Aliyempigisha ‘deki’ Mwalimu aigomea CWT

🙁🙁 KIKI~JF
 
Nasikitika Mkurugenzi kumdhalilisha Mwalimu lkn nasikitika zaidi huyo mwalimu tena wa kiume kukubali kudhalilishwa .......
 
Kishaona dalili ya kutumbuliwa huyoooo,anajifanya naye mungu mtu.Daaaahhh hua naskiaga vibaya mno kuona mwalimu akionewa au kudhalilishwa,tunajisahau sana wakati hao ndo walez na wasimamiz wa taaluma zetu
Mtumishi mbabe, Dikteta na mnyanyasaji kama huyo usitarajie Kuwa atatumbuliwa,.. Haiwezekani! Hapo asubiri kupandishwa cheo tu.. Mkulu hatumbui watu wenye tabia zinazofanana na za kwake, katumwa huyo!
 
Vitu vingine ni kujitakia tuu, Niko kazini eti mkurugenzi aniambie nideki wakati hilo halipo kwenye masharti ya kazi yangu! Labda akamlete mke wake ndio adeki.
Hapo kwa kulinda utu wangu hata awe ngosha mwenyewe halitokei labda itumike nguvu ya kijeshi
 
muda mwingne nataman nihamishiwe sayar ya mars kw muda ili nisiweze kusikia mambo yanayotokea apa kwetu.! maana ni aibu kuyasikia,kuyaona na kiyaishi.!!
Mimi natamani niwe nakutana na watu kama huyo Mkurugenzi halafu nimuoneshe kuwa ninaweza kuingia kwenye historia ya nchi.
 
Laiti ndo ningekuwa Mimi naambiwa kudeki aisee pangechimbika aaa Liwalo na liwe bwanaa.
 
WALIMU wanafanyiwa figisu figisu sana na hii ni kutokana na utegemezi wa ajira kwa ajili ya kuendesha maisha. pengine huyo mwalimu alikuwa na option mbili ya kwanza ku react kwa kumtia vichwa au kumtukana aliyempa amri ya udhalilifu ya pili ni kuvumilia na kutekeleza kwakua matokeo ya kuchukua option ya kwanza ni kuitesa familia inayokutegemea. ubongo ukachambua haraka na ukaamua kuchukua option ya pili. lakini ninahakika aliumia sana moyoni. yaani sijui ningekua mimi hapo labna wangeniscopion tu maan ningepigana tu. potelea mbali. Hongera mwalimu umeshinda hasira ambazo hupelekea kumuas Muumba wetu.
 
walimu enzi ya Mwl waliheshimika sana kwa sasa siyo tu hawaheshimiwi tena bali wana hali ngumu heri bi mkubwa wangu umestaafu hawa masadisti wameshasahau walipotoka shenz type
 
wengine hapa wanaweza kuwa wanangea kimzahamzamzaha but serious speaking ningekuwa mimi labda alete jeshi na si kwa kudeki bali anichukue kwa karandinga kunako majengo ya serikali

Lakini pia najiuliza tu kwa sauti hivi huyo mwl angekataa huyo mkurugenzi angemfanyia nn???
 

Kwa michango ninayoina hapa, kutoka kwa wachangiaji na wale wanaodai kuwatetea walimu, na kama kuna walimu kati yao au kama ni kweli CWT wamefanya hivyo, ni dhahiri kwamba walimu hawajielewi kama wachangiaji wake.

CWT kama ndio watetezi wa walimu basi walimu wameliwa.

Sitegemei mtu mwenye ufahamu wake arespond kwenye mchakato unaoendeshwa bila weledi kama huu.

CWT hawana mamlaka yoyote kisheria ya kutoa adhabu kwa Mkurugenzi wa maendeleo.

Ni aibu kuona chombo kama hicho kinachukua hatua za kimbrura kama waliosikia kuna mumiani shambani wakaenda kuua kumbe ni watafiti.

Jamii ya wasomi inapashwa kkujitofautisha na kundi la miburura ii kuonyesha njia sahihi na thamani ya elimu.

Asomaye na afahamu.

Wale wasioelewa naomba msijibu kwa sababu hamna uwezo wa kuelewa hoja yangu hata nikiwaambia. Ila wenye ufahamu wanajua ninachomaanisha.
 
Nasikitika Mkurugenzi kumdhalilisha Mwalimu lkn nasikitika zaidi huyo mwalimu tena wa kiume kukubali kudhalilishwa .......
 
Mwalimu alikubali vipi kupiga deki...tena mbele ya wanafunzi wake!? Hizi nidhamu za uoga ni upuuzi.

CWT sasa wajifunze na wawaambie walimu wao wasiwe wanakubali kutumika kwa vijiallowance kiduchu wakati wa campaign.
 
Mie nawashangaa sana waalimu wa nchi yangu nimda mrefu sasa wamekuwa mnadhalilishwa na viongozi wa serikali yenu lakini sioni juhudi zao za kujitoa kwenye unyonge huo nashindwa kuwashauri maana naona mmekwama mahali pamoja na wingi wenu hanjui cha kufanya shauri yenu
 
Daaah inauma sana, ningekuwa mie nisingefanya upuuzi huo
 
Huyu mkurugenzi anatafuta umaarufu kwa kutembelea nyota ya mwalimu aliyepigishwa deki! Maskini Tanzania yangu tumekukosea nini! Daah! Inauma sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…