Almasi adimu yagundulika Tanzania

Almasi adimu yagundulika Tanzania

Pistol

Senior Member
Joined
Oct 13, 2015
Posts
194
Reaction score
86
attachment.php

KAMPUNI ya madini ya Petra Diamonds imegundua aina adimu ya almasi ya rangi ya pinki yenye uzito wa karati 23.16 kutoka mgodi wake wa Williamson uliopo Mwadui, Shinyanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo ya madini, almasi hiyo ya pinki, moja ya madini ya rangi yanayosakwa zaidi duniani ni mfano wa ubora wa hali ya juu na ugunduzi mkubwa na muhimu zaidi kufanywa na Petra kutoka mgodi huo hadi sasa.

"Almasi za pinki hupatikana katika migodi michache duniani na uadimu wake huzifanya kuwa moja ya madini yenye rangi yanayotafutwa zaidi duniani,"taarifa ya kampuni hiyo ilisema.

Rangi ya pinki katika almasi inadhaniwa kuletwa kutokana na mabadiliko ya muundo wa molekuli, ambao unaaminika kusababishwa na aina fulani ya mtikisiko wa ardhi (seismic shock) unaotokea wakati wa kipindi cha uumbaji wa almasi.

Pande hilo la almasi litauzwa katika mnada huko Antwerp nchini Ubelgiji Desemba mwaka huu.

Jiwe hilo jipya linasemekana kuwa na ubora zaidi kuliko almasi pinki yenye ubora wa juu na uzito wa karati 16.4 iliyogunduliwa katika mgodi huo Septamba 2014, ambayo iliuzwa kwa dola milioni 2.2 sawa na Tsh bilioni 4.7.

Novemba 10 mwaka huu, mteja mmoja wa China, ambaye hakuweza kutambulika alinunua almasi ya pinki yenye umbo la mto na uzito wa karati 16.08 katika mnada huo kwa bei iliyovunja rekodi ya dunia. Aliinunua kwa Pauni milioni 19 za Uingereza sawa na Sh bilioni 61 za Tanzania kama zawadi kwa binti yake.

Katika miaka karibu 250 ya historia ya minada, ni almasi tatu tu safi za pinki zilizokuwa na uzito wa zaidi ya karati 10 zilizoonekana kwa mauzo, kwa mujibu wa taasisi ya Christie?s.

CHANZO:
Mtanzania
 
sasa hiyo bilioni 4 ,roughly si sawa na nyumba 70 za masamaki wa TRA kama alijenga kwa milioni 5o each
 
Petra wanatuibia. Magufuli kama inawezekana funga mgodi.
 
Hapo ndio tunadanganywa mwaka jana 2014 . ubora wa hiyo almasi walisema 21 trion . hii ya leo tunaambiwa ni bora kuliko ya mwaka jana et iwe na 4.bilion, what is four bilion? Hapo Arusha 4b ni hela ya kawaida mno kwenye Tanzanite sembuse almasi, hiyo ya pink..
 
Red or pink diamond ndo the expensive germ on earth. Yaani carat moja ya hiyo ni USD 10,000,000 nilikua nasoma habari jana. Kwa hiyo hapo carat 23 kuna utajiri sio chini ya USD 30,000,000 au zaid maana ikiwa ipo kwenye carat 23 ina maana possibility ya kuuzwa bei juu ni kubwa.
 
Hapo ndio tunadanganywa mwaka jana 2014 . ubora wa hiyo almasi walisema 21 trion . hii ya leo tunaambiwa ni bora kuliko ya mwaka jana et iwe na 4.bilion, what is four bilion? Hapo Arusha 4b ni hela ya kawaida mno kwenye Tanzanite sembuse almasi, hiyo ya pink..

Hiyo 4 Billion ni pesa mbuzi kwa wale mabroker pale Arusha.. Ni pesa ambayo watu wanaitengeneza kwa wiki kadhaa tu pale Mererani.. Yaani kitu adimu hivyo alafu kinauzwa bei ya kutupa hivyo??
 
Hiyo 4 Billion ni pesa mbuzi kwa wale mabroker pale Arusha.. Ni pesa ambayo watu wanaitengeneza kwa wiki kadhaa tu pale Mererani.. Yaani kitu adimu hivyo alafu kinauzwa bei ya kutupa hivyo??

Si ndio maana tunaambiwa kuwa ni Malofa mkuu.
 
Hiyo 4 Billion ni pesa mbuzi kwa wale mabroker pale Arusha.. Ni pesa ambayo watu wanaitengeneza kwa wiki kadhaa tu pale Mererani.. Yaani kitu adimu hivyo alafu kinauzwa bei ya kutupa hivyo??

mim nilitegemea iwe 4b usd na sio tsh huu ni ujinga sana aisee
 
Back
Top Bottom