Habari zenu wanajamvi,
Kila nikiangalia nashindwa kuelewa watoto wa kizazi cha leo watakuja kuwa watu wa namna gani. Siku hizi familia zilizo nyingi hususani za mjini watoto wanalelewa na wadada wa kazi yaani house girl.
Unakuta watoto wanampenda house girl kuliko hata mama yao, hapa ukijiuliza hupati picha mwenendo na ukuaji wa hawa watoto. Unakuta wazazi wote wawili wako busy kwelikweli na utafutaji mali, yaani hawana mda japo wa siku kadhaa kwa wiki za kuweza kukaa na watoto wao japo kujua maendeleo yao kiafya, kielimu na hata tabia zao kwa ujumla.
Wazazi wakitoka asubuhi wanawaacha watoto wamelala na jioni wanarudi watoto wamelala, kila kitu dada wa kazi na ndio mtoa ripoti kwa wazazi nani anaumwa au nani anatatizo gani.
Ndio maana unakuta mtoto anakuwa na tabia za ajabu mpaka wazazi wanaduwaa kazitoa wapi, wengine hawataki majukumu kabisa unakuta dogo ana mwaka mmoja tu tayari anakimbizwa baby care.
Tafakari, chukua hatua.