Amani na Utulivu

Amani na Utulivu

Mulama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
3,045
Reaction score
1,820
Wadau nimeguswa na picha hii nikaona ni share nanyi, imenishangaza hawa makada wa chama kinachojivunia kuleta amani na utulivu nchini, kwa kitendo chao hiki je amani inaletwa na wao kweli?!
 
Wadau nimeguswa na picha hii nikaona ni share nanyi, imenishangaza hawa makada wa chama kinachojivunia kuleta amani na utulivu nchini, kwa kitendo chao hiki je amani inaletwa na wao kweli?!

Muone yule jamaa wa kwanza kulia (ukiwa unaitazama picha) alivyo na jiwe kubwa?!
Muone shekhe alivyo onyesha jazba?!
Mtazame kada mwenye bahasha anavyojiandaa kurusha jiwe?!

Hapo ndipo tulipofikia kwa sasa...

Nadhani 2015 patakua pagumu sana!
 
Tena nimeambiwa huyo mwenye jiwe kubwa ni ndugu yake Mwigulu!
 
Tena nimeambiwa huyo mwenye jiwe kubwa ni ndugu yake Mwigulu!

Sidhani kama walistahili kumfanyia hivyo huyo jamaa, ukichukulia kwamba lazima kulikua na vyombo vya ulinzi kama kawaida mikutanoni kwao!
Wanazidi kutufundisha. Hakuna wa kulaumiwa!
 
hakuna amani hapo Mulama
Juzi wakati wa kusherehekea siku ya sheria duniani Jaji alikemea watu kujichukulia sheria mkononi, lakini kama uvunjifu huu unaanzia ndani ya ccm serikali itawezaje kuudhibiti?!
 
Wadau toeni maoni yenu juu ya nini kifanyike kukomesha vitendo vya kutokuheshimu sheria hasa vinapofanywa na viongozi wenye dhamana ya kusimamia sheria?
 
kafuata nini kwenye mkutano wa watu? watovu wa adabu ni vema wakaadabishwa on the spot.

Inavoonekana kwenye picha ni wao wanamkimbiza ingekuwa kawafuata kungekuwa na sehemu walipokaa inayoonesha wanafuatwa!
 
Ni dhahiri ya kwamba ccm na serikali yake vimeshashindwa kazi. Na leo hii tumemsikia Dr wa ukweli Slaa akimjibu Tendwa ya kuwa hili swala liko tayari kwenye vyombo vya sheria, pale Tendwa alipotaka CHADEMA ijieleze kwa maandishi kuhusu 'kuleta vurugu' kunakodaiwa na ccm na vikaragosi vyao. Bado tuna mwendo mrefu sana mpaka haki ya mwananchi inayopiganiwa na CDM itakapopatikana. Lakini safari imeshaanza, hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke.

Poleni sana makamanda, lakini penye ukweli kila siku uongo hujitenga!

People's Power!
 
Chama cha wauwaji.
Wameoza wote, kwa viwango (grade) tofauti.
Mungu Ibariki Tanzania!
 
Muone yule jamaa wa kwanza kulia (ukiwa unaitazama picha) alivyo na jiwe kubwa?!
Muone shekhe alivyo onyesha jazba?!
Mtazame kada mwenye bahasha anavyojiandaa kurusha jiwe?!

Hapo ndipo tulipofikia kwa sasa...

Nadhani 2015 patakua pagumu sana!

wasee wasee! Kama mbaya na iwe mbaya. Leo wanajivunia kuwa wakenya.
 
Kinachonisikitisha hawa jamaa si tu kwamba wanamjeruhi mtu bali hata nyuso zao zinaonesha chuki na roho mbaya ya kuua kwa dhamila! Ndo maana hata polisi wao wanaua watu na kuchukuliwa poa.
 
Back
Top Bottom