Amani na picha ya amani

george kessy

Member
Jun 24, 2017
29
75
Habari wakuu

Me naamni ya kwamba Moja kati ya mahitaji muhimu sana ya binadamu katika maisha yake ya kila siku ni amani.katika kitabu cha George Kaithori cha Make Peace Your Target ,amani ya kwanza kabisa anayoihitaji mtu siyo ile inayotokana na kutokuwepo kwa vita.Amani ni ile hali ya utulivu wa akili na mtuamo wa moyo wake.hii ni hali ambay anaipata mtu anapokuwa hana usumbufu au mtibuko wa aina yoyote ile akilini na moyoni mwake.

Maurus mwandishi maarufu wa vitabu vya saikolojia wa india ,anatukumbusha kwamba ili mtu binafsi aweze kuishi kwa amani ya akili yake na mtuamo wa moyo wake inampsaa azingatie miiko ya misingi katika maisha.

Kwake iwe mwiko kujigamba,kujisifu ,kamwe asikimbilie kukaa kwenye viti vya mbele katika hadharaa yeyote ile Aidha kamwe asiwatumie watu wengine kwa faida zake binafsi,ni mwiko kuwanyanyasa au kuwadharau watu wengine.kwa ujumla makatazo yote hapo juu yanatuonyesha kuwa adui mkubwa ni ubinafsi. Mtu atakuwa na amani atakapoa acha ubinafsi na kuwajali watu wengine.

Picha ya amani
Hapo zamani za kale palitokea mfalme mmoja ambaye alitaka kuona amani inaonekajae machoni.hivyo aliagiza wasanii wote nchini kwake wamchoree picha inaonyesha amani kisha atatoa zawadi kwa picha atakayoipenda kuliko zote.Agizo lile lilisambaa katika ufalme wake wote,na wasanii wakaingia katika shindano.Baada ya muda mfalme akaletewa mamia ya picha .
Alizichambua kisha akabakiwa na picha mbili.

Moja ilionyesha madhari nzuri iliyotulia ambapo mlima ukiwa umejitokeza nyuma na ziwa lenye maji mazuri yaliotulia na yenye rangi ya bluu ,na mbingu yenye rangi ya samawati ilikuwa imefunikwa kwa mawingu mazuri yenye rangi nyeupe na bluu

Picha ya pili pia ilionyesha mandhari yenye mlima na ziwa ,lakini katika picha hii mbingu isiyopendeza ilikuwa ikigeuka rangi nyeusi,mvua nyingi zilikuwa zikileta kiza katika mandhari ile na mwanga wa radi ulikuwa ukionekana ukiwaka hapa na pale katika ziwa.Ziwa lilikuwa limevurugwa kwa maporomoko ya maji.Nyuma ya ziwa ,mbali kidogo na maporomoko ya maji yale,kulikuwa na kichaka kidogo ambapo ndege alikuwa ametengeneza kiota chake.Ndege alikuwa amekaa pale kimya akifanya kazi yake,alikuwa akilalia mayai katika dhoruba lile.

Katika picha zile mbili ,mfalme alichagua ile picha iliyokuwa ina vurugu nyingi.Alipoulizwa kwanini alipenda ile yenye kuonyesha vurugu alijibu "kwa sababu kuwa katika amani haina maaana kuwa mahali pasipokuwa na kelele,vurugu au kazi ngumu.Amani maaana yake kuwa katikati ya vitu vyote hivyo,lakini bado ukawa umetulia katika moyo wako,hiyo ndiyo maana ya amani.

Asante.
 
Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
5,058
2,000
Inategemeana na makubaliano yao kabla na baada ya kufanya shoo nani alipwe zaidi, ndio maana hata leo Mh Magufuli amewapatanisha Alikiba na Diamond
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,109
2,000
Ana kwa ana na msukule.
Siku ya sabasaba jumanne, mida ya jioni, kama saa moja jioni nilipata ajali, kulikuwa na mvua, tulikuwa barabara ya Mwai Kibaki mitaa ya Kawe Beach, jirani na njia ya kwendea Mediterranio Hotel gari ya mbele yangu ikafunga break ghafla sana, nikaigonga kwa nyuma upande wa kulia na kuvunja taa ya BMW X5 new model.
Nikasimamisha gari na kushuka ili niangalie uharibifu.
Akashuka mzee wa makamo, kama miaka 60, anafoka, unajua gharama ya hii taa, unajua bei yake? Nikamwambia samahani. Akajibu samahani yako itanisaidia nini? Leta leseni yako.
Nikaona isiwe taabu, nikampa leseni yangu, akaenda kuifungia kwenye gari yake, akarudi na kunipa business card yake. Akasema Jumapili 12/07/2020 saa nane mchana unipigie.
Jana jumapili, saa nane kasoro robo nikampigia simu, nilikuwa mitaa ya Sinza nakula kitimoto 🐽🐷🐖 na cocktail Konyagi na wine🍷.
Nikachukua simu na kumpigia jamaa, sipendi kumtaja kwa jina wala kabila lake.
Jamaa akaniamuru nichukue pikipiki fasta nimfuate nyumbani kwake Mbezi Beach.
Nikachukua bodaboda hadi Mbezi Beach mitaa ya Kwa Zena Kawawa.
Nikamjulisha kuwa mimi tayari nimefika kwa Zena, basi akanipa maelekezo ya kunifikisha hadi kwake.
Nilipofika tu getini, geti likafunguka lenyewe, mimi na bodaboda wangu tukaingia ndani.
Jamani kuwa watu wanaishi high life, bonge la crib, swimming pool nzuri, bustani kali, ndege wazuri kama hauko Dsm, wanacheza na kuruka huku na huko.
Tukaa kwenye viti vya bustanini, mfanyakazi akaja akamuuliza bodaboda anakunywa nini, aagize chochote bila hofu.
Akaniita kwa jina langu akaniambia nimfuate, mzee ananiita ndani.
Nikaingia ndani, sitting room kubwa, ya kisasa sana, very organized, nikakaa hapo nashangaa shangaa uzuri wa jumba lile.
Baada ya kama dakika ishirini, jamaa akaja, nikamsalimia, akanipokea kwa uchangamfu wa hali ya juu sana.
Akawa mwema sana kwangu, akanipeleka kwenye ki mini bar kilichopo hapo ndani, yeye akachukua pombe ambayo hata sijawahi kuiona inaitwa Dom prognon sina uhakika sana. Akaniambia nijihudumie, mi nikachukua Jack Daniels ndogo na kuimimina kwenye glass.
Kimya kikatawala kama kwa dakika tatu hivi.
Jamaa akavunja ukimya, akanisifia kuwa mimi ni kijana mwaminifu, angekuwa kijana mwingine asingepiga simu, wala asingehangaika na kulipa taa ya bei mbaya.
Nikaendelea kumsikiliza, kisha nikamsihi, anisamehe, anirudishie leseni yangu.
Akasema wa kunisamehe si yeye, gari sio la kwake, ila mwenye gari yupo ndani kapumzika tumsubiri.
Akilini, nikapata picha kuwa gari itakuwa ni ya mkewe, nikaanza kujiandaa kisaikolojia namna ya kukabiliana na mwanamke tajiri mwenye kiburi, jeuri na nyodo.
Zikapira kama dakika ishirini, jamaa akasema turudi sitting room.
Tukaenda, akamwita dada kisha akaagiza amuite XXXX.
Nikajiweka sawa kukabiliana na jimama la kitajiri.
Baada ya kama dakika tatu, dada akaja na li mtu linatisha, limevalishwa t shirt kubwa ina bendera ya Tz.
Anatisha, anachuruzika maudenda. Mtoto si mtoto, kijana si kijana, umri hautabiriki.
Nikaambiwa nimuombe msamaha, maana huyo ndiyo mwenye gari.
Nikapiga magoti, nikawa nimevurugwa aisee, naongea tu maneno mara niuite huo msukule mfalme, mara niuite boss, mara uncle, mara kaka... ili mradi najisemesha.
Msukule ule ulipiga kelele mpaka nikashtuka, ukacheka sana, basi yule jamaa akaniambia niinuke, na pia XXXX (msukule) amenisamehe na amenipenda sana, kwa hiyo kuanzia sasa mimi ni rafiki wa msukule.
Akanipa leseni yangu. Hakika nilikuwa najiona kama niko ndotoni, kwenye ndoto ya kutisha na ya kuogofya sana.
Nilikuwa naona kama muda hauendi, nilitamani upepo unichukue, unitoe ndani ya jumba lile.
Hakika nilijiona ndio siku yangu ya mwisho, nikawa nasali kimoyomoyo, nilikata tamaa ya kutoka kwenye jumba lile nikiwa hai.
Basi, jamaa akaniambia sasa naweza kuondoka kwani bodaboda amekaa nje muda mrefu.
Nikaanza kuinuka kitini ili niondoke.
Jamaa akasema sijamuaga rafiki yangu.
Akamwambia dada anipeleke nikauage ule msukule.
Nikamfuara dada, tukapiga kona, tukakuta kuna lift, akabonyeza twende juu.
Tukafika, mlango una fingerprint reader, akaweka dole gumba, akafungua mlango, akaniacha mle ndani kisha yeye akatoka.
Mle chumbani kulikuwa ni kuzuri sana, chumba kina makorokoro ya watoto, chumba kikubwa, kina vigari, Spider-Man, Ben Ten, na TV kubwa inaonyesha makatuni.
Hapo nimevurugwa, sijui nifanye nini, nimefungiwa.
Nikaogopa sana, nikaanza kuhisi labda nimeletwa pale ili nigongwe na ule msukule. Nikawa nina mawazo mengi sana, baada ya kama dakika kumi na saba, mlango ukafunguliwa, akaingia jamaa, akasema naona uko na rafiki yako. Nikajibu ndio tunaangalia katuni.
Basi, tukatoka mle chumbani, akanishusha chini.
Sebuleni akauliza kama nina mke na watoto, pia akaniuliza kama nimejenga ama nimepanga.
Nikamjibu nina mke na watoto wawili, na nimepanga.
Basi akanipa laki tatu, akasema nikanunue chakula cha watoto, akanipa laki tatu nyingine, nikalipe umeme na maji, akanipa million tatu nikalipe pango ya nyumba, laki tano ya kutengenezea gari yangu, akanipa na elfu hamsini ya kumlipa bodaboda na akanionya kwa msisitizo, hela ya bodaboda nisipunguze hata shilingi moja. Na akasema niwe naenda kila jumapili kuongea na rafiki yangu.
Nilipotoka nje, nikanwambia bodaboda akimbize sana hadi nyumbani.
Nilipofika nikamwuuliza ananidai bei gani, akasema elfu kumi na tano. Nikampa elfu hamsini, jamaa hakuamini.
Nilipofika ndani, nilipitia kulala, nikalala sana. Mida ya saa saba usiku, usingizi ukakata, nikamsimulia mama watoto kila kitu.
Kashauri hizo hela tuzifanyie maombi na tusizitumie kwani ni hela za kipepo.
Kwakweli siko vizuri, leo nimeshindwa hata kwenda kazini.
Kuumwa siumwi, uchovu, hofu, mwili kama sio wangu, breakfast imenishinda, yaani nimevurugwa mazima
 
Mkuu pole sana cha maana cha kufanya kwa sasa ni kujitahidi kutuliza kichwa .
Pili ondosha mawasiliano na huyo bwana na ingekuwa vzuri hata eyo line ungevunja ili utulie uwe kwa amani.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,109
2,000
Mkuu pole sana cha maana cha kufanya kwa sasa ni kujitahidi kutuliza kichwa .
Pili ondosha mawasiliano na huyo bwana na ingekuwa vzuri hata eyo line ungevunja ili utulie uwe kwa amani.
Nimedelete WhatsApp, na laini nimevunja. Nimechukua laini yangu ambayo huwa siitumii, ile nimeiweka tu KWENYE simu ikaingia sms ya Tigo pesa, nimeongezewa sh. Laki tatu kutoka kwa wakala, Kisha baada ya muda kidogo ikaja sms nyingine, rafiki yako XXX AMEKUMISS, KAKUTUMIA LAKI TATU YA SODA.
Nimeshangaa, wameijuaje namna yangu ambayo sijaitumia siku nyingi??
 
Acha kutumia eyo simu nadhani wanaweza kuanza kutrack eyo simu na siyo line,nafikri wataalamu wa maswala ya IT watakuwa na uelewa zaidi.
Jingine jaribu kusogeza tukio hili kwa wazazi na ndugu ambao unaona wanaweza kukupa msaada bila kukusema.
Cha mwisho jaribu kumahirikisha kiongozi wako wa dini uonea atakupa mbinu namna gani ni hayo tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom