Akizungumza katika Mafunzo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa leo Agosti 18, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Shaban Itutu amelalamikia kile alichodai ni unyanyasaji wa Polisi dhidi ya wagombea wa upinzani wakati wa kampeni, akisema baadhi yao hukamatwa bila sababu za msingi.
“Polisi wamekuwa wakitusumbua kwenye kampeni. Wakiona mgombea ambaye hatokani na dola, mara moja anakamatwa. Tulishaomba hata kwenye mikutano kama hii na wao wawepo ili wajifunze kuwa kazi yao si kuwatisha wanasiasa,” ameongeza.