Amapiano Special Thread

Amapiano Special Thread

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
5,351
Reaction score
20,101
Amapiano ndio habari ya mujini kwa sasa kunako sekta ya burudani hasahasa kiwanda cha muziki. Kama Amapiano ni jina geni kwako basi sikiliza wimbo wa Mama Amina wa kwake Marioo ft Sho Madjozi na utakuwa umeshaelewa hapa nazungumzia aina gani ya muziki, hiyo ndiyo Amapiano kutoka bondeni kwa Wazulu.

Amapiano1.jpg



AMAPIANO NI NINI?
Amapiano ni mtindo wa muziki wa "House" ambao chimbuko lake ni Afrika Kusini. Mtindo huu uliibuka Afrika Kusini mnamo mwaka 2012.

Amapiano (Piano kwa lugha ya Kizulu) ni mseto wa muziki wa deep house, jazz na lounge music wenye sifa ya synths, airy pads na basslines pana na za kupendeza.

Muziki wa Amapiano una sifa ya kipekee kwa kuwa na high pitched piano melodies, Kwaito basslines, low tempo 90s South African house rhythms na percussions kutoka aina nyingine ya muziki wa wenyeji(local) wa house unaoitwa Bacardi.
Amapiano2.jpg



ASILI.
Ingawa aina hii ya muziki ilipata umaarufu katika mji wa Gauteng, kuna utata mwingi juu ya asili yake, na akaunti anuwai za mitindo ya muziki katika vitongoji vya Johannesburg - Soweto, Alexandra, Vosloorus na Katlehong.

Kwa sababu ya kufanana kwa aina hiyo na Barcadi, watu wengine wanadai aina hiyo ilianzia Pretoria na imekuwa mjadala wa kuendelea juu ya asili ya Amapiano.
Amapiano4.jpg



UMAARUFU
Mwaka 2020 aina hii ya muziki ilipata kujiongezea umaarufu kote bara la Afrika na kuongezeka kwa digital streams na mafanikio ya kuingia katika chati za juu za muziki katika nchi mbalimbali tofauti na Afrika Kusini.
Amapiano3.jpg



Tanzania.
Kwa sasa msanii aliyefanikiwa kutoa hit song ya miondoko hii ya Amapiano ni Marioo na ngoma yake ya Mama Amina akiwa amemshirikisha Sho Madjozi & Bontle Smith.

Wengine ni Amber Lulu na ngoma yake ya Shingapi, Damian Soul na ngoma yake ya Mapopo.

[/b]
 
Nimetokea kuwa shabiki sana wa aina huu ya mzki hasa ni baada ya kusikia wimbo wa mario hasa napenda kipande cha yule dada mwingine achana sho mdjoz.

Na hiyo focalistic ni fire.
Nipeni zingine mnazojua kali kali.
 
Huu mziki ukipigwa beat lake lazima uchezeshe kichwa au mguu penda usipende.

Naona unazidi tu kupenya hata nje ya SA, hata Naija nao wameanza kublend mziki wao na amapiano
 
1.Blaq diamond-woza My love
2.Costa Titch-big flexa
3.daliwonga-abomvelo
 
1. Musa keys ft Louis - Selema popo
2.Papi Cooper - Isiphithiphiti
 
Kuna nyimbo natafuta sijui inaitwa fantastic au msanii anaitwa hivyo,ilitoka mwaka Jana,binge Moja la nyimbo
 
Back
Top Bottom