Muhindi mmoja katoka tembelea wakwe zake tanga ambao pia walimpa zawadi ya mbuzi 2 na bata 4 arudi nao mjini. Wakati anarudi na gari yake njiani akasimamishwa na trafiki, wakakagua gari wakakuta fresh ila wakaamua kumtania tu
Trafiki: mzee hawa mbuzi na bata ushawakamilishia taratibu za uhamiaji? Wana vitambulisho vya uraia kweli?
Muhindi: aaah afande, hapana anzisha mambo za shariya bhana! shika hizi elfu hamsini achia mimi pita, wakati wanaandikisha zilikuwa machungani nitaenda kuziandikisha mimi nikifika.
Na bila aibu trafiki wakalamba kweli zile hela!