Ama Dr Slaa, Mbowe mmoja aende CUF au Lipumba, Seif mmoja aende CHADEMA kutii UKAWA

Yericko umeandika vyema leo, lakini wanazi wa chadema watakuja kuanza kukutukana hapa maana wao hupenda kusikia mazuri tu masikioni mwao!

wewe ndo unawaza kutukana, hakuna mchadema anayetukana hoja kama hizo zenye kulisha ubongo hayupo, hoonger yericko nyerere
 
Ndoto zako nzuri,lakini haiwezekani shekhe Seif kuamia chama cha makafir,labda Mbowe ama Slaa waje CUF cause Seif kashashinda wenye shida nyinyi wadanganyika
 
Hii trick ya Mbowe ya kuwachuuza wenzake kwa bei chee. Anazihitaji kura za Waislamu Zanzibar ndii maana anajidai anauabudu UKAWA.
Kwa janja yake atashawishi makamu ahamie CHADEMA na ikijitokeza tu hivyo na likatiba letu lilivyo la hovyo atatumia ubabe kumfanya asubmit kwake na sio kwa chama alichotokea. Hapo ndio itakuwa mwisho wa UKAWA.
 
Kwamjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977 pamoja naarekebisho yake, ni kuwa vyama haviruhusiwi kuungana bali ushirikiano tu.

Kwamjibu wa Sheria ambayo hairuhusu vyama kuungana ndio hiyo hiyo itakayozuia wagombea Urais na Makamu kutoka vyama tofauti.
Kwakuwa katiba yetu si kama ya Kenya au Nigeria kwenye political alliances

Chama kinachotoa mgombea Urais kinawezaje kupata Mgombea mwenza kutoka chama kingine bila kupoteza uanachama wake na kuungana na mgombea Urais?

Hii inamaana ikiwa mgombea urais atatoka Chadema italazimika mgombea mwenza wakutoka CUF au NCCR au NLR aukane uanachama wake na kujiunga na chadema!


Ama Dr Slaa, Mbowe nk, mmoja aende CUF, au Lipumba, Seif nk mmoja aende Chadema, au Dr Kahangwa, Mbatia au Kafulila mmoja aukane uanachama wake na kujiunga na chama kilichotoa mgombea urais.

Lakini jambo mhimu ni je, Katiba za vyama hivi zinaruhusu mtu akijiunga na chama anaweza kugombea uongozi au kuna mda maalumu wa kukaa ndipo agombee?

Naiona nchi mpya ikizaliwa yenye maziwa na asali chini ya UKAWA.


Maziwa na asali utayatafuta mwenyewe wala si wanasiasa fanya kazi jitume unatoboa, mfano mimi mwenyewe niko mbioni kuto.....!
 
Je,CHADEMA mpo tayari kutoa kura zenu endapo wagombea wote wawili watatokea CUF?Yaani mgombea urais awe Professor Lipumba na mgombea mwenza wake awe Mnyaa? Ni vigumu pia kuwaingia akilini Wana CUF kuwapigia kura wagombea wote wawili kutokea CHADEMA yaani Dr Slaa ktk urais na mwenza wake toka visiwani.In this case hakutakuwa tena na maana ya kuunda UKAWA,itakuwa na sawa na kupotezeana muda.


Myaa jembe Lipumba oke, sisi chadema tutapinga kula asilimia 100%
 
Kwamjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977 pamoja naarekebisho yake, ni kuwa vyama haviruhusiwi kuungana bali ushirikiano tu.

Kwamjibu wa Sheria ambayo hairuhusu vyama kuungana ndio hiyo hiyo itakayozuia wagombea Urais na Makamu kutoka vyama tofauti.
Kwakuwa katiba yetu si kama ya Kenya au Nigeria kwenye political alliances

Chama kinachotoa mgombea Urais kinawezaje kupata Mgombea mwenza kutoka chama kingine bila kupoteza uanachama wake na kuungana na mgombea Urais?

Hii inamaana ikiwa mgombea urais atatoka Chadema italazimika mgombea mwenza wakutoka CUF au NCCR au NLR aukane uanachama wake na kujiunga na chadema!


Ama Dr Slaa, Mbowe nk, mmoja aende CUF, au Lipumba, Seif nk mmoja aende Chadema, au Dr Kahangwa, Mbatia au Kafulila mmoja aukane uanachama wake na kujiunga na chama kilichotoa mgombea urais.

Lakini jambo mhimu ni je, Katiba za vyama hivi zinaruhusu mtu akijiunga na chama anaweza kugombea uongozi au kuna mda maalumu wa kukaa ndipo agombee?

Naiona nchi mpya ikizaliwa yenye maziwa na asali chini ya UKAWA.

ongea kiswahili bhana,kwa mjibu ndio nini?
 
Dawa ni rahisi sana, na nzuri mno, na hata Mie nitajiunga nanyi, mkifanya ifuatvyo::::

Kama luna nia ya ukweli , basi vyama vyote vilivyo ungana na kuunda Ukawa , wote wavunje vyama vyao na waanziche chama kimoja, hicho chama kitakuwa na nguvu ya ajabu, na hapatakuwa na matatizo ya Chadema kinawadhulumu CUF au Nccr nk.

One party fully United , can u do that???
 
ndugu Yericko Nyerere hakuna mahali UKAWA wamekubaliana kuwa mgombea urais akitoka cuf, mgombea mwenza atoke nccr. ninachojua ni kwamba mgombea urais na mgombea mwenza wake lazima watoke chama kimoja. ukawa sio mbumbumbu kihivyo hadi washindwe kufahamu hayo matakwa ya kisheria.

Hapo ndipo balaa na waziri mkuu atoke wapi
 
Last edited by a moderator:
Vyovyote itavyokuwa ikiwa CDM hawatapewa nafasi ya kugombea urais 100% ndio mwisho wa ukawa, kwa sababu wanajulikana wamejiweka hapo ukawa kwa kutafuta hayo tu,
 
Wataalamu wa Sheria hasa kuhusu Katiba jamani leteni maujuzi yenu.
Mkuu Yericko Nyerere umeleta mjadala huu muda muafaka!


MAKAMU WA RAIS

47.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.


(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu wa Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na watapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Rais akichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa.


(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

(4) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-

(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa sheria ya Uraia;
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;

(c) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi;

(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

(5) Chama chochote hakitazuiwa kumpendekeza mtu yeyote kuwa mgombea kiti cha Makamu wa Rais kwa sababu tu kwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais wa Zanzibar au kiti cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

(6) Makamu wa Rais hatakuwa kwa wakati huo huo Mbunge,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, wala Rais wa Zanzibar.
(7) Endapo mtu ambaye ni Waziri Mkuu, au Rais wa Zanzibar anateuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais ataacha kiti cha Waziri Mkuu, au cha Rais wa Zanzibar, kadri itakavyokuwa.
(8) Makamu wa Rais atatekeleza madaraka yake chini ya uongozi na usimamizi wa Rais, na ataongoza na kuwajibika kwa Rais kuhusu mambo au shughuli zozote atakazokabidhiwa na Rais.


CC Tumaini Makene Kurugenzi ya Habari
 
Last edited by a moderator:
Siyo lazima wagombea wa nafasi za urais na umakamo rais wawe ni makada au viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA.Wanaweza kuwashawishi watu ambao siyo wanachama wa hivyo vyama na ambao wana mitazamo na fikra huru kujiunga na chama kimoja wapo kisha wakateuliwa kuigombea nafasi hizo chini ya mwamvuli wa UKAWA.Lengo la kufanya uamuzi huo ni kuhakikisha wanakubalika kiurahisi na vyama vyote vinavyounda UKAWA;na pia kuendana na matakwa ya sheria na kanuni za uchaguzi.Ila wakithubutu kuteua wagombea wa nafasi za urais na umakamo kutoka miongoni mwa makada na/au viongozi wa wa vyama viundavyo UKAWA,uwezekano wa wagombea hao kuungwa mkono na wafuasi wa vyama hivyo utakuwa mdogo sana.
Tunajua unakoelekea, huyo sisi hatumhitaji abaki hukohuko CCM aliko.
 
Mkuu Yeriko, huwa ninakupinga kwenye yale mambo yako ya ujinga ujinga ila ukileta jambo la maana nakuunga mkono!.

Tangu ile 2010 Dr. Slaa aliposusia matokeo ya kura za urais, nikasema mtu huyo huyo ameona the playing fiels is not level, akaridhia na kusaini rules of the game na kupeleka timu uwanjani, baada ya kipigo, ndipo anakuja kulia lia kuwa the gane was not fair play and the plying ground was not level!.

Sheria zetu za uchaguzi ni kinyume cha haki za binaadamu zilizoaina kwenye katiba kwa kuwesabihinisha wagombea na vyama vya siasa!.

Niliilaani Chadema kuikumbatia sheria hii, ya kumuondoa mtumishi wa watu kwa kumfanya lazima adhaminiwe na Chama, that was a bad law!. Sasa kabla UKAWA haijakubali kuingia kwenye uchaguzi, kwanza ipiganie hizi draconian laws lazima kwanza zibadilishwe kuruhusu miungano ya vyama na hata serikali ya mseto!.

Vinginevyo UKAWA utabaki ni "a marriage of convenience" ya katiba tuu, katiba ikiishapita, its over!.

Pasco

Kuna njia tatu za kuvuka kizuizi hiki,

Ama Ukawa waingie "makubaliono memgine ya kimaandishi" sio gentleman agreement ya mkwere na laigwana, kwama chama kinachotoa toa rais, makamu mwenza atatoka chama kingine lakini atalazimika kuhama chama kwa mda tu, wanaweza kuweka miezi sita au kumi na miwili, hii itetegemea matokeo ya uchaguzi.

Ama wakubaliane kuwa wagombea urais na makamu wake watoke chama kimoja lakini kwa makubaliano maalumu kuwa ikiwa watashinda, basi ndani ya miezi mitatu tangu uchaguzi, katiba ifanyiwe marekebisho na makamu wa rais ateuliwe toka chama kingine,

Na mwisho ama kuanzia sasa upinzani uanze harakati za kudai marekebisho ya sheria na katiba hii juu ya kadhia hii.

Ifahamike kuwa kadhia hii haiishie kwe UKAWA tu, hii inawabana vyama vyote hasa ikitokea uchaguzi ujao ikalazimu kuundwa serikali ya mseto, katiba ya nchi hairuhisu uundwa wa serikali ya mseto bali inakazia kuwa chama kilichoshinda ndicho kinachounda serikali.
 
Ukawa bado kuchukua nchi labda 2020 kwa sasa chama kimoja kijitoe akili tu kikubali kuachia nafasi ya urais kwa sharti mwaka 2020 kiachiwe chenyewe na vile vile mwaka huu kiwe na wabubge wengi.

Hivi ccm mnafikiri ukawa wana uchu wa uraisi kama mlivyo. Lengo la ukawa ni kuing'oa ccm madarakani sio kwenye uraisi tu. Sioni shida raisi na makamu wakatoka chama hiki halafu waziri mkuu akatoka chama kingine na mchakato mzima wa uundaji wa serikali ukashikiliwa na ukawa ili kuleta maendeleo ya kweli nchini. Pia ili kupunguza zile 'ndioooo' za bungeni ukawa iwe na wawakilishi wengi.
 
Mahali pa kuanzia ni mgombea mwenza ambaye baadaye atakuwa Makamu wa Rais. Huyu kwa busara itabidi atoke Zanzibar kwani wagombea urais kutoka bara ndio wanaong'aa kwa sasa. Kwa hiyo swali la kujiuliza, chama gani kitatoa mgombea mwenza mzuri kutoka Zanzibar? Kitakachotoa mgombea mwenza, hakitatoa mgombea urais. Ni rahisi kumpata mgombea mwenza kutoka Zanzibar katika CUF kuliko katika CHADEMA

Kwani pia hujafikiria kwamba chama kimoja ndani ya ukawa kinaweza kikasimamisha pairs moja tanganyika na nyingine zanzibar?
 
Back
Top Bottom