Allowances: Ex-German president warns govt

Posho hizi ndizo hasa zinazo-fuel inflation kwa kiwango kikubwa;
  • Sitting allowance (Posho ya kukaa) - Viwango vyake havijulikani, kila anayelipa huamua alipe shilingi ngapi na kwa kikao kipi! Kikao hiki unaweza lipwa elfu arobaini, kingine ukalipwa laki nne.
  • Posho ya vikao haikatiwi kodi na mara nyingine mlipwaji hatakiwi kuweka sahihi popote. Unapewa bahasha, unaondoka.
  • Posho ya vikao hakatwi kodi na haiwekwi kwenye rekodi yoyote kuonesha kuwa mlipwaji kalipwa. Wakati mwingi ni vikaratasi tu vinavyoorodheshwa majina ya walipwaji na kiwango walicholipwa
  • Kuna watu wengi wanalipwa posho hizo bila kuhudhuria vikao husika, yaani si lazima uwepo kwenye kikao; unalipwa tu kutegemeana na anayelipa ameamua vipi!
Posho hii ya vikao ni jambo la aibu. Posho zingine kama posho ya kujikimu mtu anaposafiri ni halali ilipwe, lakini ni vizuri iorodheshwe kwenye payslip kuonesha kuwa mlipwaji amepata hayo malipo. Kwenye makampuni binafsi, TRA wanawalazimisha watu kuzi-retire posho hizo. Yaani kurejesha risit zinazoonesha gharama halisi zilizotumika, usipofanya hivyo; posho hiyo hujumlishwa na mshahara na kukatiwa kodi kama sehemu ya mshara. Ni aibu kuwa serikalini hawafanyi hivyo na TRA hawajihangaishi nalo. Yaani serikali yenyewe ni mkwepaji wa kulipa kodi!!!!

Haya mambo yanatia kichefu chefu. Inaelekea Tanzania tunaishi katika sayari nyingine. Kwa nini haya maposho yanaongeza mfumko wa bei? Ni kwa sababu haya maposho huongeza wingi wa fedha mtaani. Posho hizo hulipwa kwa kazi ambazo wanaozifanya wameshalipwa mshahara tayari. Wengine wameshalipwa na posho zao nyingine ambazo tunaamini ndo malipo stahili yanayothamanishwa na kazi walizofanya. Posho kama posho ya vikao ni malipo ya bure ambayo hata wanaolipwa hawazionei uchungu hizo fedha; huzitumia ovyo ovyo mara nyingi kununua vitu bila hata kuuliza bei. Wanaolipwa maposho haya wakienda kununua kiwanja Mbezi, akiambiwa milioni ishirini, hutoa bila kuomba kupunguziwa bei. Hawa na mababa wa mfumko wa bei. Mfumko wa bei husababishwa na wingi wa fedha kwenye uchumi. Wingi wa fedha usiolingana na kiwango cha bidhaa na huduma zinazozalishwa na uchumi huo.

Malipo ya fedha yasiyotokana na utoaji wa huduma au bidhaa "tangible" ndo yanayosababisha wingi wa fedha kwenye mzunguko. Mojawapo ya Mrija mkubwa wa kupitishia fedha zinazoingia kwenye uchumi bila kufuata utaratibu halali ni huu wa kulipana posho za vikao kwa viwango vinavyoamriwa "arbitrarily" na wakubwa. Hii ina madhara kwenye uchumi sawa na "money laundering".

Wanaotetea hizi posho wanatumia sababu za kijinga kabisa....... Etii wanaombwa kusaidia watu wengi na wapiga kura wao!! Kuna mbunge anaweza kuthibitisha hili?? Hizo fedha wanawagawia ndugu zao ambao wamewageuza miradi, au wapiga debe wao, halafu wanasingizia wapiga kura wao, ni utovu wa nidhamu na upuuzi mkubwa. Hata waziri mkuu kasema, eti hizi fedha wanazitumia kuwalipia wapiga kura wao. Yaani wabunge wanaweza wakatumia sababu hii ya kizembe namna hii kutetea malipo haram ya sitting allowance??

Haya tutaendelea kuyapinga kama zilivyopingwa takrima. Haya malipo ya sitting allowance ni sawa na money laundering! Yanawaangamiza watanzania wenye kipato kidogo kwa ku-fuel inflation na kufanya wale wanaotegemea mishahara halali washindwe kuishi. Hawa wanaoshindwa kupata malipo halali ya sitting allowance kwa sababu wao nafasi zao haziwawezeshi kukaa kwenye mavikao kila siku wafanyeje?

Huu ni wizi, ni utapeli wa viongozi. Ni institutionalized corruption ya hali ya juu kabisa!!
 
Allowances: Ex-German president warns govt

Wednesday, 15 June 2011 23:46


By Polycarp Machira
The Citizen Reporter

Dar es Salaam. The debate on allowances paid to civil servants took a new turn yesterday when former German president Horst Kohler warned the government that its image was at stake.Prof Kohler said in Dar es Salaam that donors were closely monitoring the debate, adding that it might end up tarnishing the government’s image before development partners if it was not handled properly.Responding to a question during a dialogue at Movenpick
Hotel, he said the debate did present a good picture of the country’s expenditure priorities.

Prof Kohler said it was not in order for a country like Tanzania, which received substantial assistance from donor countries, to set aside huge sums as allowances for government officials, who were also being paid salaries. Giving an example of his own country, he said: “In Germany, such officials have to foot their own
bills while attending official duties.” He added that payment of allowances was not a proper way of spending taxpayers’ money.

Prof Kohler said at the Maendeleo Dialogue, organised by Konrad Adenauer Stiftung (KAS) and the Tanzania Development Initiative Programme (Tadip), that Western countries were likely to react once they had all the facts on the allowances debate.

He spoke as debate on allowances paid to public officials raged. Opposition MP Zitto Kabwe last week said he would not accept allowances during Parliament’s ongoing Budget sitting in Dodoma. The Kigoma North MP said parliamentarians and government officials did not deserve to be paid allowances as they went about their official duties.

Prof Kohler urged the government to uphold transparency and accountability.Prof Kohler noted that Tanzania had made great strides in development, but added that a lot more needed to be done to promote the rule of law, saying this would enhance the public’s trust on the government.

The former Head of State, a well-known proponent of Western development assistance for African countries, said only the people, leaders and government can bring about real change in Tanzania.

Speaking on the theme of “Cooperation and Solidarity – Opportunities for International Social Market Economy”, he said there were variations among countries, making the dream of a global social market unlikely in the near future.

On the road to the new Constitution, Prof Kohler said it was necessary to bring in national
values in the envisaged law. He said the process was an opportunity for Tanzanians to discuss values to be incorporated in the Constitution, noting, for instance, that the German constitution opened up with the line “Dignity for human being is untouchable.”

While praising Tanzania for steps taken towards development, Prof Kohler said the country had numerous long-term development plans that should be implemented to accelerate growth.“It is not only important to discuss visions but you should also reflect on implementation. Let accountability prevail such that leaders are held accountable for promises they made,” he said.

Bank of Tanzania (BoT) governor Benno Ndulu said Tanzania had for a long time faced the challenge of balancing what the government and the private sector ought to do.

He said the government had the important role of complementing the positive impact of the private sector.
“The government should put in place infrastructure that supports private sector initiatives to boost growth as well as improve institutions that stand for property rights and resolve disputes,” Prof Ndulu said.

Another panelist, Dr Camilius Kassala from the Institute of Finance Management (IFM), said many African leaders would do only what is practical even if it was unethical.

He noted that a social market economy should be inclusive and provide for accountability.
Dr Kassala urged the government to facilitate the private sector’s participation in the market, adding that freedom of market must be matched with social justice.


Mr Polycarp Machira, A word "few" is missing Between to and Civil. See red.
 
mmh yaani mpaka tuambiwe na nchi nyingine ndio iingie akilini? inatia hasira, nchi iipe TZ msaada halafu wautumie kwa kulipana posho ambazo kwao hawapati, wakisikia na wengine huu mjadala tutaonja joto ya jiwe.
Huku kuhusudu mzungu kuwa ndiye anajua kila kitu sijui itaisha lini.
Hii ni hali ya juu kabisa ya kutojiamini.
Nasema kwa wengi walio watoto hawajui kwamba Mwalimu aliwatimua Wajerumani mwaka 1967 pamoja na kwamba ndio waliobuni National Housing Scheme.Mwalimu aliwatimua Wajerumani baada ya wao kutuwekea masharti ya kutuchagulia mambo ya kufanya.
Mimi sioni mantiki ya mtanzania kukubali kuwa mjerumani ndiye amwambie namna ya kuishi.Hayo ni mawazo ya kutawaliwa kifikra.
 
Anna Makinda haelewi yaani sijui kichwa chake kina nini huyu mama...ndo shida ya kukulia kwenye TANU unaanza kuwa mpika chai mpaka spika basi mawazo ni mgando kama ice cream za bahkresa
hahahahaha kumbe huyu bibi alikuwa mpika chai wa TANU,ndo mana akili yake imedumaa anapinga sana hoja ya posho......kuna mbunge wa cuf anasema vijana wakwao WANAPARA SAMAKI nini maanake?
 
Obama katuma mpishi wake aje atutungue akili namna ya kukoroga msosi chakula kiive vizuri, sisi tunakuja na hii ya kuikashifu NGO's eti wanapeleka habari mbaya kwa wahisani, tunaendesha serikali endelevu au mipasho?
Waziri mkuu wake anatetea posho kwa nguvu zote kama si mtoto wa mkulima, mpaka mishipa inamtoka usoni eti anataka posho kwa ajili ya kuwapa omba omba, au kiinimacho kuwapa wapiga kura kipindi cha kampeni?
 
William Malecela @ NY City aka kule Mount Vernon atamwambia nini Kohn na uzoefu wake wa kuijenga Ujerumani?
 
Obama katuma mpishi wake aje atutungue akili namna ya kukoroga msosi chakula kiive vizuri, sisi tunakuja na hii ya kuikashifu NGO's eti wanapeleka habari mbaya kwa wahisani, tunaendesha serikali endelevu au mipasho?
Waziri mkuu wake anatetea posho kwa nguvu zote kama si mtoto wa mkulima, mpaka mishipa inamtoka usoni eti anataka posho kwa ajili ya kuwapa omba omba, au kiinimacho kuwapa wapiga kura kipindi cha kampeni?
Wakati huo huo mwenye chadema akifikiria lupango tu ati anasahau visenti vyake na magorofa yake popote yalipo nchini.
Anaweza kuwa amiri jeshi mkuu huyu?
Aheri yule wa kupewa viposho vya wakulima
Na aheri kuandamana tu , hakuna majoto hapo!
Mie naandamana chumbani, nisijepigwa kirungu bure!
 
Akili zako zimevia kweli mwishimiwa. Yaani serikali inatembeza bakuli kuomba misaada ili kulipa sitting allowances. Huu ni uchafu, ujinga na ubazazi. Nadhani watu kama wewe mngekufa mkaisha, Tanzania would be a better place. Trust me.

Mkulu

Kwa hili nakubali kuwa Zitto na wengine wanaosusia/pinga posho ya vikao(sitting allowance ,wanatafuta umaarufu/sifa au kujijenga kisiasa.Kama wao ni wazalendo wa kweli wangepinga posho ya Ubunge(5 ml) kwa mwezi.

Mshahara wa mbunge ni 2.3 ml(basic) plus 5ml posho ya ubunge makes 7ml kwa mwezi gross kabla ya kodi.
Graduate aliyeajiriwa serikalini analipwa 0.4 ml mpaka 0.6 ,kusema sitting allowance ifutwe wakati kwa watumishi wa umma hilo nafikiri siyo sahihi kwani lipo kwenye kanuni za kudumu(standing orders) za utumishi wa umma.

Watu kama wanasheria ambao sehemu kubwa ya kazi zao zinahusisha vikao then you say posho hiyo ifutwe ambayo kimsingi siyo kwamba watumishi wote wa umma wanalipwa hiyo , huo ni ubinafsi on the side of wabunge kwani ukifanya-comparative analysis utaona kuna tofauti kubwa ya mbunge na mtumishi wa umma kimapato.

Shame on Zitto et al , msiweke siasa kwenye maisha ya watu ,kuna matatizo makubwa katika nchi hii ambayo kama yakipatiwa majawabu sahihi effect yake ni ya mara moja na inayoonekana.
 
Wayne na kwa watetezi wa uovu wameshalaaniwa na taifa. Mithali 24:24 " Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia."
 
Wayne na kwa watetezi wa uovu wameshalaaniwa na taifa. <em><strong>Mithali 24:24 " <span style="color:#0000cd;">Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia."</span></strong></em>
 
Back
Top Bottom