Aliyemteka MO Dewji ni nani?

Hujufa hujaumbika. Majumba makubwa usitiri mambo. Ziumiazo ni nyasi fahari wa wawili watifuanapo.
Acha tu nawaza huyu dereva taxi atapewa fidia gani kwa atahri itakayokua imepatikana kwake na kwa familia
 
Nyongeza gani hiyo kama nazi kwenye supu bwana?! Kwahiyo kila unsolved crime ikiungwa hapo itakuwa sawa!
Ngoja nikuulize kitu, hivi lengo la mtoa mada ni kutaka kutujuza kuchiwa kwa dereva aliye shutumiwa kumteka huyo Moo, au ni kushangazwa kwake kwa wahusika hasa wa hilo tukio kutotiwa nguvuni?

Kama akili yako inawaza tu kuachiwa kwa huyo dereva, basi uko sahihi kunishangaa! Ila kwa ambaye atajiuliza iweje wahusika hasa wa hilo tukio, kutopatikana mpaka leo, basi utaelewa ni kwa nini nimeuliza hilo swali.
 
Swali la nyongeza; Hivi walio mshambulia huyu mwamba Tundu Lissu kwa mvua ya risasi, tena mchana kweupe kule Dodoma! ni akina nani? Maana tokea 2017 mpaka leo, polisi na Serikali ya ccm wanatoa majibu mepesi mepesi tu!
Tatizo la vyombo vyetu... Matukio ambayo ni so obvious kama hayo ya MO na Lissu intelijensia yao inayashindwa kabisa. Ila yale mengine ya chini chini kama ya kina Mbowe wanayawezea kweli kweli.
 
images (77).jpeg
 
Ngoja nikuulize kitu, hivi lengo la mtoa mada ni kutaka kutujuza kuchiwa kwa dereva aliye shutumiwa kumteka huyo Moo, au ni kushangazwa kwake kwa wahusika hasa wa hilo tukio kutotiwa nguvuni?

Kama akili yako inawaza tu kuachiwa kwa huyo dereva, basi uko sahihi kunishangaa! Ila kwa ambaye atajiuliza iweje wahusika hasa wa hilo tukio, kutopatikana mpaka leo, basi utaelewa ni kwa nini nimeuliza hilo swali.
Mkuu, swali liko wazi ila wewe ni kama umeingia kwenye mtihani na majibu yako ndio maana unataka swali linyooshwe ku-fit majibu yako.

Angalizo: Majibu ya swali lako la nyongeza yanaweza yasiwe majibu la swali la msingi hapo juu.
Mo yupo lakini kimya, kunani?!
 
Wadau mtakumbukwa MO Dewji mfanyabiashara mkubwa nchini alitekwa tarehe 11 Oktoba 2018 na kupatikana tarehe 20 Oktoba 2018

Baada ya kupatika Polisi walidai wamemkamta dereva taxi kuwa ndiye aliyemteka mo dewji

Kesi hiyo haijawahi kusikilizwa mahakama zaidi ya kuiahirisha tu.

Juzi Mahakama ya Kisutu imemwachia huru mtuhumiwa huyo na kuacha maswali mengi kama

1. Kwanini polisi walisema dereva taxi ndio alimteka mo?

2. Kama mtekaji sio huyo dereva taxi kwanini alishtakiwa?

3. Nani alimteka mo?

4. Au mo dewji hakutekwa?

View attachment 1870261
Mbona unauliza swali lililo na jibu unalijua.
Hata polisi , Mambosasa alikuwa anajiuma uma kutoa maelezo.
Mwendazake!
 
Ina maana na wewe ni mingoni wa waliodhani kuwa huyo Dereva kweli ni Muhusika.

Mimi kilichonishtua ni kuona kumbe bado alikuwa ndani mpaka wa leo, kwa hesabu zangu nilijua baada tu ya Mwendawazimu kupita kombe lingefunuliwa maisha yaendelee...yaani wangeshamuachia kitambo.
 
Back
Top Bottom