Amani ni vitendo na si maneno

Mshughulishaji

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,351
1,875
Miaka ya nyuma tulikuwa tukiambiwa swala la kulinda amani na kweli tuliona viongozi wakiyaishi waliyoyasema,

Kwanini zama/kipindi hiki tunasisitizwa na ndio kwanza inaonekana kutoweka?

Mfano kumeshamiri hivi karibuni haya matukio ya kutekwa/kupotezwa na hata ule uhuru wa habari umekuwa tishio,

Tatizo ni lipi hasa ni wahubiri wa hiyo amani au ni imani imewatoka wahubiriwa?

Karibuni kwa michango.
 
Yule mwingine anahubiri amani na kuomba kuombewa ila anayofanya ni tofauti kabisa.
 
Tatizo ni maslahi tu jamani,wakati tumeongezeka kwa idadi rasilimali ni zile zile,elimu ni ileile,mitazamo ni ile ile,ubunifu haupo, bado tunaimani zile zile za kusoma_kufaulu_kuajiriwa=mshahara.Maisha tayari. Hakuna amani kwa mwenye njaa.
 
Back
Top Bottom