Amchoma visu 8 mpenzi wake

Challya

JF-Expert Member
Jun 10, 2019
462
579
Hii imetokea kwa jirani zetu hapo Kenya tarehe 09/05/2020 jioni.

Mwanamke ambae anaitwa Vigilance Shighi(29) ambae ni kabila la Mtaita amemchoma kisu mara saba kifuani na kupelekea kufariki mpenzi wake ajulikanae kwa jina la Edward Okello(33) ambae ni mjaluo.

Edward Okello alikuwa ni engineer wa ndege katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta(JKIA).

Sababu kuu iliyopelekea Vigilance kumchoma visu mpenzi wake ni wivu wa kimapenzi alikuwa akimuhisi mpenzi wake kutoka na mwanamke mwingine, baada ya kumwambia marehemu hilo suala ndipo ulipoibuka ugomvi mkubwa, katika kubishana akachukua kisu kwa hasira akamchoka mpenzi wake.
Tayari Vigilance ameshakamatwa na police.

NB: Kama upo na mtu hata kama una mpenda vipi unapomfumania au unahisi sio muaminifu usimdhuru ni bora tu uachane nae, watu wapo wengi sana kwenye hii dunia sio yeye pekee yake.

Jifunze kupenda kwa kiasi, kwani kiwango chako cha kupenda ndio kiwango chako cha maumivu baadae.

Kama wewe ni mwanaume jifunze sana kutumia pesa zako kwa kiasi kwa mwanamke ili akikusaliti usiumie sana na mwanamke jifunze kupenda kwa kiasi itakusaidia baadae.

FB_IMG_15892775074322475_1.jpeg
FB_IMG_15892774965472042.jpeg
 
Hatimae uzuri wake wote unaenda kuishia jela,sijui atawazaje saa akijitazama huku uso haueleweki wake au wale makomando wa vita vya mauamau.
 
"Mahusiano sio kwa ajili ya kila mtu"
Neno KILA MTU hapo ndo linakua ngumu kutafsirika,kwanini
Mahusiano yapo kwa kila mtu na ni kwajili ya kila mtu,ila walo ndani ya mahusiano hawawezi kuwa ndani mahusiano ya kila mtu,ndo maana kala visu,inauma,ila kamshikisha adamu sana.
 
MAPENZI HAYANA BREKI NA HAYANA KIPIMO!

HAKUNA KUPENDA KIASI WALA KUWA NA MACHALE!
UKIPENDA UMEPENDA
TUMUOMBE MUNGU ATUJAALIE WENZA BORA WATAKAOTUFANYA TUONE DUNIA KAMA PARADISO.,,.ATUONDOSHEE MASHETANI WANAOKUJA KWA MAUMBO YA WATU KUJA KUTUANGAMIZA;
 
Si angemuacha tu huyo mwanaume yeye aendelee na maisha yake, mbona simpo tu.
Hasira hasara
 
Aisee mim nikiona kuna dalili ya ugomvi chumbani huwa nafidha vitu vyenye ncha kali,haya Mambo ya kutumia hisia ni hatari

California love
 
Back
Top Bottom