Alphonce Mawazo baki Busanda

Alphonce Mawazo baki Busanda

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Siyo vizuri kabisa yaani. Mgombea wa Ubunge wa CHADEMA/UKAWA Jimbo la Busanda, Alphonce Mawazo anachachafya CCM mkoani Geita na hata kumshtua/kumtisha Dr. Magufuli anayetokea mkoa huo. Taarifa nilizonazo ni kuwa Mawazo anatamba mkoa mzima wa Geita. Anasingizia kuwa kwakuwa yeye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Geita anapaswa kutamba mkoa mzima ili kuzoa majimbo yote ya Geita.

Si vyema kabisa. Dr. Magufuli anapata wasiwasi wa kasi na kukosa utulivu. Anashambuliwa nyumbani kwake. Ashindwe mkoani mwake kweli!? Anabanwa mbavu hata jimboni mwake na huyu Mawazo wa CHADEMA. Mawazo, kumbuka ulikuwa CCM. CCM ilikulea na hata kukupa Udiwani kule Arusha. Mbona hukumbuki kulipa fadhila? Ndiyo shukrani ya punda hiyo? Wewe ungetulia tu jimboni mwako Busanda na kujipigia kampeni. Ingetosha. Si kutetemesha na kutisha. Majimbo mengine waachie wenyewe.

'Kamanda' Mawazo, punguza sifa. Au nije? Tupe nafasi ya kula nanasi bwana!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Attachments

  • Mawazo na lema_thumb[2].jpg
    Mawazo na lema_thumb[2].jpg
    33.1 KB · Views: 1,928

VUTA-NKUVUTE kama Magufuli ana wasiwasi na kamanda Mawazo basi ungemshauri aongeze push ups na sasa aruke na kichurachura kama yule wa Tunduru
 
Mawazo ni sawa na wabunge wote pamoja na NEC ya CCM akiwemo JK na Salma Jabir ndipo wanaweza kufikia robo ya ubongo wake. Kwa kifupi anaushawishi kiasi kwamba akihutubia dakika 30 unamsikiliza unaweza kujitoa mhanga kama ikibidi ufanye hivyo. Nilimsikiliza Kakola nilitamani nikauchome moto mgondi kwa hasira.
 
Siyo vizuri kabisa yaani. Mgombea wa Ubunge wa CHADEMA/UKAWA Jimbo la Busanda, Alphonce Mawazo anachachafya CCM mkoani Geita na hata kumshtua/kumtisha Dr. Magufuli anayetokea mkoa huo. Taarifa nilizonazo ni kuwa Mawazo anatamba mkoa mzima wa Geita. Anasingizia kuwa kwakuwa yeye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Geita anapaswa kutamba mkoa mzima ili kuzoa majimbo yote ya Geita.

Si vyema kabisa. Dr. Magufuli anapata wasiwasi wa kasi na kukosa utulivu. Anashambuliwa nyumbani kwake. Ashindwe mkoani mwake kweli!? Anabanwa mbavu hata jimboni mwake na huyu Mawazo wa CHADEMA. Mawazo, kumbuka ulikuwa CCM. CCM ilikulea na hata kukupa Udiwani kule Arusha. Mbona hukumbuki kulipa fadhila? Ndiyo shukrani ya punda hiyo? Wewe ungetulia tu jimboni mwako Busanda na kujipigia kampeni. Ingetosha. Si kutetemesha na kutisha. Majimbo mengine waachie wenyewe.

'Kamanda' Mawazo, punguza sifa. Au nije? Tupe nafasi ya kula nanasi bwana!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Vuta nkuvute hata sikuelewi hutaki upinzani wa kweli ???! Unataka jimbo liende wazi kisa ni mkoa anakotoka Magufuli ???!.

Aina ya watu kama wewe ndio mnaofanya Ccm ionekane kama ni serikali. UNAHUZUNISHA
 
VUTA-NKUVUTE nyinyi si chama kubwa?

Chama kubwa kama Real Madrid ila mfungaji wao Ronaldo (Magufuli) mechi imemchanganya sasa badala ya kufunga kwa adui anaelekeza mashambulizi kwenye timu yake kwa kuwakata chenga mabeki wake (Kinana, Nape, Pinda) na kutaka kushuti kwa golikipa wao JK. Timu imetaharuki wanajiuliza huyu jamaa kavuta msuba au betri yake (pace maker) imeisha chaji?
 
Last edited by a moderator:
Pole Vuta ni kuvute, jana Sumaye kasema kama hukuvuka na EL pole maana mto una mamba na boti ya EL imeshasepa
 
Mawazo ni sawa na wabunge wote pamoja na NEC ya CCM akiwemo JK na Salma Jabir ndipo wanaweza kufikia robo ya ubongo wake. Kwa kifupi anaushawishi kiasi kwamba akihutubia dakika 30 unamsikiliza unaweza kujitoa mhanga kama ikibidi ufanye hivyo. Nilimsikiliza Kakola nilitamani nikauchome moto mgondi kwa hasira.
Kujikita vijijini kwa muda mrefu kwa alphonce mawazo kumeleta ukombozi geita , ushawishi wake ni wa kiwango cha mitume .
 
Amini usiamini CHADEMA bado hawajamtumia inavyotakiwa kuzipata kura za mgombea uraisi. Huyu jamaa hakuna anayeweza kumfikia hata Mbowe hawezi kumfikia. Naomba Lowassa akija Mwanza wampe mic waone.
 
Umesikika kamanda .
 
Siyo vizuri kabisa yaani. Mgombea wa Ubunge wa CHADEMA/UKAWA Jimbo la Busanda, Alphonce Mawazo anachachafya CCM mkoani Geita na hata kumshtua/kumtisha Dr. Magufuli anayetokea mkoa huo. Taarifa nilizonazo ni kuwa Mawazo anatamba mkoa mzima wa Geita. Anasingizia kuwa kwakuwa yeye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Geita anapaswa kutamba mkoa mzima ili kuzoa majimbo yote ya Geita.

Si vyema kabisa. Dr. Magufuli anapata wasiwasi wa kasi na kukosa utulivu. Anashambuliwa nyumbani kwake. Ashindwe mkoani mwake kweli!? Anabanwa mbavu hata jimboni mwake na huyu Mawazo wa CHADEMA. Mawazo, kumbuka ulikuwa CCM. CCM ilikulea na hata kukupa Udiwani kule Arusha. Mbona hukumbuki kulipa fadhila? Ndiyo shukrani ya punda hiyo? Wewe ungetulia tu jimboni mwako Busanda na kujipigia kampeni. Ingetosha. Si kutetemesha na kutisha. Majimbo mengine waachie wenyewe.

'Kamanda' Mawazo, punguza sifa. Au nije? Tupe nafasi ya kula nanasi bwana!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Magufuli anatoka jimbo la chato,mkoa wa kagera,sio geita.
 
Back
Top Bottom