PreGE2025 Amani Golugwa: Wasira wewe siyo msemaji wetu, acha kutusemea kitu ambacho hukielewi

PreGE2025 Amani Golugwa: Wasira wewe siyo msemaji wetu, acha kutusemea kitu ambacho hukielewi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Wakuu,

Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara, Amani Golugwa amesema watu wa CCM wamegeuka kuwa wasemaji wao, lakini wao msemaji wao ni mmoja tu, Brenda.


Anasema ukiwasikiliza wasemaji wa CCM kama wasira, makalla wamekuwa kama wasemaji wao, wanawasaidia kufikisha ujumbe lakini, wakome maana wanaharibu kitu ambacho hata hawaelewi. Anasema waache mara moja kwani ni wao ndio wanajua namna ya kuelezea kauli mbiu yao, ambapo kishwali chake kinasema Bila Mabadiliko Hakuna Uchaguzi.

Ameongeza kuwa Mzee wasira aache kuongea kitu ambacho hakielewi, watamwelewesha mabadiliko yanayotakiwa, akisema kuwa ni vigumu sana pengine kuyakubali lakini sauti ya watu/wengi itakayopigwa kipindi hiki masikio yake (wasira) yataachia na ataelewa wanachomaanisha.

Mkutano huu na waandishi wa habari umefanyika katika ofisi ya Makao Makuu ya Chama Mikocheni, Dar.
 
Wakuu,

Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara, Amani Golugwa amesema watu wa CCM wamegeuka kuwa wasemaji wao, lakini wao msemaji wao ni mmoja tu, Brenda.

Anasema ukiwasikiliza wasemaji wa CCM kama wasira, makalla wamekuwa kama wasemaji wao, wanawasaidia kufikisha ujumbe lakini, wakome maana wanaharibu kitu ambacho hata hawaelewi. Anasema waache mara moja kwani ni wao ndio wanajua namna ya kuelezea kauli mbiu yao.
Huyu Mzee wasira wasipompumzisha kuna siku atatukana😅😅
 
Back
Top Bottom