Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,198
- 37,526
Uchaguzi mdogo umemalizika mgombea XYZ kashindwa kunyakua ubunge baada ya kumwaga mifedha kibao,alianzisha vikundi vya vijana na kina Mama fedha zilitolewa kwaajili ya kuanzisha miradi ya kiuchumi,alitoa viroba vya unga wenye njaa wakapona na njaa zao,alitumia karata ya ukabila haikufua dafu.Iweje kura hazikutosha hakuna namna lazima chungu kivunjwe wale wote waliotafuna fedha za mgombea na kura hamkutoa jiandaeni kupuputika kama majani makavu.
Haiwezekani mtafune fedha za mgombea XYZ halafu kura mkampigie mgombea ABC hakuna namna safari hii lazima mkomeshwa mjifunze kutunza ahadi mchana hadi usiku. Mifuko iliyojaa unga mlichukua ili mpate nguvu za kupiga kura bila makosa wengine hamkufika hata vituoni kupiga kura maana yake nini kama si dharau wakati wa kukomesha tabia mbaya ya kula vya watu bila fadhila wala uchungu ndio huu.
Tangazo hili ni sehemu ya taarifa rasmi kabla chungu hakijavunjwa wale wote walioshiriki kutafuna fedha na mgombea heshima wajitokeze watubu,wajiapize kutokurudia tena makosa yao yasiyosameheka.Mji umetaharuki wapiga kura wanapenda maisha yao kitisho cha kuvunjwa chungu kimewatia kiwewe X-MASS na Mwaka mpya si muhimu tena nguo hazinunuliwi,mbuzi wa sikukuu hanunuliwi kwa hofu ya kufanywa kitowewo cha misiba.
Yarabi tunusuru maisha yetu yapo hatarini.
Nawasilisha.