Incredible
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,031
- 1,604
Watanzania wenzangu, binafsi nilivutiwa sana na kauli ya Rais Kikwete aliposema anapenda tudumishe amani na majirani zetu wa Rwanda. Lakini nakatishwa tama ninapoona Kikwete huyohuyo ameagiza Wanyarwanda wasiokuwa na vibali waondoke. Nikweli hairuhusiwi mtu asiye na kibali kuishi nchini mwetu. Lakini agizo la Kikwete limekuja kipindi kibaya. Kwanini agizo hili lije wakati huu ambapo uhusiano wetu unadorora? Mimi nadhani tumjulishe rais wetu kwamba adui wetu siyo Rwanda bali maadui tulio nao ni Rushwa, Ufisadi, Madawa ya kulevya, Udini, Umaskini, Kushuka kwa kiwango cha elimu n.k. Ili katika miaka 10 ambayo anaongoza nchi hii yaani miezi 120, basi atumie miezi 18 iliyobaki walau aanze kupambana na hawa maana hawa ni maadui wa ndani. Maadui hawa wa ndani hawaitaji mizinga, mabomu wala damu za wanyarwanda au watanzania wasio na hatia.