Aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa ACT-Wazalendo, Kadawi Limbu, kugombea ubunge kupitia CHADEMA

Tumia akili kufikiri. Limbu ndie mwanzilishi wa ACT, atatumikaje na Chama Kingine kukiharibu chama alichokitolea jasho kukianzisha?

Au unataka kusema CDM walimtuma aanzishe chama kingine ili ikitokea baadae coincidence Zitto akatimkia huko ndio akiharibu chama?

vilaza wako wengi wala usishangae
 
Last edited by a moderator:
Kwanza chanzo cha habari hakieleweki,

Hata hivyo Chadema siyo sawa na ACT kuwa ukishachukua fomu tayari umeshakuwa mgombea,

Hata Zitto anaweza kuchukua fomu lakini hawezi kuwa mgombea wa Chadema.

Hiyo sio hoja heri angeenda chama kingine hata asipoteuliwa kugombea ubunge ni dhahir alitumwa kutuvuruga wazalendo!
 
Alienda ACT au alianzisha ACT? Au wakati ACT inaanzishwa kulitangazwa nafadi ya mwenyekiti kwa yeyote mwenye vigezo kuomba? Nakumbuka kabla ya ACT alisemekana kuwa chama kingine alichokianzisha! Hivi hakuwemo kwenye chama kilichoshindwa kuanza cha hakina Sitta na Nnauye?
Mkuu kwani kuna ubaya mimi kuishi Karatu?
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa ACT-Wazalendo, Kadawi Lucas Limbu amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Magu kwa tiketi ya CHADEMA.Hii ndio ahadi aliyokuwa ameahidiwa na CHADEMA.

Hivi ndivyo Chadema walivyokuwa wanaihujumu ACT-Wazalendo lakini walishindwa vibaya na ndio maana kila kukicha CHADEMA wako busy na kuishambulia ACT-Wazalendo.

Jiwe Limewapata.

Sasa CHADEMA wameumbuka.

Unaongelea magu ipi? hii niliyozaliwa au nyingine? Magu hatuna mgombea Wa aina hiyo?
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa ACT kadawi Lucas Limbu amechukuwa fomu kugombea ubunge kupitia Chadema limbu ndio Yule aliye kuwa akiendesha mgogoro ndani ya chama cha ACT-Wazalendo baada ya kuondolewa na Halmashauri kuu, ambapo alienda Mahakamani na kubwagwa vibaya.

Je? Ndugu wadau huyu hakuwa anatumika na Chadema?

Maana Shukurani aliyopewa ni kugombea jimbo la magu? Kumbe alikuwa anaendesha migogoro ndani ya ACT huku ni mwana chama waCHADEMA.

Ameona ccm na Act are going to die completely a natural super death ! Well done Limbu!
 
Tumia akili kufikiri. Limbu ndie mwanzilishi wa ACT, atatumikaje na Chama Kingine kukiharibu chama alichokitolea jasho kukianzisha?

Au unataka kusema CDM walimtuma aanzishe chama kingine ili ikitokea baadae coincidence Zitto akatimkia huko ndio akiharibu chama?

Kweli nyani haoni kundule
 
Last edited by a moderator:
Hiyo siyo hoja kumbe ule mgogoro wa Limbu na ACT mlikuwa mmemtuma Limbu kuivuruga ACT - Wazalendo daah!!!.

Limbu kajiunga lini Chadema?


Kweli Chadema wameishiwa.

Kwani Zitto alijiunga lini ACT? Mbona hiki kilikuwa chama cha Limbu? Kweli CCM ina matawi mengi.
 
Na baada yamkumtuma kuivuruga ACT amerejea kwao. Ila CHADEMA walivyo na roho mbaya, wamemtumia tu kama condom na mwisho wa siku hawatampitisha kugombea ubunge

Kama CCM walivyomtumia Stella Mwampambwa na wenzake
 
Limbu hawezi kugombea ubunge kupitia CHADEMA kama kachukua fomu atakuwa ana gombea kupitia chama cha ACT ambacho alikianzisha mwenyewe.
 
Nimefuatilia kidigo suala la aliekuwa mweyekiti wa muda wa ACT ndugu Limbu
kwenda kugombea ubunge kupitia CHADEMA nimeshangaa sana

Ingawa ningependa kuamini kuwa CHADEMA haikuhusika na mgogoro wa ACT
au kuamini kuwa CHADEMA hawako bize kupambana na Zitto na ACT kuliko
kuwa bize na kupambana na CCM lakini hili linafanya watu wengi tujiulize maswali tele

swali kuubwa kuliko yote ni je CHADEMA ni tofauti kiasi gani na CCM?

na kama tofauti ya CHADEMA na CCM ni ndogo au hakuna hasa kwenye suala
la kufanya siasa chafu za 'kuwatumia' watu na 'kununua' watu ili kuleta fitina kwenye
vyama vingine....je kwa nini watu waiamini CHADEMA?

maswali ni mengi kwa kweli........
 
Back
Top Bottom