Am soooo tired of being lonely

Wadau wa jukwaa tukufu la MMU, upweke ni kitu kibaya sana wapendwa! Pamoja na uzuri niliobarikiwa na Mungu lkn sijabahatika kupata wa kuniondolea upweke,natamani nipate mtu anipende nami nimpende,aniambie i miss u,i love u,nakuhitaji,anipe maneno matamu ya mahaba,sijawahi kupata,niliyewahi kuwa nae ilikuwa sawa na sina mpenzi!simu mpaka nipige mimi,msg niandike mimi vinginevyo atanyamaza hata wiki!am so desparate nahitaji counselling au msaada niondokane na hii hali tafadhali.

I love you Kibali.
I miss you like crazy!
Nikinywa maji kwenye glasi nakuona.
 
Pole sana! wapo watu wenye mapenzi ya ajabu, hukutafuta wakati wa kutaka kukupeleka kitandani tu, baada ya hapo hakukumbuki mpaka shida ije tena. Ila ka wewe ni Me mie nipo niko lonely pia na huwa napenda mapenzi kama yako ya kujali. Waweza nipm.
we si mwanamke? na yeye ni mwanamke pia? au ndio mambo ya .... ?
 
Pole sana! wapo watu wenye mapenzi ya ajabu, hukutafuta wakati wa kutaka kukupeleka kitandani tu, baada ya hapo hakukumbuki mpaka shida ije tena. Ila ka wewe ni Me mie nipo niko lonely pia na huwa napenda mapenzi kama yako ya kujali. Waweza nipm.

asante sana Remmy,pole pia!kweli ulichoongea ndicho,natamani nimpate nani tupeane mapenzi ya kweli,mi ni ke mwaya
 
Mapenzi ni hatari, hata ungekuwa mtalaam wa kuruka vihunzi lazima upite kwenye tanuru ili uive. Hiyo ni changa moto yako my dear. Kaa tulia wa kukuoa atakuja hawa wengine watakuvua nguo na kukuacha unalalama una mikosi. Siamini kama kuna mkosi!
 
nije wapi?
labda uje wewe...
wenzio wadada wengi wanatutokea style hiyo

namaanisha uje tena na ushauri,kwa hiyo na mimi natakiwa nianze kutokea wanaume?Boss hivi huoni kuwa ni ngumu kwa mwanamke jamani?nitafurahi mimi nikitokewa
 
Mapenzi ni hatari, hata ungekuwa mtalaam wa kuruka vihunzi lazima upite kwenye tanuru ili uive. Hiyo ni changa moto yako my dear. Kaa tulia wa kukuoa atakuja hawa wengine watakuvua nguo na kukuacha unalalama una mikosi. Siamini kama kuna mkosi!

asante caroline,kutulia nimetulia ila mawazo hayakosi kuniandama na upweke sana!rafiki zangu wote wana watu wao na familia,najiuliza kwanini mimi?!mbaya zaidi nina muda sijatongozwa!
 
Wadau wa jukwaa tukufu la MMU, upweke ni kitu kibaya sana wapendwa! Pamoja na uzuri niliobarikiwa na Mungu lkn sijabahatika kupata wa kuniondolea upweke,natamani nipate mtu anipende nami nimpende,aniambie i miss u,i love u,nakuhitaji,anipe maneno matamu ya mahaba,sijawahi kupata,niliyewahi kuwa nae ilikuwa sawa na sina mpenzi!simu mpaka nipige mimi,msg niandike mimi vinginevyo atanyamaza hata wiki!am so desparate nahitaji counselling au msaada niondokane na hii hali tafadhali.

oooooh,namim nina tatzo kama lako hata nikitoka job soon hata wa kuniambia pole kwa majukum,,,,au hata wa kunichagulia shati la kuvaa asb
 
Nahisi Remmy alihisi ya kuwa kibali ni mwanaume na ndo mana akatoa lake la moyoni sio ushoga
OOOh, nimekuelewa. Sio kwamba naona sio sawa wanawake kua pamoja ila nilitaka kushangaa wawe wamefika uhuru wa kiasi cha kutongozana live JF. Kwa kweli TZ hatujawa tayari kupokea uhusiano wa namna hii.
Ila I hope atasoma ushauri tunampa mwenzie nae afatilie.
 
asante caroline,kutulia nimetulia ila mawazo hayakosi kuniandama na upweke sana!rafiki zangu wote wana watu wao na familia,najiuliza kwanini mimi?!mbaya zaidi nina muda sijatongozwa!
Labda nikuulize ndugu yangu: una miaka ngapi hivi? kama haupo comfortable sema tu kati ya .... na ..... ili nione kama kweli umri wako unaweza kua ndio shida alafu nikupe ushauri muafaka
 
asante mpendwa nimekuelewa,sasa je kwanini sitongozwi kabisa?!wanaume wanapenda nini ambacho labda mimi nakikosa?inanichanganya sana!

hilo lisikupe shida jijenge wewe kwanza .hebu jaribu kuangalia pia the way unavyocomunicate na wa2 inaweza ikawa tatzo
 
asante caroline,kutulia nimetulia ila mawazo hayakosi kuniandama na upweke sana!rafiki zangu wote wana watu wao na familia,najiuliza kwanini mimi?!mbaya zaidi nina muda sijatongozwa!

huyo wa kwanza ulimtongoza wewe???
 
Boss mbona umekamia sana kwenye uzuri,kiukweli niko kiwango huwa naambiwa na me/ke,sasa unanishaurije Boss wangu?
hapo ndipo patakapokuharibia na usifurahie mahusiano hata mara moja,jiulize kwanini watu wanaamua kumpenda mtu kipofu,kiwete n.k kwahiyo huo uzuri ambao unadhani utapendwa kwa ajili yake sio kweli kwani wengi watakutamani watakuvua nguo na kukuacha kwa kuendelea kujiamini eti we mzuri na muda unazidi kwenda na utakapofikisha miaka 30+ kama bado utaanza kuwatongoza na kumbe uli*******ni wako ulikufanya ujione ni mzuri huenda ndo maana huyo jamaa amekuchukulia poa,huo uzuri huwa haudumu ila moyo na tabia nzuri,
TAFAKARI CHUKUA HATUA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
oooooh,namim nina tatzo kama lako hata nikitoka job soon hata wa kuniambia pole kwa majukum,,,,au hata wa kunichagulia shati la kuvaa asb

pole Bajabiri kweli ni kipindi kigumu sana
 
Labda nikuulize ndugu yangu: una miaka ngapi hivi? kama haupo comfortable sema tu kati ya .... na ..... ili nione kama kweli umri wako unaweza kua ndio shida alafu nikupe ushauri muafaka

RR nina kati ya 28 mpaka 32 asante kwa wema wako
 
hilo lisikupe shida jijenge wewe kwanza .hebu jaribu kuangalia pia the way unavyocomunicate na wa2 inaweza ikawa tatzo

inawezekana pia,kuwa wakati nahisi kama nakuwa sana siriaz sijui nifanyeje jamani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom