Ameachwa kisa hawashabiiani

Swenailie

JF-Expert Member
Feb 15, 2016
240
229
Ndugu habarini

Naomba mniambie hivi mtu akiamua kukuacha kisa hamshabiiani utafanya nini? Utalia Au utamshukuru Mungu na kumuomba akusaidie uondokane na udhaifu wako akupe mtu sahihi mtakaeshabiiana.???

Kuna dada alimpenda sana mkaka flan sasa huyo kaka amemuacha amemuambia hawashabiiani. Mdada analia tu hadi ameathirika kisaikolojia anajihisi anamapungufu ambayo mwanaume hawezi kuyavumilia.

Hali kubwa Ni unywaji wa pombe na starehe huyo kaka anapenda kujirusha na kunywa pombe Mdada hayuko hivo Ni bon town na maisha yake Ni yakitown. Wengi waliotambua uhusiano wao walikuwa wanahofu ila yule dada anadai alimpenda mkaka hivo hivo alichokuwa anakifanya Ni kumsihi asinywe pombe kupitiliza na starehe ziwe na mipaka. Tatizo limekuja pale yule dada anapoona huyu kaka anayoyafanya akikasirika akagomba yule kaka anaona Mdada anataka kumcontrol yule dada hadi anajiskia vibaya. Ilitokea siku huyo kaka alikwenda kunywa pombe siku ambayo kesho yake alikuwa anaingia kazini na mazngira ya kazi yake hawaruhusiwi pombe yule dada alikasirika akamind akihitaji asinywe siku za kaz kulinda kibarua chake kwa manufaa yake na watoto wao kilichotokea yule kaka akaona anafatiliwa akabadilika kabisa.

Kwa kupishana huko mkaka kaona waachane hawaendani Mdada analia Kila siku anataman waendelee yeye atafanya atakabyotena.

Huyu dada Ni upendo? Au utumwa? Mm sielewi ningekuwa mm ningelia nikanyamaza nkasonga mbele..

Kama hatushabiiani lazma amemuona wanaeshabiiana. So hata akiendelea kulia anaemlilia hamkumbuki hata.

Naona siku hizi kuishi na mtu lazma mshabiiane. Wanaume wengine ndo wanataka hamsini hamsini kumbe ukinywa lazma na mwanamke anywe Utakalofanya lazma na yeye afanye. La siivo sio type yako.
 
hamwezi kufika popote kama hamuendani tabia.
huyo dada analazimisha mfupa kwenye chungu , kitapasuka!!!

mwambie akue kiakili
mwanammke halisi hawezi kupenda mwanaume wa dizaini hio hata siku moja... aache kupenda masharobaro
 
Ndugu habarini

Naomba mniambie hivi mtu akiamua kukuacha kisa hamshabiiani utafanya nini? Utalia Au utamshukuru Mungu na kumuomba akusaidie uondokane na udhaifu wako akupe mtu sahihi mtakaeshabiiana.???

Kuna dada alimpenda sana mkaka flan sasa huyo kaka amemuacha amemuambia hawashabiiani. Mdada analia tu hadi ameathirika kisaikolojia anajihisi anamapungufu ambayo mwanaume hawezi kuyavumilia.

Hali kubwa Ni unywaji wa pombe na starehe huyo kaka anapenda kujirusha na kunywa pombe Mdada hayuko hivo Ni bon town na maisha yake Ni yakitown. Wengi waliotambua uhusiano wao walikuwa wanahofu ila yule dada anadai alimpenda mkaka hivo hivo alichokuwa anakifanya Ni kumsihi asinywe pombe kupitiliza na starehe ziwe na mipaka. Tatizo limekuja pale yule dada anapoona huyu kaka anayoyafanya akikasirika akagomba yule kaka anaona Mdada anataka kumcontrol yule dada hadi anajiskia vibaya. Ilitokea siku huyo kaka alikwenda kunywa pombe siku ambayo kesho yake alikuwa anaingia kazini na mazngira ya kazi yake hawaruhusiwi pombe yule dada alikasirika akamind akihitaji asinywe siku za kaz kulinda kibarua chake kwa manufaa yake na watoto wao kilichotokea yule kaka akaona anafatiliwa akabadilika kabisa.

Kwa kupishana huko mkaka kaona waachane hawaendani Mdada analia Kila siku anataman waendelee yeye atafanya atakabyotena.

Huyu dada Ni upendo? Au utumwa? Mm sielewi ningekuwa mm ningelia nikanyamaza nkasonga mbele..

Kama hatushabiiani lazma amemuona wanaeshabiiana. So hata akiendelea kulia anaemlilia hamkumbuki hata.

Naona siku hizi kuishi na mtu lazma mshabiiane. Wanaume wengine ndo wanataka hamsini hamsini kumbe ukinywa lazma na mwanamke anywe Utakalofanya lazma na yeye afanye. La siivo sio type yako.
Pole sana kwa yaliyokukuta, believe me within six months utakuwa unacheka na kujiona mjinga kwa machozi unayoyatoa sasa hivi.
 
Huyo mdada ana miaka mingapi?Mpaka hapo alipofika huyu jamaa hamuhitaji japo watu wanasema anaepanda kikweli hachoki kuvumilia lakini kwa hili naona imetosha ajipange,wapo wasiokua na tafran wala kumchubua roho kwani huyu jamaa ananini cha zaida ebu muulize akwambia kama rafiki yako kipenzi basi atakwambia anachokikosa kwa huyo huenda kuna wengine wanafani zaidi ya za huyo anaemsugua ROHO yake...
 
Kinachomliza nini? Mbona dyudyu zipo nyingi tu tena decent kabisa. Akijituliza ataonwa tu na mtu wa kaliba yake.
 
tatizo vigezo vya wadada ndio huyo kaka anavyo..

sio yeye tu kizazi cha watoto wa mafisadi kinasumbua sana wadada wengi mjini na wana bahati ya kupendwa kweli na hao wadada..

ila wengi wao ni pombe na starehe maana ndio maisha waliyokulia..

mdada mpaka anakupenda sana ni uhakika wa kufanya maisha na wewe..

sasa hao vijana pamoja na ma starehe yao wadada wanawapenda sababu uhakika wa maisha upo..

hata akiolewa ni bonge la harusi ( hii ndoto ya wadada wengi)

pili kuanza maisha hupangi vyumba vya shida shida.. appartment za urithi zipo tayari...

na ana uhakika wa kusaidiwa kimaisha kwa network za hao watoto wa mafisadi..

hayo yote yanafanya mdada ashindwe kumwacha huyo mkaka shida wanachokosea ni kutaka kuwabadilisha hao wakaka ili waishi kama good boys ambayo sio maisha waliyokulia
 
huyo pombe anayokunywa ovyo s bure kuna Kitu ananywea-------- muwache dad wa watu huenda atamwokoa kutoka kwenye utumwa wa ombe maana kampenda na madhaifu yake.
 
Kumbe hadi wamezaa wote watoto alaf mshikaji anamwacha kisa hawaendani? Hapa kuna tatizo!! Wakubaliane tu waishi pamoja kwa manufaa ya watoto wao. Isitoshe ushauri wa dada ni mzuri sana.
 
tatizo vigezo vya wadada ndio huyo kaka anavyo..

sio yeye tu kizazi cha watoto wa mafisadi kinasumbua sana wadada wengi mjini na wana bahati ya kupendwa kweli na hao wadada..

ila wengi wao ni pombe na starehe maana ndio maisha waliyokulia..

mdada mpaka anakupenda sana ni uhakika wa kufanya maisha na wewe..

sasa hao vijana pamoja na ma starehe yao wadada wanawapenda sababu uhakika wa maisha upo..

hata akiolewa ni bonge la harusi ( hii ndoto ya wadada wengi)

pili kuanza maisha hupangi vyumba vya shida shida.. appartment za urithi zipo tayari...

na ana uhakika wa kusaidiwa kimaisha kwa network za hao watoto wa mafisadi..

hayo yote yanafanya mdada ashindwe kumwacha huyo mkaka shida wanachokosea ni kutaka kuwabadilisha hao wakaka ili waishi kama good boys ambayo sio maisha waliyokulia
Kwa Hilo hapana hatujui anampendea nn maana hata ukiuliza anajibu anampenda tu and hata kama Ni hela si kwamba huyo kaka anahela sana Au nn na huyo dada si mtu wa kusema anagharama sana Au anamatamaa ya hela. Sema sijui nn mdada kapenda haelewi mwenyewe kapendea nn
 
Kuna dogo mmoja aliolewa na jamaa mmoja, jamaa mwenyewe kila siku alikuwa na issue na polisi, mara wamekuja kuserch ndani, mara yuko ndani, mara binti anatafuta pesa ya kumwekea dhamana. Tulimsihi sana atoke kwenye ndoa ile, binti mwenyewe wa kishua. Alitujibu ni yeye na roho yake ndio anajua kwanini anampenda jamaa. Lilitushuka na kunawa mikono.
 
Kupata mtu mnaefanana naye kwa kila kitu nayo ni changamoto mno..Ndiyo maana kwenye ndoa tunaamini Mme akiwa kimeo,...Mke ana kuwa mzuri sana kama hapo nahisi Mwanaume amekurupuka tu maana mwanamke alikuwa anamshauri vizuri sana na kwa faida yao wote lakini yaelekea mwanaume alikuwa hampendi huyo mwanamke akatafuta sababu tena isiyo na mashiko kabisa kumpiga chini...
 
mwanaume ndie anaetakiwa kupenda! mwanamke anafundishwa kupenda! hivyo ukiachwa jua HAJAKUPENDA...... PERIOD!
ah ah ah umenifurahisha, wanaume wanatakiwa kutupenda, na wanawake tunatakiwa kuwatii waume zetu. u hav spoken well
 
Back
Top Bottom