fundibaskeli
Member
- Nov 9, 2016
- 84
- 115
Waziri Mkuu wa zamani Mheshimiwa Edward Lowassa amekamatwa na Polisi mkoani Geita. Mh. Lowassa amefika Geita leo akitokea Kagera kwenye ziara, alipofika stendi ya zamani Geita wananchi wakamsimamisha. Aliposhuka kwenye gari kuwasalimu wanageita, polisi wakamkamata na kumpeleka kituo cha Polisi Geita.
Mpaka sasa hajaelezwa kosa lake lililopelekea mpaka kukamatwa.
Vilevile Upendo Furaha Peneza ambaye ni Mbunge Viti Maalum CHADEMA amekamatwa, alikua kaambatana na Lowassa.
More updates.....
Pagan Amum anasema,
Waziri Mkuu mstaafu na aliyekuwa mgombea urais kwa CHADEMA Mh. Edward Lowassa na mbunge wa Geita (M) Viti maalum Upendo Peneza wamekamatwa Geita mjini. Kwa sasa wako kituo cha polisi...
Kosa ni Mh. Lowassa na Upendo kusalimiana na wananchi wakiwa njiani kuelekea katika kampeni kata ya Nkome, Geita vijijini
Ikumbukwe Ni siku ya Ijumaa Mh. Peneza alikamatwa na kuachiwa kwa dhamana, kwa kosa la kusema kuna njaa nchini, hivyo serikali ichukue hatua za haraka kusaudia wananchi. Leo kakamatwa tena. Na pia, siku hiyo hiyo Mh. Mnyika, Katambi na wengine 3 walikamatwa hapo hapo Geita Mjini
Taarifa zaidi zitaendelea kuja......
======
More updates:
> Wakati Lowassa anakamatwa, Mabomu ya machozi yalipigwa
> Inadaiwa kuna Waandishi walikamatwa pia
> Sasa hivi, saa 10:50 jioni, Lowassa kahamishwa toka kwa OCD kaelekea kwa RPC wa Geita.
Aachiwa: