huko tangu mwalim anatawala hadi leo hawajapata faida,kwa hyo hatupat chochote
Umeua mkuu, nimecheka sana.
huko tangu mwalim anatawala hadi leo hawajapata faida,kwa hyo hatupat chochote
Red or pink diamond ndo the expensive germ on earth. Yaani carat moja ya hiyo ni USD 10,000,000 nilikua nasoma habari jana. Kwa hiyo hapo carat 23 kuna utajiri sio chini ya USD 30,000,000 au zaid maana ikiwa ipo kwenye carat 23 ina maana possibility ya kuuzwa bei juu ni kubwa.
Hahaha life la mererani utaliweza kaka? kule full shida aisee labda tuwe wanunuzi au unasemaje? Tafuta mtaji basiTwende mererani mkuu.
Red or pink diamond ndo the expensive germ on earth. Yaani carat moja ya hiyo ni USD 10,000,000 nilikua nasoma habari jana. Kwa hiyo hapo carat 23 kuna utajiri sio chini ya USD 30,000,000 au zaid maana ikiwa ipo kwenye carat 23 ina maana possibility ya kuuzwa bei juu ni kubwa.
Sisi tutapata ngapi!
Kwa hiyo bei ni bora likae pale BOT tu.. labda kama mleta taharifa kakosea
![]()
KAMPUNI ya madini ya Petra Diamonds imegundua aina adimu ya almasi ya rangi ya pinki yenye uzito wa karati 23.16 kutoka mgodi wake wa Williamson uliopo Mwadui, Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo ya madini, almasi hiyo ya pinki, moja ya madini ya rangi yanayosakwa zaidi duniani ni mfano wa ubora wa hali ya juu na ugunduzi mkubwa na muhimu zaidi kufanywa na Petra kutoka mgodi huo hadi sasa.
"Almasi za pinki hupatikana katika migodi michache duniani na uadimu wake huzifanya kuwa moja ya madini yenye rangi yanayotafutwa zaidi duniani,"taarifa ya kampuni hiyo ilisema.
Rangi ya pinki katika almasi inadhaniwa kuletwa kutokana na mabadiliko ya muundo wa molekuli, ambao unaaminika kusababishwa na aina fulani ya mtikisiko wa ardhi (seismic shock) unaotokea wakati wa kipindi cha uumbaji wa almasi.
Pande hilo la almasi litauzwa katika mnada huko Antwerp nchini Ubelgiji Desemba mwaka huu.
Jiwe hilo jipya linasemekana kuwa na ubora zaidi kuliko almasi pinki yenye ubora wa juu na uzito wa karati 16.4 iliyogunduliwa katika mgodi huo Septamba 2014, ambayo iliuzwa kwa dola milioni 2.2 sawa na Tsh bilioni 4.7.
Novemba 10 mwaka huu, mteja mmoja wa China, ambaye hakuweza kutambulika alinunua almasi ya pinki yenye umbo la mto na uzito wa karati 16.08 katika mnada huo kwa bei iliyovunja rekodi ya dunia. Aliinunua kwa Pauni milioni 19 za Uingereza sawa na Sh bilioni 61 za Tanzania kama zawadi kwa binti yake.
Katika miaka karibu 250 ya historia ya minada, ni almasi tatu tu safi za pinki zilizokuwa na uzito wa zaidi ya karati 10 zilizoonekana kwa mauzo, kwa mujibu wa taasisi ya Christie?s.
CHANZO:Mtanzania