Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
GIZA nene limetanda juu ya mahali alipo mshitakiwa namba moja katika kesi ya kusafirisha wanyama hai nchini Qatar, Kamran Ahmed.
Mshtakiwa huyo jana alipaswa kuwepo mahakamani ambako inasikilizwa kesi yake lakini hakutokea kwa mara ya tatu.
Juzi kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi, Simon Kobelo, iliahirishwa baada ya mshitakiwa huyo kutotokea mahakamani bila taarifa yoyote.
Wakili wa Ahmed, Edmund Ngemela na wadhamini wake nao hawakutokea hivyo mahakama ilitoa hati ya kukamatwa mshitakiwa huyo.
Hata hivyo licha ya mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa mshatikiwa huyo, jana pia Ahmed hakufika mahakamani bila taarifa zozote.
Kutokana na mshtakiwa huyo kutofika mahakamani hapo kwa mara ya tatu, upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Evetha Mushi, ulidai unafuatilia anwani za wadhamini wake.
Mushi, alidai wadhamini hao hawafiki wala kutoa taarifa mahakamani juu ya mtu waliyemdhamini.
Hakimu Simon Kobelo, aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 17, mwaka huu na kama mshtakiwa Kamran Ahmed, atakuwa amepatikana itaanza kusikilizwa mfululizo Mei 6 na Mei 7.
Ahmed na wenzake watatu Martin Kimath, Michael Mrutu na Hawa Mang'unyuka wanadaiwa kusafrisha wanyama hao hai Novemba 26, mwaka 2010 kwenda Qatar kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Wanyama wanaodaiwa kukamatwa maeneo ya Mto wa Mbu, Elboret na Engaruka Wilaya ya Monduli mkoani Arusha .
Chanzo: Tanzania Daima la leo (26/3/2014)