Alliance Global in Motion siyo DECI nyingine?

Alliance Global in Motion siyo DECI nyingine?

Wanajamvi,

Kama mjuavyo Tanzania tunaishi kwa matukio, kuanzia kikombe cha babu, Deci, D9 Club, Mayai ya kware, Kilimo cha green house, Ufugaji wa Sungura na sasa Alliance Global in Motion.

Nimeleta hii mada kwa sababu kila mtu unayekutana naye sasa hivi mtaani atakueleza ni namna gani unaweza kuwa tajiri ndani ya mwaka mmoja kwa kujiingizia kitita kisichopungua million mia moja thelathini.

Nikiangalia maelezo ya wahusuka bado naona PYRAMID ndani yake. Kwani kwa kuanza unapaswa kutoa kiasi cha laki tano na zaidi, unapewa bidhaa, alafu unatafuta watu wawili ambao nao watajiunga kwa kiasi hicho hicho, hapo wewe ambaye ni memba mkuu unapata elfu 34 kama gawio toka kwa kila mwanachama.

Maelezo ni mengi na trend inaenda mpaka makundi 16, Swali wana jamvi hii kitu vipi? siyo deci nyingine hii? Wenye uelewa na hii kitu hepu leteni data hapa ili kama kunafaida watu wapige hela ila kama ni Deci 2 watu wachukuwe tahadhari.

Nawasilisha.
Siyo DECI wala sio Ponzi

DECI iliiuwa toa pesa upate pesa wao wakisema unapanda mbegu. Ponzi Ni toa pesa upate pesa

Allison in Motion Global ni toa hela upate virutubisho lishe na hivyo watu wanatumia na wanapata afya njema wenye changamoto za afya....na pia watu wanajipatia pesa kupitia virutubisho hivyo. Ukitaka kujua zaidi nipigie 0767233658
 
Hawa jamaa walikuja MOSHI na Arusha wakanipigia simu kwamba wanaendesha workshop mahali nikaenda ila nilishangaa mnapofika wanaanza kujitambulisha kuwa kuna wanafunzi wa vyuo wamekuwa millionaires baada ya kujiunga nao. Nikauliza wakasema kujiunga ni sharti ulipe 560,000 alafu watakutumia bidhaa ndani ya wiki. Kibaya zaidi hawatoi receipt wala bank account na badala yake unampa MTU cash bila documents yeyote. Office hawana ila wanasema office yao IPO dar maeneo ya makumbusho. Nimekimbia ila simu zao utazikimbia maana kila SAA wanakupigia

Hii 2019 kila kitu kiko sawa....makao makuu ya Alliance in Motion Global Tanzania yapo Mikocheni. Unalipa pesa unapewa virutubisho lishe pamoja na receipt ya EFD.

Kila siku huwa tunafanya biashara za network marketing lakini hatujui!

Ukitaka kujua zaidi nipigie +255767233758
 
Bora utumie hvyo virutubisho tu mpka viishe ila co laki 5 kwa 34k

Naona humu wapo wa kufanya profit sharing ndyo mana wanakupa elimu nzuri tu

Kazi hii ni nzuri sana kama utapata mgonjwa ambaye atapona kupitia hizo dawa Mana atajiunga chapu sana kukuinua wewe

ila sisi tunao ringia kiburi Cha uzima ni ngumu sana kujiunga


Cc.mwenyebikra yake
 
Tatizo la hawa jamaa bidhaa/suppliment zao ni hovyo hazina ubora kabisa. Efficacy yake ni zero. Ukitumia ni kama umekula mtama au mbege tu.
 
Back
Top Bottom