Alwayz inanikera sana polisi kutamka haya!!

ANDREWZ

Member
Oct 17, 2012
66
70
Ni sababu zipi za msingi ambazo huperekea Polisi mara wawakamatapo wauza madawa ya kulevya,nyara za serikali,thamani ya vitu hivi hutangazwa,hasa madawa ya kulevya(JANGA) Swali
Je,si kweli kwamba thamani ya vitu hivi kutangazwa huvutia watu kujihusisha?
Mawazo yako tafadhari
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,678
2,000
Nilianzisha uzi kuhoji ni wapi yalipo madawa ya kulevya yanayokamatwa, hadi leo sijapata jibu la maana. au ulishwahi kuona yameteketezwa? mbona bangi wanaichoma kisha wanaita na mavideo camera kibao kila mahali inakua ni nyuizi
 

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,269
2,000
inabidi tujiulize, yanathamani? au hayana thamani, jibu ni kwamba madawa ya kulevya na nyara za serikali vyote ni bidhaa haramu zinapomilikiwa kinyume cha sheria, lkn ili serikali iweze kuandaa mashtaka kwa watuhumiwa inalazimu ijulikane thamani halisi ya madawa hayo, vilevile tutake tusitake mtaani jamii inafahamu bei ya bidhaa hizo, hivyo serikali huchukua bei ya mtaani mara mzigo na kutoa thamani nzima kukamilisha malengo ya kisheria.
 

ANDREWZ

Member
Oct 17, 2012
66
70
bubu hiyo like wamaanisha kuwaunga mkono polisi kutangaza ama?
niambie kama una mtaji
 

ANDREWZ

Member
Oct 17, 2012
66
70
Polisi inatumia bei ya mtaani,
kwa mantiki hiyo wauzaji wanafahamika,wapi wanapojumua,soko na wateja wao,swali kwanini serikali kama ipo serious na jambo hilo isiende huko kuliko routecourse?
 

katalina

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
262
0
Sasa hapa kinachokukera nini. Utamshitakije mtu bila ya kujua thamani ya huo ushahidi. Nakushauri upendekeze ulitaka wawe wanasemaje ili wanapokuwa wanatamka hayo maneno uone burudani 'rohoni' mwako.
 

ANDREWZ

Member
Oct 17, 2012
66
70
Sasa hapa kinachokukera nini. Utamshitakije mtu bila ya kujua thamani ya huo ushahidi. Nakushauri upendekeze ulitaka wawe wanasemaje ili wanapokuwa wanatamka hayo maneno uone burudani 'rohoni' mwako.

Issue hapa si mi kufurahi moyoni issue niliyoirise ni kutajwa kwa bei na kwamba kwa kufanya hivyo kunawavutia watu na hasa vijana kushawishika kujiingiza katika biashara hiyo haramu,so mawazo yangu mimi ni omission ya price na kuwekwa maneno yenye kuogofya kidogo,mfano maneno yenye kutoa athari ya madawa hayo eg,madawa yenye kuaribu akili
 

okaoni

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
1,396
2,000
Issue hapa si mi kufurahi moyoni issue niliyoirise ni kutajwa kwa bei na kwamba kwa kufanya hivyo kunawavutia watu na hasa vijana kushawishika kujiingiza katika biashara hiyo haramu,so mawazo yangu mimi ni omission ya price na kuwekwa maneno yenye kuogofya kidogo,mfano maneno yenye kutoa athari ya madawa hayo eg,madawa yenye kuaribu akili
andrew lengo la polisi si kuvutia watu kwa kutaja dhamani kubwa ya madawa hayo haramu.ni matakwa ya kisheria hasa kwenye sheria ya madawa ya kulevya kwamba mtu atapata adhabu kutokana na kiwango cha madawa alichokutwa nacho na adthari za wingi wa madawa hayo kama yangeinia kwenye soko haramu(black market) ni kwa minajili hiyo basisheria inabainisha wazi kuwa kwa madawa yaliyokamatwa yenye thamani ya ths milioni kumi basi hata chombo kilichotumika kusafirisha chaweza kutaifishwa. kwa maono yangu naona wako sawa kutaja thamani ili jamii ijue adhabu watakayoipata mwisho wasiku na kutisha wengine wasitende vitendo vya namna hiyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom