Aliyempigisha ‘deki’ Mwalimu aigomea CWT

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
ELIUD Mwaiteleke, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, aliyeamuru Hamis Sengo, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Shilala kudeki darasa mbele ya wanafunzi ‘amekitolea nje’ Chama Cha Walimu (CWT) mkoani Mwanza baada ya viongozi wake kutaka kumuona na kumtaka aombe radhi.

Tukio la mkurugenzi huyo kumdhalilisha mwalimu huyo mbele ya wanafunzi wake, lilitokea Oktoba 17, mwaka huu shuleni hapo, baada ya ‘bosi’ huyo wa halmashauri kukuta baadhi ya madarasa yakiwa machafu.

Mkurugenzi Mwaiteleke akiwa ameambatana na maofisa wengine wa serikali ngazi ya wilaya hiyo, alifika shuleni hapo majira ya jioni na kumuita mwalimu (Sengo) ili aeleze kwanini madarasa ni machafu na kumtaka kudeki kitendo kilichotekelezwa na mwalimu huyo bila kupinga.

Sibora Kisheri, mwenyekiti wa CWT mkoani hapa amesema kuwa wamelipokea tukio hilo kwa masikitiko na kwamba wamemtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi bila mafanikio.

“Tumefanya mazungumzo na tukaazimia kumtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi na kumhamisha mwalimu huyo shuleni hapo kwa gharama zake na asifanye kitendo hicho kwa mwalimu mwingine.

Endapo mkurungezi huyo atashindwa kutekeleza maagizo hayo, tutachukua hatua kali zaidi kwani tumechoka kuonewa na viongozi wa serikali kila kukicha.

Kisheri amesema kuwa viongozi wa CWT walienda kuonana na mkurugenzi huyo lakini hakutaka kuonesha ushirikiano kwao na alidai kwamba leo anasafiri hawawezi kuonana na sisi.

“Mkurugenzi ni msimamizi wa watumishi lakini tunashangaa kuona kiongozi kama huyo anageuka kuwa mnyanyasaji na viongozi wasidhani kama sisi ni wanyonge, tunaweza kuchukua maamzi magumu zaidi ya hayo,” amesema Kisheri.

Alipopigiwa simu yake zaidi ya mara tano, ilikuwa ikiita na kukatwa lakini baadae ilipokelewa na mkurugenzi huyo kumtaka mwandishi kuwa yupo barabarani na hawezi kuzungumzia suala hilo.

Mkurugenzi: Nipo barabarani, sikusikii vizuri ni tukio gani?

Mwandishi: Ni tukio la kumuamuru mwalimu kudeki darasa ulilolifanya Oktoba 17.

Mkurugenzi: Ngoja nikutumie namba za afisa habari wa wilaya (Misungwi) atakueleza suala hilo.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Kishaona dalili ya kutumbuliwa huyoooo,anajifanya naye mungu mtu.Daaaahhh hua naskiaga vibaya mno kuona mwalimu akionewa au kudhalilishwa,tunajisahau sana wakati hao ndo walez na wasimamiz wa taaluma zetu
 
Na mwalimu nae jamani, mbona anakuwa muoga hivyo? Au ana vyeti feki? Kwani angekataa? Maana najua hata wangetunishiana misuri, mbele ya mahakama haki ingetendeka tu. Halafu bado tunawaza kuja kuwa na kizazi cha free thinkers? Kwa aina hii ya uoga wa walimu? Mungu aiingilie kati.
 
Vitu vingine vinauma sana..mwalimu nae ikabidi atii tu masikini..
 
muda mwingne nataman nihamishiwe sayar ya mars kw muda ili nisiweze kusikia mambo yanayotokea apa kwetu.! maana ni aibu kuyasikia,kuyaona na kiyaishi.!!
 
Mhh jamani mbona mnawanyanyasa walimu? Kilio chao nani anakisikiliza?

Pole ziwaendee walimu wote
 
ELIUD Mwaiteleke, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, aliyeamuru Hamis Sengo, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Shilala kudeki darasa mbele ya wanafunzi ‘amekitolea nje’ Chama Cha Walimu (CWT) mkoani Mwanza baada ya viongozi wake kutaka kumuona na kumtaka aombe radhi.

Tukio la mkurugenzi huyo kumdhalilisha mwalimu huyo mbele ya wanafunzi wake, lilitokea Oktoba 17, mwaka huu shuleni hapo, baada ya ‘bosi’ huyo wa halmashauri kukuta baadhi ya madarasa yakiwa machafu.

Mkurugenzi Mwaiteleke akiwa ameambatana na maofisa wengine wa serikali ngazi ya wilaya hiyo, alifika shuleni hapo majira ya jioni na kumuita mwalimu (Sengo) ili aeleze kwanini madarasa ni machafu na kumtaka kudeki kitendo kilichotekelezwa na mwalimu huyo bila kupinga.

Sibora Kisheri, mwenyekiti wa CWT mkoani hapa amesema kuwa wamelipokea tukio hilo kwa masikitiko na kwamba wamemtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi bila mafanikio.

“Tumefanya mazungumzo na tukaazimia kumtaka mkurugenzi huyo kuomba radhi na kumhamisha mwalimu huyo shuleni hapo kwa gharama zake na asifanye kitendo hicho kwa mwalimu mwingine.

Endapo mkurungezi huyo atashindwa kutekeleza maagizo hayo, tutachukua hatua kali zaidi kwani tumechoka kuonewa na viongozi wa serikali kila kukicha.

Kisheri amesema kuwa viongozi wa CWT walienda kuonana na mkurugenzi huyo lakini hakutaka kuonesha ushirikiano kwao na alidai kwamba leo anasafiri hawawezi kuonana na sisi.

“Mkurugenzi ni msimamizi wa watumishi lakini tunashangaa kuona kiongozi kama huyo anageuka kuwa mnyanyasaji na viongozi wasidhani kama sisi ni wanyonge, tunaweza kuchukua maamzi magumu zaidi ya hayo,” amesema Kisheri.

Alipopigiwa simu yake zaidi ya mara tano, ilikuwa ikiita na kukatwa lakini baadae ilipokelewa na mkurugenzi huyo kumtaka mwandishi kuwa yupo barabarani na hawezi kuzungumzia suala hilo.

Mkurugenzi: Nipo barabarani, sikusikii vizuri ni tukio gani?

Mwandishi: Ni tukio la kumuamuru mwalimu kudeki darasa ulilolifanya Oktoba 17.

Mkurugenzi: Ngoja nikutumie namba za afisa habari wa wilaya (Misungwi) atakueleza suala hilo.
Hayo aliyofanya ni maagizo kutoka juu kwa aliemteua.

Hii ndo picha halisi ya serikali ya chama cha mapinduzi
 
Kumdhalilisha mwalimu haikubaliki kabisa, kama anadharaulika ni bora kuliko udhalilishaji.

Huwa najiuliza always hivi huyu mkurugenzi angeweza kufanya kitendo kama hiki kwa mwalimu aliyewahi mfundisha?
 
Hawa waalimu uchagua CCM, ni muda wa kujitambua sasa.
 
dunia ni mapito sote tutakufa na tutaiacha2
acheni tudharauliane maana Mungu aliyaumba na hayana budi kuwepo lakini sote mwisho wetu ni kaburini.
 
Bado sinema ya serikali ya awamu hii na walim inaendelea inauma sana jamani
*Walimu, Walimu, kwa nini kila siku udhalilishaji wa walimu,
Hivi huyu Mh. bila Mwl. wake angekuwa na cheo Kama hicho
 
Back
Top Bottom