Aliyeshindwa ubunge kuvunja chungu

Aliyeshindwa ubunge kuvunja chungu

Haaa haaa kwahiyo Chungu kikivunjwa mwanae ataondoka ?????.

Monaban ametoa chozi, walimuhakikishia yeye aongee vizuri na watu, Lodi Lofa anakuja kumalizia kwa mkono, jumapili ucku wamekesha ccm mkoa wanaimba ccm mbele kwa mbele, wakijua ya Kwa Kafulila yanatokea Arusha maana Lodi Lofa alisema Atatangazwa Monaban haijalishi kapata kura ngapi, alipo ona sura za watu wa chuga na walivyojazana pale njiro ucku wa manane kulinda kura Lodi lofa aliondoka bila kuaga Monabana kusikia lema katanfazwa chozi likadondoka hamuoni lodi lofa wa mzee wa bao la mkono, hasira anamalizia kwenye vyungu, imekula kwake mpaka mwanae amekula hela ya babake.
 
Uchaguzi mdogo umemalizika mgombea XYZ kashindwa kunyakua ubunge baada ya kumwaga mifedha kibao,alianzisha vikundi vya vijana na kina Mama fedha zilitolewa kwaajili ya kuanzisha miradi ya kiuchumi,alitoa viroba vya unga wenye njaa wakapona na njaa zao,alitumia karata ya ukabila haikufua dafu.Iweje kura hazikutosha hakuna namna lazima chungu kivunjwe wale wote waliotafuna fedha za mgombea na kura hamkutoa jiandaeni kupuputika kama majani makavu.

Haiwezekani mtafune fedha za mgombea XYZ halafu kura mkampigie mgombea ABC hakuna namna safari hii lazima mkomeshwa mjifunze kutunza ahadi mchana hadi usiku.Mifuko iliyojaa unga mlichukua ili mpate nguvu za kupiga kura bila makosa wengine hamkufika hata vituoni kupiga kura maana yake nini kama si dharau wakati wa kukomesha tabia mbaya ya kula vya watu bila fadhila wala uchungu ndio huu.

Tangazo hili ni sehemu ya taarifa rasmi kabla chungu hakijavunjwa wale wote walioshiriki kutafuna fedha na mgombea heshima wajitokeze watubu,wajiapize kutokurudia tena makosa yao yasiyosameheka.Mji umetaharuki wapiga kura wanapenda maisha yao kitisho cha kuvunjwa chungu kimewatia kiwewe X-MASS na Mwaka mpya si muhimu tena nguo hazinunuliwi,mbuzi wa sikukuu hanunuliwi kwa hofu ya kufanywa kitowewo cha misiba.

Yarabi tunusuru maisha yetu yapo hatarini.

Nawasilisha.

Vya Mollel tumekula na chungu kipasuke tu hatuogopi,hatukumuomba sembe katupatia mwenyewe
 
mambo ya kuvunjiana vyungu, peleka uswazi, huku bara hizo issue hazipo
 
Haaa haaa kwahiyo Chungu kikivunjwa mwanae ataondoka ?????.
Ndio manake mkuu Ngongo, dogo alikuwa anapewa hela awape vijana anawanunulia pombe wanakunywa wote, yey analipa bili za nyama na pombe, so mwanane chungu kina muhusu.
 
jana mchana alikua anakula nyama carwash kwa sunda na prof majimarefu......yani alikua mpweke kma kuku mwenye kideri

Inaelekea maji marefu kaja kutubu, ndumba zake hazija msaidia kuupata ubunge, jamaa kachezea hela kweli kweli.
 
Inaelekea maji marefu kaja kutubu, ndumba zake hazija msaidia kuupata ubunge, jamaa kachezea hela kweli kweli.

mzee anastress naskia aliambiwa hana ubavu wa kua mbunge akasema pesa ndio itaongea sasa wa2 wamekula hela n ubunge kakosa....labda kamleta majimarefu kuvunja chungu
 
Ngongo, tokea lini Arusha mkawa washirikina wa kufikia level hii??? Na je, kwa wale ambao walikura hela na kutimiza ahadi zao kwa kumpigia kura watapongezwaje? Au nyie mnajua kulaumu tu kupongeza hapana?
 
Last edited by a moderator:
Kuvunja Chungu ni Ibada ya matambiko ya kimila ya jamii nyingi za kiAfrika zikilenga kutanzua tatizo au kulipiza kisasi bada ya kufanywa jambo/mambo ya uonevu.

Shetani ashindwe kwa jina

La Yesu Kristo wa Nazareth!
 
Hakuna namna nimeshaiweka nyumba yangu na kigari changu mkweche sokoni nitumbue raha kabla dhahama haijanifika.
Poleni lakini wana arusha arumeru na moshi mumefanya maajabu kuonyesha kwamba fedha si mali kitu bali utu
 
Huu si uchawi ni aina ya mitambiko ya jamii ya kimaasai kama umefanya jambo baya labda umeua haujaonekana au hakuna ushahidi wa kukutia hatiani.Wazee wa kimila jamii ya kimaasai Malaigwanani wataitisha mkutano na kutangaza nia ya kuvunja Chungu sababu itawekwa wazi,waliohusika watatakiwa kujitokeza na kurejesha kitu kilichoibiwa labda ni Mbuzi au Kuku.Chungu hakivunjwi bila kutangaza hilo ni sharti la kwanza kabisa.

Mfano nimewahi kuona matangazo ya kusudio la kuvunja Chungu likiwa limepata baraka za Mwenyekiti wa Kitongoji na kubandikwa sehemu mbali mbali ili wahusika walisome na ikiwezekana wajitathimini na pengine waombe msamahaa kwa mujibu wa mila au itakavyoamuliwa na muathirika wa sakata hilo.

Tukirejea kwa mgombea XYZ sijamtaja jina mpaka sasa kwakuwa hili jambo ni nyeti sana ,kama umekula fedha zake na umempigia kura hapo hakuna madhara kabisa shida ni iwapo umekula fedha zake kura ukampigia mtu mwingine au haukwenda kupiga kura kabisa.

Ngongo, tokea lini Arusha mkawa washirikina wa kufikia level hii??? Na je, kwa wale ambao walikura hela na kutimiza ahadi zao kwa kumpigia kura watapongezwaje? Au nyie mnajua kulaumu tu kupongeza hapana?
 
Chungu sio kitu Ya mchezo, kama atavunja twafaaa unga hata Mimi nilipata na nkapeleka na nyumbani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom