mimba.

IVF mbegu hukutanishwa nje ya mji wa mimba, ambayo ni more complex na ghali. Ila njia poa itategemea na tatizo la msingi la wahusika pia.
 
Kwa sasa ni sehemu ya suluhisho kwa matatizo mengi ya infertility kwa wanandoa au wenye kuhitaji kupata watoto kwa mtindo huo/bila kuhusisha mzazi wa pili moja kwa moja/baba.
Ni kweli na amshauri tu huyu waende na mumewe wakapandikize mimba.
 
Back
Top Bottom