Ambao hawajaandikisha vitambulisho vya Taifa-NIDA

Ambao hawajaandikisha vitambulisho vya Taifa-NIDA

Kwa nini NIDA wasishirikiane na NEC ili watoe vitambulisho vya taifa/ kadi ya mpiga kura!!
.Hiyo si ingepunguza gharama??

Mawazo yako mazuri sana. Hakuna haja ya kuwa na lundo la vitambulisho ambavyo kazi yake ni kuonyesha makazi na uraia.
 
Hii ajenda ni nzuri sana sasa mimi nina kitambulisho cha mpiga kura na cha mkaazi. Je, hapo naruhusiwa kuandikishwa? Naomba kuelewe ndugu zanguni.
 
Hawa watu ni wasumbufu sana.

Nilifika kwenye kituo chao nikiwa na vielelezo vyote kwajili ya uhakiki...lakini nikasubirishwa kwa zaidi ya saa moja na nusu bila huduma,huku nikiwashuhudia wafanyakazi wakizungumza na simu-mambo yasiyo ya kazi,mara kutembea-tembea pasipo mpango wakati sisi tumepanga mstari n.k nilikerwa na nilikerwa na nikaondoka,hadi hapo nitakapopata nafasi nyingine.
 
Hoja ni nzuri nami naomba kuelimishwa kwani nami ni muathirika wa Hili Jambo. Sikujiandikisha hapo kabla
 
Nilibahatika kuandika namba yao (NIDA) ya simu 0762416666

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Kama bado haujajiandikisha nenda kwenye kituo chochote cha nida na viambatanisho vyako na utapata huduma mkuu..
 
Nashukuru sana mmenifumbua macho manake nilikuwa nahofu kwema nimepitwa kumbe zoezi ni endelevu!
 
aa wanazongua sana.
liwalo na liwe nimezaliwa tz cheti chakuzaliwa ninacho..

wakisema sio RAIA wanipeleke huko kunakostahili
 
Sitojiandikisha mpaka nijue hatima ya muungano. 👎
 
Mawazo yako mazuri sana. Hakuna haja ya kuwa na lundo la vitambulisho ambavyo kazi yake ni kuonyesha makazi na uraia.

Halafu wataishije mjini?

Hizo ni project tu za watu,ni sawa tu vidhibiti mwendo,au vizima Moto!!Watu lengo Lao ni kupiga hela sio kutengeneza utambulisho,ndio maana unaona kuna mambo meeengi ambayo Yana malengo yanayofanana!!!!
 
Jamani ,hivi sasa utaratibu ukoje?Mimi nilijiandikisha mwanzo kwenye kata yangu na jina langu likabandikwa.Sasa utaratibu ukoje !na ofisi za kinondoni ni wapi jamani .Unaaannzaanzaje ?Tujuzane basi
 
Mmmm bandiko la 2014! Jamii forums threads never expire.
 
Wanajamii nauliza kwa wale ambao hawajaandikisha kabisa vitambulisho vya Taifa je kuna utaratibu gani wa kumuwezesha kuandikishwa na kuwemo katika orodha ili hatimae kupata kitambulisho pale vitakapotoka? .
majibu ya kistaarabu waungwana naamini wengi wenu ni wasomi na wastaarabu sana, msaada tafadhari heshima kwenu wakuu
Mkuu mbona karibu kila wilaya kuna ofisi ya NIDA!kila siku zoezi linaendelea tu!we nenda ofisi ya mkuu wa wilaya iliyopo karibu ulizia zoezi lipo linaendelea tu kila siku,mimi juzi nimekwenda mkuranga ofisi ya wilaya nimejiandikisha.
 
Mimi kila siku nakuta ofisi ya mtendaji imefungwa hadi nimezira.
 
Back
Top Bottom