PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Licha ya kuwepo kwa taarifa na tetesi za uwezekano wa kutokea maandamano katika maeneo mbalimbali nchini, hali ya amani imetawala katika mji wa Singida, huku shughuli za ulinzi na usalama zikiimarishwa katika maeneo yote muhimu.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanyika mapema leo katika mitaa ya mji wa Singida unaonyesha kuwa baadhi ya wafanyabiashara hawajafungua maduka yao wakisema wanachukua tahadhari kutokana na taarifa hizo, ili kuepusha hasara iwapo kutatokea vurugu au uvunjifu wa amani.
Aidha, imebainika kuwa vituo kadhaa vya mafuta vimefungwa, hatua inayodaiwa kuchukuliwa kwa tahadhari ya kuangalia mwenendo wa siku nzima. Baadhi ya madereva walionekana wakizunguka kutafuta huduma katika maeneo mbalimbali ya mji bila mafanikio, jambo lililosababisha msongamano mdogo katika vituo vilivyoamua kuendelea na shughuli.