Ama kweli Nabii hakubaliki kwao.

Ama kweli Nabii hakubaliki kwao.

TANO MLIMA

Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
92
Reaction score
49
huyu jamaa anajitahidi kweli kuleta maendeleo ya kweli
lakini kuna baadhi ya watu hawaridhishwi na wanapuuzia utendaji kazi wake!(magufuli)

-anajenga reli (treni ya umeme) ambayo kwa tanzania ilijengwa miaka zaidi ya mia iliyopita,leo anaijenga.!!

anatimiza mradi mkubwa wa umeme wa stiggler's gorge utakaozalisha umeme mwingi! zaidi ya uliopo tanzania kwa sasa!

-ameongeza ukusanyaji wa mapato tanzania

-kaleta mwelekeo mpya wa uchibaji madini na kwa kiasi utanufaisha watanzania

kapunguza rushwa(ufisadi) pia kuondoa watumishi hewa na wenye vyeti feki!

Pia meli itakayotengenezwa ziwa victoria.haijawahi kutengenezwa tangu 1996!

-bila kusahau elimu bure!

-Pia nidhamu na heshima ya kazi imerejea na urasimu maofisini wa njoo kesho,tuko bize,amesafiri nao pia umepungua!

na mengine meeengi!

Yaani ni rais mwenye hamu na mipango ya kuwatumikia watanzania wote

napenda huyu jamaa aendelee tu kutawala maana hata tukiwaleta wale wengine ni sawa na kuleta walaji wapya wa kodi za watanzania!
 
Ameongeza ukusanyaji mapato halafu wanafunzi wananyimwa mikopo we wa wapi aisee
 
Anakubalika sana tu. Sababu anaeleza mapato yameongezeka na wakulima wana pata ruzuku na wanalima na kuuza vizuri kwa faida, mbaazi soko zuri, wafanyakazi wamepandishwa madaraja yao, deni la taifa limepungua, mikopo wanafunzi wanafurahi kupata 100% ile bombadia imeshanunuliwa kama walivyojinadi halafu wameanzisha mahakama ya mafisadi kina Mkapa wako jela hivi sasa
 
Shilingi daima ina pande mbili.. Geuza shilingi yako uangalie kama upande wa pili unafanana na wa kwanza
Usichanganye mwanga wa mwezi ukadhani ni wa jua
 
Hayo mapato mbona hatuyaoni? Elimu bure...hivi unajua jinsi walimu na wanafunzi wanalivyo na mazingira magumu kwa sababu ya hiyo elimu bure? Watoto wa walala hoi hawapati mikopo? Wafanyakazi hawaongezwi mishahara? Hayo madeni yananayokopwa kinyemela je?

Kama gharama za ujenzi wa hostel za udsm tu tumedanganywa,kwanini tusiamini kuwa hata hili la mapato kupanda pia tunadanganywa?
 
Back
Top Bottom