Ambassador from Tanzania: Who is Mwanaidi Maajar?

kwani LOWASA sio kichwa
- hiyo ya utalii tuliibiwa tu hakuna kitu kilichofanyika sikuona impact ya yale matangazo kwa waingereza nilichokuwa nasikia ni malaria za CHERRY COLEY tu hizo hela za utalii ni kijiko cha sukari bahari.
watalii wanakuja bongo ni kwamba wafanyeje tu na wanaletwa na vitu ambavyo awawezi kuvipata mahali kwingine kutoka na wizi na miundo mbinu hapo alichofanya huyo mama na kundi laki ni kununua nepi nyingi za mtoto wakati wamimba mtoto akatoka amekufa

- Mkuu chonde chonde, huyu mama ameacha shirika lake la Sheria, la 50 Million Shillings per year kulijenga taifa na mshahara wetu mbuzi, please mkuu yale matangazo yametuinua sana taifa, I mean sio kila ishu iwe ligi tu kwenye hili taifa tunao wachapa kazi na huyu mama ni mmojawapo ,mimi sijaona wala kusikia makosa yake kwa taifa na ninaomba kunawa mikono na hii mada, maana sasa hivi mtaanza kumtukana mama wa watu bila sababu za msingi, I mean sometimes tuwe na shukrani wanapotokea viongozi wanaofaa, baadala ya kuwashambulia tuu! khaaaaa! Huyu mama amekosa nini hasa?

- Alipokwenda UK ameshambuliwa wee! lakini kwenye ukweli uongo hujitenga kule UK ameacha historia ya kuchapa kazi, huyu ni mchapa kazi sana na anafaa sana kwa taifa, sio goi goi!


Willie @ NYC, USA.

mkuu connect hii dot Rex Attorneys, na huyo mama .ina maana mkuu hujui huyo firm imefanya nini TANESCO
hafaru ni huyo mama aliyea andika barua kutoka huko USA ubalozi akitaka serikali ilipe hela za mambo binafsi ya mfanyakazi wa ubalozi wetu kwa kumnyanyasa mfanyakazi wake wa ndani

ubalozi wa uk alikotoka CAG kaweka bayana kuna zaidi ya milioni 500 zimetumika bila kufuata utaratibu

-- bado ujajibu swali langu kwani LOWASA sio kichwa?
watu wengi wanaoliibia ili taifa ni wale wanaojifanya watu wa watu kupata huruma, rejea sifa za matapeli
lugha nzuri ndio kinGa ya ufisadi MKUU si unaona MO biashara zake zinakwenda tu vizuri kwa kujifanya mtu wa watu

kama yeye alikuwa nalipwa Milioni 50 kwa mwaka kaziacha kwa nini? au ndio kupata access ya Diplomatic BAGS
kwa nini hakuakikisha TANESCO wanapata ushauri bora kama kweli yeye ni mzalendo.
hata huko BOT kuna mambo ya ovyo mangapi na washauri wenyewe ndio hawa
elimu yake kaitumia kama kisu kutumaliza wanyonge simple and clear

-- Na hii tabia ya kuwaita watu vichwa hali wanamaliza mali za umma ni kukosa uzalendo,
tafuta report za mahesabu ya balozi ndio utajua huyo mama ni nani ? hakuna majungu hapa ni kwamba hafai na uteuzi wa jk unajulika lazima uwe mchafu kwanza ili akupe kazi.
taja mtu msafi anayefanya kazi na jk kama sio mnafiki sitta na mwakyembe tu waliobaki ni kundi la waporaji
 
Mkuu naona umenunuliwa kuwatetea mafisadi wa chama chako kwa nguvu zote. In red, if you have not seen and heard, why not shut your big mouth and learn what you are told. You see my brother I hate people who tend to defend every wickedness of this government. How often have you denied the truth about dubious moves done by your fathers (government). You (CCM) tend to deny every thing, and actually you always change the colors (Black to white). Kama hujui kuwa huyu mama ni fisadi jifunze na ameingia hapo kimagumashi, learn from today. Hujui hawa Rex Attorneys wameingamiza hii nchi kiasi gani.

- Duh! hivi toka lini JF tukakatazana kutoa maoni yetu just because wewe huyapendi, my record iko very clear of what I stand for ama sivyo usingekwua na hito hate unayoisema, sijawahi kutetea maviongozi magoi goi kwangu ni mwiko wala kuogopa kusema maoni yangu in any ishus, ni jana tu nimesema hivi vyama vyote vifutwe wka sababu havina agenda ya kukusanya kodi ambao ni tatizo sugu la taifa, CCM hawakusanyi kodi na Chadema hawataki kumlipia kiongozi wao maarufu kodi, wote hawtufai taifa,

- HOWEVER: hapa sijaona kosa la huyu mama, liesemni basi tuchambue pumba na mchelle! badala ya maneno ya vitisho na ukiranja wa JF, sema kosa lake nini hasa amelifanya UK au hapo alipo sasa?


Willie @ NYC, USA.
 
-- bado ujajibu swali langu kwani LOWASA sio kichwa?
watu wengi wanaoliibia ili taifa ni wale wanaojifanya watu wa watu kupata huruma, rejea sifa za matapeli
lugha nzuri ndio kinGa ya ufisadi MKUU si unaona MO biashara zake zinakwenda tu vizuri kwa kujifanya mtu wa watu

kama yeye alikuwa nalipwa Milioni 50 kwa mwaka kaziacha kwa nini? au ndio kupata access ya Diplomatic BAGS
kwa nini hakuakikisha TANESCO wanapata ushauri bora kama kweli yeye ni mzalendo.
hata huko BOT kuna mambo ya ovyo mangapi na washauri wenyewe ndio hawa
elimu yake kaitumia kama kisu kutumaliza wanyonge simple and clear

-- Na hii tabia ya kuwaita watu vichwa hali wanamaliza mali za umma ni kukosa uzalendo,
tafuta report za mahesabu ya balozi ndio utajua huyo mama ni nani ? hakuna majungu hapa ni kwamba hafai na uteuzi wa jk unajulika lazima uwe mchafu kwanza ili akupe kazi.
taja mtu msafi anayefanya kazi na jk kama sio mnafiki sitta na mwakyembe tu waliobaki ni kundi la waporaji

- Mnamuonea tu kwanza huyu mama aliomba kuacha ubalozi baada ya UK, alitaka kurudi nyumbani ni taifa ndio tumemuomba aendelee, mkuu samahani sana mimi huwa siendi na upepo wa bendera au kufikirishwa kwa mafungu, ninasema hivi hebu onyesheni makosa yake akiwa ubalozini UK amelikosea nini taifa? na hapo alipo sasa amelikosea nini taifa? hapa hatuna muda wa majungu majungu ni mwiko hapa!

Willie @ NYC, USA.
 
Hivi Foreign Affairs hakuna wanataaluma ambao ni wanadiplomasia halisi? Inashangaza UN yupo mwandishi wa habari; Washington kuna wakili; hivi mh. Membe hana wanadiplomasia wa kutosha mpaka balozi zetu wapelekwe watu wa fani tofauti? Huyu mama kama sikosei alikuwa die hard member wa cuf, pili hakuwa mwajiriwa wa serikali pamoja na kuwa mh.Raisi ana mamlaka ya kumteua mtu yeyote kidogo kuna mushkeli kwenye uteuzi wake kama ni suala la kuwa yeye ni lawyer nadhani pale sheria kuna malawyer waliobobea; hapo pana sirikali just, uteuzi wake hauhusiani na udini wala mapenzi just connect the dots

Chama
Gongo la Mboto DSM

- Kazi ya ubalozi ni Presidential appointees, sasa ni uamuzi wa Rais ambao sisi wananchi wa Jamhuri tumempa dhamana kwa kumchagua kisheria kua Rais, ingawa ni muhimu sana in the future hawa Presidential appointees wakawa confirmed na bunge, lakini kwa sasa Rais ana haki ya kumcchgua yoyote yule ndio maana ya Demokrasia inayoitwa the winner takes all kama yetu!

Willie @ NYC, USA.
 
Taifa lilimuomba?????au aliemteua????sijasikia kua taifa limemuomba
- Mnamuonea tu kwanza huyu mama aliomba kuacha ubalozi baada ya UK, alitaka kurudi nyumbani ni taifa ndio tumemuomba aendelee, mkuu samahani sana mimi huwa siendi na upepo wa bendera au kufikirishwa kwa mafungu, ninasema hivi hebu onyesheni makosa yake akiwa ubalozini UK amelikosea nini taifa? na hapo alipo sasa amelikosea nini taifa? hapa hatuna muda wa majungu majungu ni mwiko hapa!Willie @ NYC, USA.
 
Nashangaa sana ubalozi wetu wa USA unashida gani?Maana nimekutana na wageni kutoka USA wanaVisa zao ambazo wanaambiwa siyo za kweli au wnatakiwa wapewe visa nyingine hapa Tanzania na wakati mtu kaishalipa USD100 zake huko USA..Naomba huyo mama haweke mambo sawa huko.Ukiwauliza watu hao wa uhamiaji wanasema Ubalozi wtu huko USA hauna Afisa uhamiaji..wanakwenda kiushikaji tu lakini sio maafisa uhamiaji
 
- Rais anapokuomba anwakilisha taifa kwa hiyo unaombwa na taifa!, jamani hata haya mambo madogo maodogo nayo taabu! ahhhh!Willie @ NYC, USA.
..nimefuatilia michango yako kwenye hii mada nimegundua kwamba kumbe nilikuwa namtizamo usio sahihi juu yako... Yani mshkj wewe ni mweupe pee.. nanga kbs upstairs! ..hamna kitu aisee! ..duh kaaazi kweli kweli!
 
Kaka Willie,
Pole na kazi heshima mbele.

Unahaki ya kutoa mawazo yako na misimamo yako, hilo halina shida.
Tunajua Ubalozi ni kazi ya kutajwa jina na mkuu wa nchi, hilo halina ubishi, uwe na sifa au la ukitajwa jina unakwenda. Sina wasiwasi na creditial za mama Maajar, balozi wetu nchini USA. Ila nina wasiwasi na ethics kama kiongozi anayetuwakilisha. Vile vile ninawasi wasi na uzalendo wake. Historia ya biashara zake sio nzuri.

Rex attoney imeliingiza Taifa hasara kubwa. Kwa ushauri mbaya uliokuwa na mazingira ya rushwa na uhujumu uchumi. Katika mazingira hayo Rex attoney imetoa ushauri wa kimazabe kwa tanesco kwa manufaa ya the other sides. Moral and ethical obligations hazikufuatwa, huku wakiwa ni waomi wenye uelewa mzuri waliamua kuiibia nchi kwa makusui. Kesi ya Tanesco, Dowans/Ricmond. Rex alikuwa kote kote.

Upatikanaji wa hii tender ya kesi kupitia Tanesco na Kuishauri Tanesco, bila shaka uliasisia na Balozi Maajar kwa kuwa na ukaribu wa Mkuu wa kaya. Wakala kubwa wakatuacha mpaka leo umeme ni historia.

Unaweza kusema hapa alikuwa anafanyabiashara hana kosa, kosa ni la kwetu sisi tulioshindwa ku-vett. Kumbuka hawa wanatumia heavy weight vimemo, na mgawo mkubwa kutumaliza. Uzalendo uko wapi???? Mzunguko wa fedha chafu ndio unawaweka madarakani, tuwatetee kwa lipi? Kweli unategemea atatuletea mwekezaji makini, wakati yupo kimaslahi yake zaidi.

Ni lipi jema kalifanyia taifa tangu kuteuliwa kwake ubalozi?
 
..nimefuatilia michango yako kwenye hii mada nimegundua kwamba kumbe nilikuwa namtizamo usio sahihi juu yako... Yani mshkj wewe ni mweupe pee.. nanga kbs upstairs! ..hamna kitu aisee! ..duh kaaazi kweli kweli!

Chipanga,
Bill is one of the owners of JF...IF YOU DONT KNOW
 
Wiiliam!

Tetea tu ,maana uko kwenye system,maana dada zako nao ni wateuzi wa Kiranja mkuu!
Fact huyu mama ni fisadi,angalia firm yake na mikataba ya Tanesco!

Wakati wa Nyerere,huwezi kuibuliwa kuwa balozi,mpaka upitie mkondo wa Foreign Affairs!
Kuhusu UK,alikuwa balozi wa CCM nchini UK!

Kwa hiyo kusema haya ni majungu,ni kujipendekeza,i guess may be umetumwa na huyu mama kumsafisha.
Haya yote mabilioni atayaacha tu siku moja


- However: sina uhakika alifikaje kwenye ubalozi, lakini in her case the end justifies the means!, Wa-Tanzania tuache majungu majungu huyu mama ni kichwa sana na taifa tunahitaji viongozi kama huyu! Creative na Active!


William @ NYC, USA. [/QUOTE]
 
Very creative, humble and hard working. Above all, educated, commited to National interest than cheap political popularity...mama fanya kazi achana na watu wenye mawazo ya kisemenari
 
Well said, nakugongea thanks mkuu!!

Tusiwe wavivu wa kufanya uchambuzi!! Hivi, all all the people waliopo Foreign Affairs, waliosomea International Relations & Diplomacy...wenye Ph.D na uzoefu wa miaka mingi JK alimuona Mama Majaar peke yake??.....kuna kingine zaidi ya hiyo CV (angempa kazi Ministry of Justice basi)...huyu alipelekwa nje...kurahisisha baadhi ya mambo! Fumbueni macho na masikio...nuseni!!!
 
- Wa-Tanzania wakati mwingine tuache majungu majungu, huyu mama ni kichwa na anafaaa sana binafsi ninamkubali, akiwa UK amelitangaza sana taifa letu kwenye utalii, amewaunganisha sana wananchi wetu kule, sijawahi kusikia Chadema wamefungua tawi kule akakataa kwenda, toka amefika DC tayari tunausikia tena ubalozi wetu kule, I mean mnyonge mnyongeni!

- However: sina uhakika alifikaje kwenye ubalozi, lakini in her case the end justifies the means!, Wa-Tanzania tuache majungu majungu huyu mama ni kichwa sana na taifa tunahitaji viongozi kama huyu! Creative na Active!


William @ NYC, USA.

Nisingekuwa na simile ningetupia tusi, lakini uvumilivu niliofundishwa wa kuwavumilia wasiofikiri vizuri na wasiofikiri kama ninavyofikiri mimi umenifanya nisite. Hapa watu hawazungumzii chadema, watu wanazungumzia masuala ya kitaifa kama ambayo mama yako na baba yako wanayoyapigia kelele. Nchi hii kwa kweli inaliwa na inaliwa na watu wenye akili nzuri waliosomeshwa vizuri na pesa zilizotoka katika ardhi ya nchi hii na katika miili ya watanzania wenzao. Hao ndio wanaotutia katika mikatba mibovu na dili zinazorudisha nyuma taifa letu. Si suala la kusema nani chademe nani CUF na nani CCM. Hapa ni nani mwizi na nani anatuhujumu. Ingawa najua CCm ina watu wengi wanaofanya mambo mabaya isifike wakati sasa mtu akikemea mabaya aonekane anaikemea CCM ingawa hiyo ndio imekuwa sababu ya kujivua gamba, lakini isiwe tu likisemwa baya basi udhani watu wanaofanya hivyo ni wapinzani. Tupo tunaokubali ukweli na kuikubali hali. Muulize mzee Butiku, Anne Kilango na hata Kinana watakuambia na kukufunza. Jifunze kufikiri kwanza kabla ya kutoa wazo
 
Taifa lilimuomba?????au aliemteua????sijasikia kua taifa limemuomba

Hivi Balozi Mahiga alikorofishana nini na JK mpaka akatemwa na kuokolewa Na Baki Moon? Leo tunaambiwa Maajar, mchapa kazi taifa limemuomba,Isije kuwa Ridhwani ndipo alipooolea, hivi ridhwan aliooa wapi vile? Naomba nikumbusheni
 
- Kazi ya ubalozi ni Presidential appointees, sasa ni uamuzi wa Rais ambao sisi wananchi wa Jamhuri tumempa dhamana kwa kumchagua kisheria kua Rais, ingawa ni muhimu sana in the future hawa Presidential appointees wakawa confirmed na bunge, lakini kwa sasa Rais ana haki ya kumcchgua yoyote yule ndio maana ya Demokrasia inayoitwa the winner takes all kama yetu!

Willie @ NYC, USA.

William mamlaka ya Raisi wetu yanajulikana, kilichoshangaza wengi wakati wa uteuzi wake wa awali huyu mama hakuwa mwanadiplomasia, hakuwa mwajiriwa wa serikali la zaidi alikuwa ni mtu CUF, hapa hatuongelei hypothesis; fuatilia law firm yake na matukio ambayo yameitia serikali kwenye mikataba ambayo haieleweki, kilichofanyika baada ya kuibuka kashfa za Tanesco ndipo huyu mama alipoondelewa na kupewa ubalozi; kila serikali inapokumbwa na kashfa wahusika huondolewa nchini chukulia mfano wa Balali tumeambiwa amefariki Marekani na amezikwa Marekani, kwa mtumishi wa umma Gavana hata Raisi hajui Gavana wake amezikwa wapi? Hata ubalozi wetu ulikuwa na taarifa za juu juu sasa huu si wazimu? Unavyomsifia mchapa kazi mimi nadhani angetufaa zaidi hapa ofisi ya mwanasheria mkuu ili atusaidie kufanunua mikataba. Tunatakiwa tuwe makini sana kwa masuala ya Diplomasia kwani wao ndio wanatuwakilisha ughaibuni, wewe chukulia UN tunapeleka mwandishi wa habari kwenye vyombo kama hivyo ukweli inabidi tupeleke watu waliobobea kwenye mambo ya Diplomasia; hii ndio sababu kubwa hata ukienda kwenye balozi zetu unajikuta kama vile upo wizarani Dar kutokana na utendaji wao mbovu.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom