Habari zenu wanajamvi!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mimi ni mwanamke wa miaka 26 sasa...natafuta mwenye sofa zifuatazo.
.Mcha Mungu, yaani mwenye hofu ya Mungu, awe mkristo tu.( esp SDA)..sio lazima awe dini hiyo ila mwenye dini hiyo atapewa kipaumbele zaidi.
.Awe mrefu kiasi...sio sana. Ila asiwe mfupi Sana.
.Awe na umri wa miaka kuanzia 27 - 29.
.Awe anafanya kazi serikalini au ktk kampuni yoyote hapa Dar es salaam..( mi naishi Dar kwa sasa..that's why nasema awe mkazi wa hapa Dar).Naomba nisisitize hapa, awe anafanya kazi. Kama huna kazi...am sorry.
.Elimu awe degree, masters na kuendelea.
.Awe mkweli, muaminifu, mkarimu, mpenda watu , asie na majivuno, dharau,kiburi, mcheshi na mwenye heshima.
.Akiwa msukuma au mnyamwezi atapewa kipaumbele zaidi. Wakurya, wahaya...HAPANA.
.Sifa zingine tutaendelea zaidi kuelezana!
Sifa zangu;
.Heshima, mpole, mcheshi,mkweli, muaminifu muungwana, mnyenyekevu, mpenda watu, na mcha Mungu.
.Mnene kiasi,mweupe.
.Elimu yangu degree+ post
.Umri miaka 26
Naomba msamaha kwa wale watakaokwazika kwa post yangu...maana binadamu tunatofautiana, hatuko sawa kiuelewa. Kuandika vipaumbele vya dini na makabila hakumaanishi mimi ni mbaguzi....ila nimeamua kua mkweli na honest kuliko kujivika uongo usiokua na sababu. Hivyo mtanisamehe bure.
Na ukiona post haikufai...pita kimya kimya...ni kwa walio serious tu. Sipendi matusi wala kejeli. By the way hata ukitukana na kukejeli..Nishakusamehe tayari, maana mi mwenyewe nimeshasamehewa mengi tu.
Please kwa mwenye sifa hizo naomba ani PM.
Natanguliza Shukrani.
Jumamosi njema.