kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,936
Israel, Palestine, Somalia, Ethiopia, Uarabuni, Misri na Sudani ni mataifa ambayo watu wao wanaomba Mungu sana, lakini vitendo vya uvunjifu wa amani vimekithiri pia. Kuhesabu waliokufa, waliojeruhiwa na wanaozikimbia nchi zao ni mambo ya kawaida kwao. Hii inamaanisha kuwa kuomba Mungu pekee hakutoshi kudumisha amani na utulivu ndani ya nchi. Hivyo kuna umuhimu wa kutafuta nyongeza katika kudumisha amani yetu badala ya kutegemea maombi pekee.