Ally Amani Karume anakaribisha machafuko Zanzibar?

Chimemena

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,376
452
Habari Wakuu!
Wakati tunaendelea kutofakari na kuchambua maamuzi ya kujiuzuri kwa Muhongo, kutangazwa na kuapishwa kwa Mawaziri leo naomba pia tujiulize na kuangalia siasa zinazofanywa huko Zanzibar na mtoto wa rais wa kwanza wa Zanzibar Balozi Ally Amani Karume kwa manufaa ya wazanzibari na watanzania kwa ujumla.

Huyu mwanasiasa sijui ndo kujipigia debe urais wa Tanzania ana wa Zanzibar kama ilivyonenwa hapo awali amekuwa akibeza na kukejeri muundo wa serikali ya Kitaifa ama Maridhiano uliofanyika kati ya CCM na CUF huko Zanzibar uliosimamiwa na kaka yake Rais mstaafu Amani Karume kwamb ni waj ajabu, haufai na hajawahi kuona mahala popote duniani na anashangaa kwa nini iwe Zanzibar yenye makamu rais wawili?

Bila kurejea nyuma tulikotoka kwa uhasama ulikuwepo kati ya cuf na ccm zanzibar mpaka kukatana mapanga, kuuwawa na kupoteza wengine lakini balozi Karume amekuwa akionyesha wazi kuwa na nia ya kuvunja maridhiano haya na kuwakehi viongozi waliopo madarakani, wako wapi watu wa kumkanya ama kumweleza mazuri ya muundo huu au hata kujaribu kumuuliza kaka yake kwa nini alifanya hivyo?

Je nia na dhamiri yake ni kutaka kuleta tena machafuko Zanzibar au anataka nini?
 
Tatizo la tanzania hatutaki kutumia sheria. Kila kitu kikiongozwa na sheria mambo kama hayo yasingekuwepo. Kila siku tunaishi kwa kamati na maridhiano. Sheria zimetungwa za nini saaa.
Kabla hujaanza kumfikiria yuko sahihi au laa, fikiria kwanza kwa nini hayo maridhiano yalitokea? Na kama ishu ilikuwa ni uchaguzi je ulikuwa wa wazi na huru?
 
Habari Wakuu!
Wakati tunaendelea kutofakari na kuchambua maamuzi ya kujiuzuri kwa Muhongo, kutangazwa na kuapishwa kwa Mawaziri leo naomba pia tujiulize na kuangalia siasa zinazofanywa huko Zanzibar na mtoto wa rais wa kwanza wa Zanzibar Balozi Ally Amani Karume kwa manufaa ya wazanzibari na watanzania kwa ujumla.

Huyu mwanasiasa sijui ndo kujipigia debe urais wa Tanzania ana wa Zanzibar kama ilivyonenwa hapo awali amekuwa akibeza na kukejeri muundo wa serikali ya Kitaifa ama Maridhiano uliofanyika kati ya CCM na CUF huko Zanzibar uliosimamiwa na kaka yake Rais mstaafu Amani Karume kwamb ni waj ajabu, haufai na hajawahi kuona mahala popote duniani na anashangaa kwa nini iwe Zanzibar yenye makamu rais wawili?

Bila kurejea nyuma tulikotoka kwa uhasama ulikuwepo kati ya cuf na ccm zanzibar mpaka kukatana mapanga, kuuwawa na kupoteza wengine lakini balozi Karume amekuwa akionyesha wazi kuwa na nia ya kuvunja maridhiano haya na kuwakehi viongozi waliopo madarakani, wako wapi watu wa kumkanya ama kumweleza mazuri ya muundo huu au hata kujaribu kumuuliza kaka yake kwa nini alifanya hivyo?

Je nia na dhamiri yake ni kutaka kuleta tena machafuko Zanzibar au anataka nini?

nilisikiliza kipande kidogo cha hotuba yake kinatia kichefuchefu. kwa maneno yale naamini hawatakii mema wazanzibar
 
Huyu jamaa huwa kila analolifanya kaka yake Amani Karume yeye huwa lazima alipinge,na kwa sasa hana kazi ya kufanya muda wake wa ubalozi umekwisha,anajidai eti anashangaa na hajaona duniani muundo huu wa serikali anasahau hapo Congo palikua na makamu raisi wanne.
 
Asibabaishe watu bado kesi ya kuua haijafa asione kimya akafikiri watu wamesahau .
Ndugu wa marehemu wapo na mashahidi wapo.
Ni ujinga tu kwa serikali hii kumpa ubalozi huko nyuma wakati anahusika kuua huko znz.
Yaani ccm wanafikiri watu wajinga ? Kumbomoa huyu ni kwa cuf kumpa ukweli kwenye mkutano kwamba aliua kwa makusudi mtoto wa kike baada ya kukataliwa.
Ali Nabwa aliandika haya . Hivo msibabaishwe na watu mikono yao ina damu za raia.
 
Mkuu hyo sie wa nchi jiran hatuijui hebu tupe kidogo ilikuaje
 
Wako wapi wanasiasa wakongwe kama Mzee Moyo kumshauri na kumuasa huyo mtangaza nia?
Namshangaa sana hata Kinana, Shein, Nape na kakaye kuendelea kumchekea huyu mkaribisha machafuko!
 
Back
Top Bottom