Ameambiwa ana tatizo la Hormone Imbalance

Ameambiwa ana tatizo la Hormone Imbalance

robbinhood

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2020
Posts
541
Reaction score
1,539
Habari ndugu zangu..!
naombeni ufafanuzi juu ya hili jambo lililomkuta Mwenzangu
Kipi ni mshauri?

screenshot hapo chini imelezea tatizo lake hadi kupelekea kuelezwa hivo na daktari
Screenshot_20201111-164910.jpg
 
Sasa alivyo fikiri ku>google ndipo atakapo pata matibabu? Si awaone watibabu ili wapate kumtibia hiyo hormone imbalance ndipo atakapo weza kupona na kuweza kushika mimba pasipo na kutibiwa hawezi kushika mimba na la wala kuzaa.

HORMONE IMBALANCE
Hormone imbalance ;
Hili n tatizo linalo wakumba akina mama (wanawake) wengi ambalo husababishwa na kiwango kidogo cha Hormone ya ESTROGEN.

DALILI ZA HORMON IMBALANCE
_kupungua hamu ya tendo la ndoa
_kutoshika mimba
_.mzunguko wa hedhi kubadilika badilka
_kuto pata usingizi vizuri
_kuongezeka uzito
_kupata choo kwa shida
_mapigo ya moyo kuto kuwa sawa
_maumivu wakati wa tendo la ndoa
_maumivu ya kichwa
_mafua ya Mara kwa Mara
_kupoteza kumbu kumbu
_uchovu wa Mara kwa Mara
_ngoz kavu
_maumivu ya mifupa na viungo
_kujiskia joto ghafla hasa wakati wa usiku
_kuwa na mawazo na wasi wasi
Ukiona una dalili hizi basi jua una tatizo la hormone imbalance
 
Sasa alivyo fikiri ku>google ndipo atakapo pata matibabu? Si awaone watibabu ili wapate kumtibia hiyo hormone imbalance ndipo atakapo weza kupona na kuweza kushika mimba pasipo na kutibiwa hawezi kushika mimba na la wala kuzaa.

HORMONE IMBALANCE
Hormone imbalance ;
Hili n tatizo linalo wakumba akina mama (wanawake) wengi ambalo husababishwa na kiwango kidogo cha Hormone ya ESTROGEN.
DALILI ZA HORMON IMBALANCE
_kupungua hamu ya tendo la ndoa...
Ubarikiwe sana mkuu
 
Inabidi aende hospitali kupimwa ili ijulikane ni hormone gani hazijabalance! Estrogen or progesterone or otherwise. Ili apate tiba stahiki.. inaweza kuwa very simple
Hospital nying hazipimi oestrogen au progesterone level lakn huwa inakua costful sana na the common symptom huwa ni AUB especially kwa wanawake ambao wako kwenye reproductive age na matibabu yake huwa ni simple tu COC ambazo zina both estr na proge
 
Nina tatizo la hormone imbalance..
Naombeni mawasiliano ya mtaalamu wa tatizo Hilo..mwenye kutibu na tatizo lisijirudie tena Jamani..
Inategemea na sehemu ulipo na hormonal imbalance ni pana inategemeana ni imbalance ya hormones zipi,hivo ni muhimu kwenda hospital wabaini tatizo na kukupatia matibabu..
 
Nina tatizo la hormone imbalance..
Naombeni mawasiliano ya mtaalamu wa tatizo Hilo..mwenye kutibu na tatizo lisijirudie tena Jamani..

Tafuta gyno yoyote mzuri atakusaidia... hili limekua tatizo very common of late kwa sisi mabinti... i know kuna treatments nyingi na depending na situation ya mtu some of them zina kikomo na kwa wengine ni mwendo wa kurudiarudia tiba.

NB: usiende kwa GP utaambiwa its normal tafuta gyno mzuri mwenye experience zake and sometimes u can see hata gyno wawili kujiridhisha tu (juzi nmempeleka dogo mmoja hosp bahati mbaya tukamkosa gyno akamuona GP wa kawaida khee kamwambia mtoto wa watu its normal kukosa mzunguko for more than 8mnths aanze kuitake seriously akifika 23 yrs nlichoka)

All the best.... and usisahau kumshirikisha Mungu as well, haya mambo sio sometimes
 
Nina tatizo la hormone imbalance..
Naombeni mawasiliano ya mtaalamu wa tatizo Hilo..mwenye kutibu na tatizo lisijirudie tena Jamani..
Unaweza kutibiwa kwa dawa za asili na matatizo yako ya hormone imbalance yakaisha lakini hapa katika hili Jukwaa tumekatazwa tusiweke contact zetu. Haturuhusiwi na wahusika wa JF Doctor. Kama unao ujanja ututafute kwa ujanja wako ili uweze kutupata tupate kukutibia upate kupona maradhi yako.
 
Inategemea na sehemu ulipo na hormonal imbalance ni pana inategemeana ni imbalance ya hormones zipi,hivo ni muhimu kwenda hospital wabaini tatizo na kukupatia matibabu..
Umeeleza vema mkuu. Vipi kuhusu kwa wale wanaokwenda kwa Tabibu JJ Mwaka badala ya kwenda hospital kwanza?

Tiba mbadala zinaweza kumaliza tatizo pasipo kwenda hospital?
 
Unaweza kutibiwa kwa dawa za asili na matatizo yako ya hormone imbalance yakaisha lakini hapa katika hili Jukwaa tumekatazwa tusiweke contact zetu. Haturuhusiwi na wahusika wa JF Doctor. Kama unao ujanja ututafute kwa ujanja wako ili uweze kutupata tupate kukutibia upate kupona maradhi yako.
Ahsante
 
Tafuta gyno yoyote mzuri atakusaidia... hili limekua tatizo very common of late kwa sisi mabinti... i know kuna treatments nyingi na depending na situation ya mtu some of them zina kikomo na kwa wengine ni mwendo wa kurudiarudia tiba...
Ahsante sana, nitafanya ivyo.
 
Umeeleza vema mkuu. Vipi kuhusu kwa wale wanaokwenda kwa Tabibu JJ Mwaka badala ya kwenda hospital kwanza?

Tiba mbadala zinaweza kumaliza tatizo pasipo kwenda hospital?
Sina experience sana na huyo mtu hapo juu lakini akifanya vipimo ikajulikana imbalance ni ya hormones zipi Tiba mbadala pia wanaweza kumsaidia, Lakini my Take ni muhimu kujua imbalance ni ya kitu gani you can find ni estrogen, progesterone, Testosterone, T3, T4 na matibabu ni tofaut tofaut anahitajika a sensitive doctor to dertemine the underlying imbalances to come up with an appropriate Rx
 
Tafuta gyno yoyote mzuri atakusaidia... hili limekua tatizo very common of late kwa sisi mabinti... i know kuna treatments nyingi na depending na situation ya mtu some of them zina kikomo na kwa wengine ni mwendo wa kurudiarudia tiba...
Ana umri gani huyo binti maana kama hajapata menses for 8 months hiyo tayar ni amenorrhea na inaweza kuwa primary,secondary au physiological na kipimo cha kwanza kwa binti au mwanamke yeyote of reproductive age suffering from loss of menses ni UPT kabla hatujaanza kuangalia other causes

NB:Every woman of reproductive age is pregnant untill proven otherwise
 
Hospital nying hazipimi oestrogen au progesterone level lakn huwa inakua costful sana na the common symptom huwa ni AUB especially kwa wanawake ambao wako kwenye reproductive age na matibabu yake huwa ni simple tu COC ambazo zina both estr na proge
Wanapima hormonal profile hasahasa hospitali kubwa kidogo. Ndipo it can be choosed km apewe progesterone only therapy au COC.
Hormonal imbalance yaweza kuwa excessive progesterone na ukimpa COC inazidisha progest
 
Back
Top Bottom