Mara nyingi viongozi wetu huimba wimbo wa amani kana kwamba ni mali ya kila mmoja wetu. Lakini ukweli mchungu ni kwamba amani hiyo ipo kwao tu—sisi wananchi wa kawaida hatuioni wala kuifaidi.
Ni sisi tunaotekwa.
Ni sisi tunabambikiziwa kesi.
Ni sisi tunadhurumiwa.
Ni sisi tunaotukanwa na kunyanyapaliwa kwa sababu ya miradi ya serikali.
Na ni sisi haohao tunaobeba jukumu la kulipa kodi.
Swali linabaki: inakuwaje mtu aje kututaka tuheshimu amani ambayo kiukweli haipo? Kisingizio kikubwa kimekuwa kwamba wale wanaotuhimiza familia zao hazipo hata hapa nchini. Hii imekuwa kama turufu ya kila mara.
Lakini kumbuka—sisi si wa kwanza kutaka mabadiliko, na kadri muda unavyosogea, shinikizo la wananchi litafikia hatua ya kutaka mwanga wa kweli wa mabadiliko uangaze.
Bahati mbaya kwao, viongozi hawa ndio wanatulazimisha kufanya tusiyoyataka. Wameshindwa kujua namna ya “kula na kipofu kwa heshima,” wamezidi kufurahia madaraka kiasi cha kujisahau kabisa.
Ukweli ni kwamba, Tanzania (Tanganyika) haijawahi kupata uhuru wa wananchi wote. Uhuru walioupata ni wao viongozi pekee—sisi wengine bado tupo kwenye minyororo ya umasikini, manyanyaso na kukosa sauti.