Ama kweli nimeamini kikulacho kinguoni mwako...sitakaa nimuamini tena mtu yoyote.

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Habari za majukumu wakubwa na wadogo..
Niko na rafiki yangu wa karibu mfanyakazi mwenzangu, jirani yangu wa damu.
Ndani ya kipindi hiki kidogo cha mda wiki kama mbili nilimuagiza rafiki yangu aninunulie tv ya inch 32 used pamoja na king'amuzi cha Zanzibar cable.

Nilimwambia TV ya inch hiyo kutokana na bajet yangu maana kuna mambo mengine ambayo nilitaka niyafanye kwa wakati huu..
Alizunguka karibia wiki mzima hajaichukua.

Sasa kila nikimuuliza anajaribu kunambia tusubiri mzigo ufunguliwe..
Hapo sikuwa na shaka kwasababu nilikua nimeshamuachia jukumu hakuna shida. Mwisho wa siku ananitumia ujumbe kachukua ya inch 42 kwa maana ya kwamba et ya 32 hakuna kwa hapo alipozowezea.

Ikabidi achukue huku nikiwa na deni la ziada nikaamua kumpa tu hiyo pesa akalipe maana alinambia amekopa.... Hilo ni suala dogo maana hela ilikua ya kawaida.

Nakuja kwenye suala la mapatano ya kununua nyumba.

Kuna sehemu ya kwanza alinambia ameipata na bei yake mwenyewe kaanza milioni 23 lakini kwa bahati akipapatua akakubaliana nae mwisho 18.5m... Hapo tukaacha kama yalivo huku nikisubiri pesa zangu za kuja kununulia...

Nilisikia ipo na sehemu nyingine pia nikamuagiza aende..

Huko alinambia mwenyewe anataka m25 lakini yeye ataongea nae mpaka 24 ipatikane... Katika na hapo nilijaribu kuwa mvumilivu huku nikijaribu kufanya uchunguzi kwa kumuagiza wife kila step anayopita yeye..

Mapatano ya nyumba ya kwanza, rafiki yangu alinambia mwenye nyumba mwisho alitaka m18.5 majibu ya wife mwenye nyumba mwisho alitaka 17.5.

Upande wa nyumba ya pili, rafiki alinambia mwenye nyumba amekubaliana nae bei atapunguza kidogo ila hakunitajia ni kiasi gani mwenye nyumba anahitaji...
Leo siri zote zimefichuka baada ya wife kufatilia..

Amezungumza na mwenye nyumba kamwambia mwisho ni m23.5, lakini kwa rafiki yangu kipenzi alinamwambia mwenye nyumba mimi nitakapokuja kuichukua aseme kaniuzia 24 na aandike hivo hivo..

Ila kwakuwa mwenye nyumba hapendi kudhulumu alimmwaga na kumwambia kwamba "sipendi kuandika uongo na pia kama ni hakiba yako hiyo pesa atakupa lakini sio kwa njia ya utapeli" na hayo maneno kamwambia wife ndio maana nikayapata mimi. Kumbuka rafiki alimwambia aandike hivo kwa kisingizio kwamba eti kuna madalali wengi lol...

Sasa mwenye nyumba akamwambia wife "kwanini mnakua na madalali wengi haujui pesa itawatoka nyingi?" Hapo wife akawa na mashaka ya kwamba kumbe kikulacho kinguoni mwako.

Sasa hivi rafiki nimemtoa moyoni kabisaa.. Sihitaji kumshirikisha tena jambo lolote.. Lakini kwa bahati nzuri sijamwambia na pia sipendi kumwambia maana atakuja kujitenga baada kumwambia ukweli kikubwa kuliko yote nataka nimpige chenga kwa kila kitu bila kujua aone nimeshaganikisha tu.
 
Ndg.

Kikulacho ki mwilini mwako siku hizi mkuu.

Kilishahama kwenye nguo kikahamia mwilini long time.
 
Mkuu hio ni kawaida ya binadamu, mtu pekee ambae ungemtuma na asingekuibia ni yesu peke yake,

Hapo ukute hata mkeo nae kafanya hivyo hivyo au atakupiga kwenye kodi ya kupangisha,

Cha kukushauri usiue urafiki na huyo rafiki yako,
Kuwa na mazoea ya kwenda wewe mwenyewe kwenye ishu zako,

Usiongeze maadui ongeza marafiki,
Huyo udhaifu wake ushaujua,
So next time hakusumbui tena.

Nii hayo tu mkuu
 
Matajiri raha sana
Anakaa tu anaagiza

Hivi kuna mtu hapendi pesa
Mie hata Dukani siwezi kumtuma mtu nakwenda mwenyewe
 
Shida na raha kwa nini unamtumia rafiki kwenye shughuli nyeti kama hizo? wewe mwenyewe upo na mzima kabisa? na inaonekana upo zenji, zenji hakuna foleni za kutisha barabarani na maduka ya TV used ni mengi mnooo, issue nyeti unaingia mwenyewe front kaka.
Hapana mkuu sipo Tz..
 
Kwani huyo unaemtuma yeye hana familia? Cha juu chenyewe kidogo tu umekuja kutoa povu huku!
 
sasa huyo rafiki yako yy hana kazi zingine za kufanya? kama ww ni mgeni jijini huyo rafiki yako ni dalali na hiyo ni kawaida tena mbona anakupiga padogo sana.
 
Pia hujui kwnye negotiation mwanamke ni rahisi kupunguziwa Zaidi., hiyo nyingine huwa wanalipana umefanya kosa kubwa sana kumtumia mke wako kwenye inshu za hivyo atakuja kuliwa dkk ambayo hujategemea
 
Back
Top Bottom