Ameathiriwa na malezi ya utotoni?

Mine eyes

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
6,464
7,140
Hili ni tatizo au ni nature ya mtu..?

Wanajamvi naombeni maoni /ushauri wenu kwa hili.

Dada ninayemfata kuzaliwa ni ana sijui niseme tabia tofauti .na kwa mujibu wa wazazi hali hii ilimtokea siku moja baada ya kuchapwa na baba kipindi hicho akiwa bado ni mtoto wa miaka 5.
Alilalamika sana kwamba kaonewa lakini hakusikilizwa....kachezea fimbo na lakini si baba wala yeye hakuna aliyesema ni kwa nini kachapwa!
Kwamba hata mama alipo taka kujua sababu hakupata jibu ,basi toka hapo
akaanza kubadilika kwa kasi ,ule ucheshi,ucheza na furaha na kucheka mda wote ikawa kinyume!
Si nyumbani yaani popote alipokwenda ile ikawa ndio muonekao wake mpya ,baadae sana mpaka walimu na wazazi na ndugu waliingilia kati kuhusu hili lakini haikusaidia maana mpaka hivi ukubwani yuko vile vile na ukimuuliza sana sababu yeye kubwa ni kulia na labda akwambie hajui kwa nini au akutizame tu!
Yeye huwa haongei mpaka alazimike sana,anakaa masaa mengi peke yake kajiinamia ,hapendi ukaribu au kelele wala mjumuiko wowote,halafu ana aina fulani ya kutizama kitu au mtu ambayo ni ngumu kuitafsiri,sasa ana miaka 31 anafanya kazi na anaishi peke yake hana mpango wa ndoa wala bf!
Tumejaribu sana kumsaidia mpaka watu wa tiba lakini hakuna mabadiliko,inaniumiza sana kwa vile nahisi kuna kitu kinamsumbua bila yeye kujua au ni nini..??
 
Huyo atakua na pepo mana kma kuchapwa ndio kumfanye akose furaha ni maajabu makubwa....kuna wa2 wamelelewa n mama wa kambo wenye roho za kishetani yani kipigo na kulazwa njaa still wko na furaha kwenye maisha yao.....mcheki mshana jr achungulie kwenye GPS yke
 
Huyo usijekukuta mzee alimu abuse na stick akapigwa, na ni kosa kubwa sana kutokumsikiliza mtoto anachotaka kusema, kwa kawaida mtoto akikosea ukimchapa atakiri , ukiona bado anabisha hajafanya ujue asilimia kubwa hajafanya kweli, hilo jibu analo mzee wako na muhusika mwenyewe
 
Nimejikuta navutiwa na aina ya maisha alio chagua kuishi huyo ndugu yako aiseeee.....
Mkuu,
Wewe unaona kama dada yako ana maisha flani ya hovyo. Lakini kiuhalisia minaona dada yako amechagua aina flani ya maisha yasio na kero kwenye hii Dunia.
Yaani wewe una muhurumia, wakati yeye anaona kabisa kwamba hiyo aina ya maisha anayo ishi ndio bora kuliko maisha mengine yeyote hapa duniani..
 
Hii imekaa kiroho zaidi. Initiative mnayotakiwa kuchukua ni kubwa ili kurescue huyu binti.

Watumishi wa Mungu walioitwa na wanaoongozwa na roho wanaweza kusolve. Sio watumishi watakao kurupuka tu ngoja tumuombee apone inaweza isifanye kazi.
 
Maskini weeee!,nimesikia vibaya, sisi wazazi wengine hua hawachukui mda wakukaa na watoto kuwasikiliza au kuwauliza
chochote ili ujue mtoto wako ana weakness gani au anasumbuliwa na nini zaidi yakusema huyu mtoto ni msununu kama
bibi yake,msiri kama shangazi yake,hajiamini kama mamake mdogo,baada ya kutafuta tatizo liko wapi. mwenyezi mungu
Atunusuru ...
 
Mkuu unahaki ya kuumia mtu mda wote kimya kama kafiwa.
Jaribu kuwa karibu zaidi na ikibidi kuwa mwema kupitiliza mtoe aut mkiwa na marafiki hasa hasa wale anaowakubari yeye.
 
Mambo ya mabinti kuwa abused na baba zao yapo kwa wingi sana.

Mimi nina mdogo wangu wa kike (mtoto wa baba mdogo). Sasa baba mdogo akaja kufariki, wakati huo, huyo binti ana miaka kama 10 hivi.

Sasa baada ya hapo mwenendo wake wa shule haukuwa mzuri sana. Binti akawa hataki kusoma, yeye ni mapenzi na mabwana kwa kwenda mbele.

Mzee wangu akaingilia kata kutaka kujua kwa nini hali hipo hivyo.

Baadae huyo binti akaja ku confess kuwa alikuwa anafanya mapenzi na baba mdogo tokea akiwa na miaka 6.
 
Msaidie kutembelea nyumba za ibada haswa semina za neno la Mungu ipo siku atapona katika hilo sononeko lake
 
Ana jinni mkausho. Ni jini hatari sana kwa kuwafanya watu wanune hovyo.
 
Hili ni tatizo au ni nature ya mtu..?

Wanajamvi naombeni maoni /ushauri wenu kwa hili.

Dada ninayemfata kuzaliwa ni ana sijui niseme tabia tofauti .na kwa mujibu wa wazazi hali hii ilimtokea siku moja baada ya kuchapwa na baba kipindi hicho akiwa bado ni mtoto wa miaka 5.
Alilalamika sana kwamba kaonewa lakini hakusikilizwa....kachezea fimbo na lakini si baba wala yeye hakuna aliyesema ni kwa nini kachapwa!
Kwamba hata mama alipo taka kujua sababu hakupata jibu ,basi toka hapo
akaanza kubadilika kwa kasi ,ule ucheshi,ucheza na furaha na kucheka mda wote ikawa kinyume!
Si nyumbani yaani popote alipokwenda ile ikawa ndio muonekao wake mpya ,baadae sana mpaka walimu na wazazi na ndugu waliingilia kati kuhusu hili lakini haikusaidia maana mpaka hivi ukubwani yuko vile vile na ukimuuliza sana sababu yeye kubwa ni kulia na labda akwambie hajui kwa nini au akutizame tu!
Yeye huwa haongei mpaka alazimike sana,anakaa masaa mengi peke yake kajiinamia ,hapendi ukaribu au kelele wala mjumuiko wowote,halafu ana aina fulani ya kutizama kitu au mtu ambayo ni ngumu kuitafsiri,sasa ana miaka 31 anafanya kazi na anaishi peke yake hana mpango wa ndoa wala bf!
Tumejaribu sana kumsaidia mpaka watu wa tiba lakini hakuna mabadiliko,inaniumiza sana kwa vile nahisi kuna kitu kinamsumbua bila yeye kujua au ni nini..??
Isije ikawa alibakwa na kuchapwa, watu waliobakwa au kuumizwa sana kihisia hata wakiwa watoto huwa hawaji kuwa normal kama kwa tabia hizo za dada ako inawezekana alijihisi kubaguliwa toka mtoto
 
Huyo baba yake hakumuabuse kweli??? Sorry labda alimbaka au kum-abuse sexually kwa namna yoyote na fimbo akampiga....

Au mtu /watoto walimuabuse na baba hakumsikiliza na kumchapa

Kuna tatizo mahali
 
ni vigumu sana kuamini kama mtoto tabia yake ilichange ndani ya siku moja tena zaidi ya miaka 25 iliyopita bila kuusisha kunyanyaswa kingono/kisaikolojia but ni vigumu zaidi kuhamini maana baba yake mzazi ndiye aliyehusika kumchapa

sitaki kuhamini icho nilichokiandika juu ila ninachoamini dada yako ni MBINAFSI na hayo ndio maisha aliyochagua yanayompa raha
she is matured enough to decide what is good and what is bad for her..ni kwamba mmechelewa sana
 
Huyo usijekukuta mzee alimu abuse na stick akapigwa, na ni kosa kubwa sana kutokumsikiliza mtoto anachotaka kusema, kwa kawaida mtoto akikosea ukimchapa atakiri , ukiona bado anabisha hajafanya ujue asilimia kubwa hajafanya kweli, hilo jibu analo mzee wako na muhusika mwenyewe

Hilo limo miongoni mwa zile hisia za wengi lakin
Hatuna uhakika maana hakuna kati yao aliye wahi
Kusema .mzee ameshafariki si dada angeongea basi.
 
Pepo mchafu wa kibri kinyongo kununa kisirani toka kwa huyu Dada kwa jina LA Yesu. Ila mbona asilimia kubwa mboko tumepigwa na hatujawa hivo
 
Asa
Hii imekaa kiroho zaidi. Initiative mnayotakiwa kuchukua ni kubwa ili kurescue huyu binti.

Watumishi wa Mungu walioitwa na wanaoongozwa na roho wanaweza kusolve. Sio watumishi watakao kurupuka tu ngoja tumuombee apone inaweza isifanye kazi.

Asante kwa ushauri mkuu,tumekwenda huko ila bado au sijui tunakutana na wajanja..?
 
Back
Top Bottom